Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,930
- 31,171
Heshima kwako Shamu,
Mkuu umezungumzia mambo mawili makubwa.
Moja Kanisa linafanyabiashara wakati hawalipi kodi,Jibu Mradi wa kuzalisha umeme kwa vyovyote lazima uendeshwe na kampuni ambayo itafuata taratibu zote za uendeshaji wa kampuni eg,kulipa kodi zote zinazotakiwa kulipwa na makampuni mengine ambayo hayamilikiwi na mashirika ya dini eg PAYE,VAT,SDL na Corporate tax.kampuni hatakuwa na tofauti na makampuni mengine unayoyajua pengine tofauti kubwa ni umiliki "Kanisa katoliki.
Mbili, Makanisa mengi Tanzania hasa RC,KKKT na Anglican wana structure nzuri sana kiasi kwamba kuanzisha miradi mkubwa kama vyuo vikuu,Mahospital makubwa ni jambo rahisi sana.Mfano ukitembelea dayosisi ya Arusha utakuta uongozi umepangwa sawa sawa eg mkuu wa dayosisi ni askofu then anakuwepo mtendaji mkuu [Katibu mkuu] lazima awe na degree ya masuala ya utawala na uongozi,then mweka hazina lazima awe na CPA au sifa inayolingana na hiyo then mwanasheria lazima awe na degree ya sheria,afisa mipango na uchumi lazima awe na degree ya uchumi au sifa zinazolingana na hizo then utakuta mkuu wa afya au elimu nao lazima wawe na sifa zinazolingana na wajibu wa kazi zao.
Mkuu wangu ebu chungulia BAKWATA au kamati ya kutetea mali za waIslam au Shura ya maImamu au Ulamaa hakika utakutana na viongozi wasiokuwa na vision wala mission.Utakumbana na viongozi wanopigania umiliki wa misikiti,utakumbana na viongozi wanauza mali zilizoachwa na waIslam [wakfu],utakutana na viongozi wadanganyifu na wenye lugha za kichonganishi eg Mfumo kristo,waIslam tunaonewa na nk.
Hakika waIslam wa Tanzania ukiondoa Aghakhan wamelala hawana fikra za maendeleo hawatoi nafasi kwa waIslam wasomi,badala yake wamejikita kwenye mihadhara isiyo na tija kwao na kwa taifa.
Tatizo siyo kufanya biashara bila ya mpinzani. Tatizo ni kwamba unashindana na mashirika ambayo hayalipi kodi; lakini yanafanya biashara kama mtu mwingine ambaye analipa kodi. Huoni kama hili tatizo? Unajua tatizo litakapotokea baadaya kama haya mashirika ya dini yatakuwa monopoly ktk sector? bila ya kulipa kodi?
Hii nchi ilijaribu Ujamaa na ulishindwa vibaya sana. Sasa kwanin tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele? Huu mpango wa Kanisa kutoa huduma kwa wananchi ni kuwarudisha nyuma WTZ. Unawafanya WTZ kuwa wategemezi zaidi wa misaada. Taifa halijengwi kwa misingi hii.