MOROGORO: Polisi inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za ubakaji na udhalilishaji wa mwanamke

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu kumi na mmoja kwa tuhuma za kumdhalilisha mwanamke mwenye umri wa miaka 21 kwa kumtishia kwa kisu,kumbaka na kusambaza picha za kudhalilisha za tukio hilo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao 11, ni pamoja na mmoja Idd Adam (32) mkazi wa Makambako mkoani Iringa,aliyehusika kumtishia kwa kisu ili abakwe na kumrekodi video binti huyo,na mtuhumiwa Zuberi Thabit (30) mkazi wa mbarali mkoa ni Mbeya aliyembaka binti huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Kamanda Mateo amesema watuhumiwa wengine tisa wakiwemo wanaume saba na wanawake wawili,wakazi wa dakawa mkoani Morogoro wanashikiliwa kwa tuhuma za kusambaza kwenye mitandao ya kijamii picha za utupu za tukio hilo la ukatili na udhalilishaji dhidi ya mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa ni mjamzito.

Wananchi wa mkoa wa Morogoro wamepokea kwa hisia tofauti tukio hilo la ubakaji na udhalilishaji wakitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa,huku wengine wakishauri ndugu jamaa na marafiki kuwa karibu na binti huyo ili kumfariji na kumshauri awe mvumilivu katika wakati huu mgumu kwake .
 
Idd Adam (32) mkazi wa Makambako mkoani Iringa,aliyehusika kumtishia kwa kisu ili abakwe na kumrekodi video binti huyo,na mtuhumiwa Zuberi Thabit (30) mkazi wa mbarali mkoa ni Mbeya


Kuna motive gani behind this
 
Wekeni hapa hiyo video
Muombe Manyerere Jackton, yy ndy alianza kuipost hii habari juzi kuwa kaletewa video ya tukio hilo na ndugu yake flani,
Nadhani atakua amewasaidia polisi maana kwenye uzi wake alitambua mpka guest house kulingana na mashuka ya hiyo guest yalivyoandikwa. Na akasema anahisi iko Dakawa.
 
Back
Top Bottom