ACT Wazalendo yataka hatua za haraka kukabiliana na Tembo

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
322
255
Akizungumzia Kadhia ya Wanyama aina ya Tembo kuvamia makazi ya wananchi katika maeneo mbali mbali ya Tunduru mkoani Ruvuma Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Zitto aliitaka serikali,kuchukua hatua za kukabiliana na matukio ya Tembo kuvamia vijiji hali kwa kile alichoeleza hali hiyo inatishia usalama wa watu na uhakika wa chakula nchini.

Alisema mbali na serikali kuchukua hatua ni muhimu pia itoe fidia(kifuta jasho na machozi)kwa uharibifu unaofanywa na Wanyama hao katika maeneo mbali mbali nchini kwa kuangalia hali halisi ya Maisha kwa mujibu wa sheria wakati hatua zingine zikiendelea

Aliongeza kuwa kumekuwa na vilio vya wananchi wa Ligunga na maeneo mengine yanayozungukwa na hifadhi ya wanyama ya Selous kutokana na kuibuka kwa kasi wimbi la uvamizi wa Tembo kwenye makazi ya watu

“Idadi ya matukio na vijiji vinavyovamiwa na tembo inazidi kuongezeka kila uchao nchini, juzi tumesikia Nachingwea kuna hatari ya njaa kutokana na mashamba yao kushambuliwa na Tembo. Hapa Tunduru tumerekodi matukio ya mara kwa mara ya athari za Tembo wapo wananchi waliopoteza maisha, waliojeruhiwa na kupoteza mali zao,”alisema Zitto Kabwe

Aliongeza kuwa ACT Wazalendo kupitia kwa Katibu Mkuu wake Ado Shaibu iliitaka Serikali iwajibike kwa kufanya utafiti wa kina kujua kwanini kuna ongezeko kubwa la mtukio ya tembo kutoka Mbugani kuvamia Vijiji,pamoja na kuongeza udhibiti wa matukio hayo kupitia idaraa ya Wanyama Pori

Aliwataka wananchi kuungana na chama hicho kuishinikiza serikali kuchukua hatua za kunusuru athari zaidi za Wanyama hao kwa kuiwajibisha serikali kama ambavyo chama hicho kinafanya.

“Sisi tunaitaka Serikali itoe fidia (vifuta jasho na machozi) ya uharibufu unaofanywa na wanyama hao kwa kuangalia hali halisi ya maisha kwa mujibu wa Sheria wakati hatua zingine zikiendelea, ni jambo la kushangazwa sana kuona Serikali haijali kabisa vilio vya wananchi wala kuchukua mapendekezo ya kuzima vilio na kufuta machozi yao.”alisema.

IMG_20221115_121955_101.jpg
 
Back
Top Bottom