Morogoro: Auwawa na mashemeji zake baada ya kushindwa kumalizia deni la mahari ya dada yao shilingi laki tano

Wakilipa cash lawama wanavunja undgu wakibakiza mnawaua

Wachague lipi
Maandiko katika kitabu kitakatifu cha Biblia exodus 22:6 - inakatazwa mahari isilipwe Kama mwanamke hakuwa bikira. Inatakuwa kulipwa Na Yule aliye mtoa bikra. Sasa Kama mwanamke mwenyewe alikuwa garasa tayari, hiyo mahari ilikuwa ya nini?
 
Ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nimeshindwa kujizuia kucheka japo simaanishi nimefurahi.R.I.P Mwamba.

Vijana mnaojiandaa kuoa kueni makini.
---
WATU wanne wa familia moja akiwemo Masele Machibya Masele (65) mkulima na mkazi wa Tabora wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kula njama na kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Itegete, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro ambaye alikuwa anadaiwa kushindwa kulipa deni la mahari ya Sh 500,000.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama ametoa taarifa hiyo ambapo amesema, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa Agosti mwaka huu katika kijiji hicho kilichopo wilayani Kilombero.

Mkama amewataja watuhumiwa waliokamatwa ni Masele Machibya Masele (65), mkulima na mkazi wa Tabora, Mwalu Ndama Hassan (18), Pawa Ndama Kema (16) na Rehema Masele (35), wote ni wakulima na wakazi wa kijiji hicho.

Amesema watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa walikula njama ya kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Itegete, ambapo kimsingi inadaiwa alikuwa ameshindwa kulipa deni la mahari.

“Hawa ni wafamilia moja, Masele Machibya Masele ni Baba mkwe wa marehemu, alitoka Tabora kuja kumdai mahari mkwewe, na hao wengine ni mke na watoto wa marehemu“ amesema Mkama

“Sasa walipoona huyo (Marehemu) amekuwa mkaidi muda mrefu halipi mahari na ameshapata watoto tayari waliamua kula njama na kumuua“ amebainisha Kamanda Mkama.

Nipashe
Mazuzu by nature
 
Screenshot_20230902-020500_Opera Mini.jpg
 
Hapo naona mdaiwa alikua anawajibu ujeuri sana kila anapodaiwa,uzalendo ukawashinda,sababu kuu ya kumuua sio mahari bali majibu yake yakifedhuli kwa wadai wake,

Kitu kingine kimenistaabisha pia ni watoto wa marehemu kuhusika kumuua Baba yao mzazi!
 
Ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 nimeshindwa kujizuia kucheka japo simaanishi nimefurahi.R.I.P Mwamba.

Vijana mnaojiandaa kuoa kueni makini.
---
WATU wanne wa familia moja akiwemo Masele Machibya Masele (65) mkulima na mkazi wa Tabora wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kula njama na kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Itegete, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro ambaye alikuwa anadaiwa kushindwa kulipa deni la mahari ya Sh 500,000.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama ametoa taarifa hiyo ambapo amesema, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa Agosti mwaka huu katika kijiji hicho kilichopo wilayani Kilombero.

Mkama amewataja watuhumiwa waliokamatwa ni Masele Machibya Masele (65), mkulima na mkazi wa Tabora, Mwalu Ndama Hassan (18), Pawa Ndama Kema (16) na Rehema Masele (35), wote ni wakulima na wakazi wa kijiji hicho.

Amesema watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa walikula njama ya kumuua Hassan Ngema (51) mkulima na mkazi wa Itegete, ambapo kimsingi inadaiwa alikuwa ameshindwa kulipa deni la mahari.

“Hawa ni wafamilia moja, Masele Machibya Masele ni Baba mkwe wa marehemu, alitoka Tabora kuja kumdai mahari mkwewe, na hao wengine ni mke na watoto wa marehemu“ amesema Mkama

“Sasa walipoona huyo (Marehemu) amekuwa mkaidi muda mrefu halipi mahari na ameshapata watoto tayari waliamua kula njama na kumuua“ amebainisha Kamanda Mkama.

Nipashe
Mambo yanazidi kunoga ukweni

View: https://twitter.com/Nipashetz/status/1698574664136568894?t=jXUjyPNwxIU5ATjUZsEXMw&s=19
 
Back
Top Bottom