Morogoro-Mangae: Waliouawa na tembo wafikia 16

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Ngalia Mihule(59) aliyekuwa mkazi wa Mangae, Mvomero mkoani Morogoro ameuawa na tembo na kufanya idadi ya waliuawa na tembo katika kijiji hicho kufikia 16.

Uvamiaji wa tembo katika kijiji hicho umekuwa janga kubwa wananchi wameomba serikali wawarudishe wanyama wao kwenye hifadhi ya Mikumi.

Uvamizi wa tembo mara kwa mara katika Kijiji hicho unafanya watoto washindwe kwenda shule na wananchi kuwa na hofu ya kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinus Bandio amewataka TAWA walifanye kazi kwa kuwa wao ndio wanaoshughulika na wanyama walio nje ya Hifadhi.
 
Back
Top Bottom