kabisa mkuu"" halafu alikuwa nikijana Mdogo tu kwa wakati ule..lakini ni nunda mla watudah jamaa alisumbuaga moro huyo yaan walivomuua watu walipumua nasikia yule ndo alikua bosi wa majambazi pale moro
huko lukobe sasa hivi ni town watu wamejenga balaa yaan moro imebadilika sana.Namimi hii hapa, niliishi Moro mwaka 1993/4, Eneo la Mazimbo, kipindi hicho ni Poli tu kuanzia Mazimbu Kanisa Katoliki hadi Daraja la treni Tinge tinge karibu na Kambi ya Wakimbizi ya Mazimbu. Asubuhi Lukobe Shamba, kulima mpunga, jioni kumwagilia bustani za babu pembezoni mwa mto Ngerengere. Nilijifunza kulima miwa, choroko na kuvua Dagaa uduvi. Tukiamka mimi na dada zangu ni kwenda Kupanga foleni ndani ya Kambi za wakimbizi wa South Africa kuchukua mbao za kuni za kupikia nyumbani. Wakati mwingine wasimamizi wa Wakimbizi (UNHR), utufungulia Makontena tuchukue nguo na viatu, tukifika nyumbani tunauza. Mjini kati Moro kwenda mpaka sikukuu, Sisi tulikua wapori pori tu uko Mazimbu.
Standard 7 Bungo primary 1995Kuzaliwa kukua kusomea kazi ndo nilitupwa hukooo ila nimepamis mno saivi pamejengeka sana tofauti na miaka hiyo
Cc Smart911
Standard 7 Bungo primary 1995
1996-99 Kigurunyembe Secondary O-level
A-level 2000-2002 Forest Hill Secondary
Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
Nilihamia Dar,kwa Mama, Baada ya Elimu ndefu nikarudi Mwaka 2012/13, niliyoyaona, Nimeamini Maisha Safari. Watu sasa wapo Mkundi huko wanapolomosha manyumba, nilienda kuishi Bigwa na Misongeni.huko lukobe sasa hivi ni town watu wamejenga balaa yaan moro imebadilika sana.
Forest Hills watoto wa pateli au sio nawewe ni mwarabu nini make ndo wamejaa pale!Standard 7 Bungo primary 1995
1996-99 Kigurunyembe Secondary O-level
A-level 2000-2002 Forest Hill Secondary
Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
Mzee Baba, nyinyi wapambanaji mbona bado hamna maendeleo!?. Hujasikia Bill Gates anasema "Siku zote wavivu ndio Wabunifu"?. Maana hupenda kutafuta njia rahisi sana ya kutatua tatizo ili wapate Muda wa kula bata.Wavivu sana, wanapenda vigodoro,
Sema tu washukuru LAPF mfuko wa pension wamewajengea stand ya kisasa
ww umesoma mwere umemaliza mwaka gani mm nimesoma pale
sapna na shani cinema zilisha kufa zaman cjui kwa sasa hiviKatika vyote mi nakumbuka sinema shani cinema na sapna. Alafu pale maeneo ya mlapakolo kulikuwa na muuza chips mmoja alikuwa anaitwa Peter, yule jamaa alikuwa anachoma mishikaki ya hatari sana ingawa baadae akapata mpinzani aitwae Kabele kama sijakosea
dah kumbe juzi tu mm nilimaliza mwaka 2000.