Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Na Mwandishi Maalum
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Jumatano, Desemba 3, 2008 amekutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) cha Zimbabwe, Bwana Morgan Tsvangirai, Ikulu, mjini Dar Es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Bwana Tsvangirai amemweleza Rais Kikwete juu ya mazungumzo yanayoendelea kati ya MDC na chama tawala cha Zimbabwe cha ZANU-PF kuhusu uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini humo.
Bwana Tsvangirai amemweleza Rais Kikwete kuwa mazungumzo hayo bado yamekwama na akamwomba mwenyekiti huyo wa AU kutumia mamlaka ya umoja huo kuangalia jinsi ya kukwamua mazungumzo hayo.
Mazungumzo hayo ya kuundwa kwa serikali ya kitaifa nchini humo ni mchakato wa AU, ambayo imeiomba Jumuia ya Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC) kusimamia moja kwa moja mazungumzo hayo chini ya mpatanishi Mheshimiwa Thabo Mbeki, Rais wa zamani wa Afrika Kusini.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
03 Desemba, 2008