More than serious nahitaji mume wandugu

Wana JF, mimi ni mwanadada na leo nimeona nijitoe muhanga kabisa maana ninahitaji mume/mchumba. Niko tayari kupokea kukosolewa ila kwa yule aliyeko kwenye shinda kama yangu tafadhali ni PM.
Mimi ni Mkristo ninayempenda Mungu na ninahofu ya Mungu ndani yangu, tayari niko kwenye umri wa kati ya 30-33 na ninahitaji mume wa kati ya 33 na kuendelea. Awe na elimu ya kujitosheleza, mfanyakazi au aliyejiajiri. Kabila lolote Tanzania na pia awe Mkristo. Hili swala naomba tu mchukulie kwangu ni kitu halisi hapa sina utani na wala siko kwa ajili ya kumpotezea mtu muda. Na katika hili pia namshikirisha Mungu nikiamini mume/mke mwema anatoka kwa Bwana. Na pia kwa wale watakao nishauri na kunitia moyo kwenye hili nawashukuru. Kaka zangu popote pale ulipo na unajiona kweli unahitaji mke naomba uni PM lakini kama ni swala la mzaha au kujaribisha naomba usipoteze muda.

Nimekupata dada nina imani kuwa kweli una hilo hitaji la mume. Na ni vizuri kuwa unamshirikisha Mungu ktk hili.

Ushauri wangu kwako ni kama ifuatavyo.

Kwanza forum hii inaweza kukusaidia kimawazo zaidi kutokana uzoefu wa watu mbalimbali kumpata mtu sahihi kwa maana ya mume.

Kwa vigezo ulivyotoa kwa kweli kabisa ni wazi utapata kwa haraka sana mwanaume si mume?

Swala la mume linahitaji zaidi kuishirikisha roho kuliko nafsi. Hapa namaanisha kuangalia zaidi maswala ya upendo zaidi kuliko muonekano wa nje!

Umesema juu ya awe na kazi elimu ya kutosha etc hivi vyote ni material. Kwa hayo machache nakushauri na nawaomba wadau wengine kutoa ushauri wa kuweza kujua ni yupi atakufaa kama mume na si mwanaume. Naamini kuwa roho mtakatifu amekuwa akikufunulia lakini kwa namna moja au nyingine ujaweza kutambua. Ni wazi kwa umri wako umekutana na vijana wa kiume ambao baadhi walionyesha nia lakini wengine hawakuonyesha. Hapa JF utapa ushauri ikiwa ni pamoja na jinsi gani ya kutambua mapenzi ya kweli. Sikushauri kwa vigezo ulivyoainisha kama viwe ndio ilani yako. Naamini umeshawaona vijana wengi wa aina hiyo lakini kwa namna moja umewaona hawakufai.
 
Hahahahaaaaaaa lol umenifurahisha sana ulivyojibu nikisoma kati kati ya mistari naona..................

nikirudi kwa mtoa mada i wish you all the best dear na uzidi kumuomba mungu
 
JENA hata mie nina hitaji mke lakin kigezo cha umri wa mwanaume umtakaye zina nitoa hebu punguza iwe 30yrs nami niwe included niko siriaz kabisa ukijibu ha2a nyingine itafuata wako ninaweza
 
Nakuomba ufanikiwe dada yangu, ila angalia sana ya moyoni kuliko ya nje, ya moyoni yakishakuwa mazuri ya nje Mungu mwenyewe atayatengeneza tu. nitakuweka kwenye maombi yangu ili siku moja uje utupe ushuhuda maana kuna watu naona wanasema hapa huwezi kupata mume.
 
Jamani wana JF nawashukuru wote kwa ushauri wenu, najisikia vizuri kwamba kuna watu wameelewa kwamba niko serious na wengi wenu mmenishauri vizuri. Nazidi kuwaomba mzidi kuniombea ili niweze kukamilisha hili zoezi na ninauhakika nikifanikisha tu lazima nirudi kutoa shukrani za dhati.
 
All the best jena dont forget to pray because without God's grace we can not achieve whatever we want to do.
 
What a coincedence! Wana Jf heshima kwenu, ni mara yangu ya kwanza kuchangia humu jamvini lakini nakutana na habari njema za mchumba, ki ukweli niko single na ninahitaji mchumba umri miaka 34, nafanya kazi serikalini lakini nina hofu kweli na namna hii ya kupata mchumba ni kweli naweza kupata mtu anayefaa kweli kimaisha? Jamani.. "we are talking about life here! Let's be more than serious!
 
Shibalanga, karibu sana JF!
Si umeona dada hapo ametangaza nia, tuma maombi Shibalanga, huwezi kujua, labda ndo mpango wa Mungu awakutanishe hapa JF. Kila la heri!
 
What a coincedence! Wana Jf heshima kwenu, ni mara yangu ya kwanza kuchangia humu jamvini lakini nakutana na habari njema za mchumba, ki ukweli niko single na ninahitaji mchumba umri miaka 34, nafanya kazi serikalini lakini nina hofu kweli na namna hii ya kupata mchumba ni kweli naweza kupata mtu anayefaa kweli kimaisha? Jamani.. "we are talking about life here! Let's be more than serious!

tamaa mbaya mkuu, ila kana jina zuri eti!
 
Jena njoo kwangu ni single nina umri wa 35, mkristo. Mm nataka mwanamke mrefu mwenye kiuno kilichogawanyika.
 
Kila la heri Jena, ukifanikiwa usisite kuja kutupa taarifa ili kuwatia moyo wengine wenye nia kama yako lakini wanahisi pengine hawatafanikiwa.
 
Nakutakia kila la heri. Mungu akujalie haja ya moyo wako. Mimi nilikuja na shida yangu hapa wengi wamenisaidia sana kwa ushauri. kwa hiyo dada nakutia moyo usikate tamaa mume atapatikana humu humu ndani.
 
Midhali uko tayari kukusolewa, kushauriwa uwe tayari zaidi. Mi si mkristo sitarajii kuku PM. Imenenwa "mpendelee nduguyako lile ambalo unalipenda wewe nafsini mwako". Tafuta contacts za Dr W Slaa (mgombea urais Tz 2010). Huyu anakidhi karibu vigezo vyako vingi na ana shida, Inasemekana amefikia hadi kuazima au kupora wake za watu jinsi alivyo na shida ya mke.

1 Anapenda na ana uwezo wa kukosoa, katika ndoa yenu uta enjoy na hilo, 2 umri wake ni zaidi ya miaka 33. 3 ni Mkristo, ni padri mpenda bwana hata katika Uchaguzi mkuu wakristo wengi waliridhika nae. 4 ana elimu ya kujitosheleza naamini hakusoma shule za Memkwa wala UPE, 5 kajiajiri kisiasa zaidi, posho yake siijui kwa siku ni kiasi gani lakini matanuzi anayo, usishangae posa za awali na pete vinaweza kuletwa kwa helikopta kama kwenu hakuna barabara, wakati wa ndoa yenu mnaweza mkajinunulia gari la kwendea msalani na lingine sokoni n k.

Sikufatilia kabila lake halisi kama ni mtusi au mmasai ila dalili za ubantu na uhutu hana. any way midhali kigezo kwako si tatizo naamini utamtafuta.

Hii isije ikafikirika namfagilia Slaa peke yake ila na wewe pia nataka ukipate unachotafuta
 
The world is not fair at all.." watu kama huyo Nduguyangu they are good for nothing and fit for no where..." watu wako serious unaleta upuuzi wako hapa! Kama huna cha kuchangia kaa pembeni!
 
Dada Jena umenitia moyo sana manake hata mie nahitaji mchumba lakini nilifikiri hapa ndani sio mahali sahihi pa kulizungumzia kumbe nakosea. Kila la kheri mama.
 
Midhali uko tayari kukusolewa, kushauriwa uwe tayari zaidi. Mi si mkristo sitarajii kuku PM. Imenenwa "mpendelee nduguyako lile ambalo unalipenda wewe nafsini mwako". Tafuta contacts za Dr W Slaa (mgombea urais Tz 2010). Huyu anakidhi karibu vigezo vyako vingi na ana shida, Inasemekana amefikia hadi kuazima au kupora wake za watu jinsi alivyo na shida ya mke.

1 Anapenda na ana uwezo wa kukosoa, katika ndoa yenu uta enjoy na hilo, 2 umri wake ni zaidi ya miaka 33. 3 ni Mkristo, ni padri mpenda bwana hata katika Uchaguzi mkuu wakristo wengi waliridhika nae. 4 ana elimu ya kujitosheleza naamini hakusoma shule za Memkwa wala UPE, 5 kajiajiri kisiasa zaidi, posho yake siijui kwa siku ni kiasi gani lakini matanuzi anayo, usishangae posa za awali na pete vinaweza kuletwa kwa helikopta kama kwenu hakuna barabara, wakati wa ndoa yenu mnaweza mkajinunulia gari la kwendea msalani na lingine sokoni n k.

Sikufatilia kabila lake halisi kama ni mtusi au mmasai ila dalili za ubantu na uhutu hana. any way midhali kigezo kwako si tatizo naamini utamtafuta.

Hii isije ikafikirika namfagilia Slaa peke yake ila na wewe pia nataka ukipate unachotafuta
Nilitegemea kwa mtu mpenda haki kama wewe na kwa imani yako iliyo safi na kwa usomi wako utajitendea haki kwa kuweka hapa hukumu ya shauri hilo, ili kutia nguvu shutuma zako.. Si tulisikia suala hilo lilifikishwa mahakamani? Mlalamikaji alichemka huko au alishinda??
 
Jamani wana JF nawashukuru wote kwa ushauri wenu, najisikia vizuri kwamba kuna watu wameelewa kwamba niko serious na wengi wenu mmenishauri vizuri. Nazidi kuwaomba mzidi kuniombea ili niweze kukamilisha hili zoezi na ninauhakika nikifanikisha tu lazima nirudi kutoa shukrani za dhati.

just a question...kwa nini unataka kuolewa kiasi hicho?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom