Money is Power (MP) ni nini?

Mr Suprize

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
825
847
Wakuu habari yenu!
Kwanza niseme sijaanzisha huu Uzi kwa lengo La kupromote au kuponda biashara ya MTU. Mimi binafsi nahitaji kujua Yale ambayo siyajui kama tujuavyo JF ni pana na ina kila aina ya watu!

Katika pitapita zangu kwenye mitandao ya kijamii , kupitia mtandao Wa Facebook nilikutana na post ya kijana mwenzetu anaitwa Herry Samir Sovi (hilo ndo jina analotumia Fb) akitoa fursa kwa vijana ambao ni wasanii chipukizi kujiunga na chama kinachoitwa Money is Power , wakishajiunga yeye Herry Samir Sovi atawasaidia kuwafikisha mbali kimuziki.


Post ilinivutia japo Mimi sio mwanamziki, nikaamua kumfatilia vizuri kwa timeline yake nijue anafanya kazi gani hadi ajitoe kuwasaidia vijana wenzake. Nilichokiona kwenye Timeline yake ni picha za shuhuda mbalimbali za watu kutoka mikoa mbalimbali hapa Tanzania wakimshukuru kwa kuyabadili maisha yao kupitia chama cha Money is Power.
Baadhi ya watu waliuliza kupitia comments , money is power ni nini? Swali halijibiwi kwenye comment bali Walikuwa wanapewa namba wawasiliane WhatsApp kupata maelezo kuhusu Money is power,

Nikachukua namba nikamcheki whatsapp bhana Herry Samir Sovi nilichoambiwa kwa kifupi ni hivi;
°Money is power ni chama kilichoanzishwa uingereza miaka ya 70. Kwa hapa Tanzania kina miaka 15 sasa tangu kiingie.
°kwa mujibu wa ye mwenyewe Herry Samir Sovi ni mzaliwa Wa Kigoma alikuwa muuza viatu soko la kariakoo, siku moja alikuja mzungu kununua viatu kwake, yule mzungu baada ya kuona hali anayopitia bhana Herry katika utafutaji Wa maisha aliguswa sana akaamua kumshirikisha habari za hiki chama cha MP .
°Herry kwa woga na mashaka (kishingo upande) akaamua kujiunga huku akilini mwake akijua ni chama cha kutoa kafara kama ilivyo kwa vyama vingine vya utoaji kafara. Lakini hali haikuwa hivyo , mwanzoni ndugu zake walimtenga baada ya maisha yake kubadilika ghafla , ndugu waliamini jamaa amejiunga na vyama vya utoaji kafara .
°Money is power ni chama cha mafanikio ambacho ukijiunga wanakupa Tsh million 100, Wanakununulia nyumba popote utakapochagua,na pia unapewa usafiri gari aina ya BMW mpya.
°Ni chama ambacho hakitoi kafara na sio Freemason
°Kujiunga inabidi ununue vifaa flani hivi (nimesahau) kwenye maduka ya waarabu , cost haizidi Laki moja inategemea na mkoa uliopo.
Baada ya kununua hivyo vifaa utapewa form ukishajaza unapata gari BMW , Tsh million 100, na nyumba bure. Hizo Pesa unatumia kadri uwezavyo.
°Chama kinaofisi kila mkoa hapa Tanzania.
°Chama hakichagua dini,kabila,wala kipato cha MTU yeyote anaruhusiwa kujiunga kikubwa anunue hivyo vifaa.

Nilitamani sana kuona kilichoandikwa kwenye form ila niliambiwa huwezi kupewa form bila kununua hivyo vifaa.

Nikiangalia testimonies za watu kwenye page yake ya Facebook wanamshukuru sana na wanatamani Tanzania ingepata vijana kama bhana Herry Samir Sovi ingekuwa mbali sana kiuchumi.

YEYOTE ANAYEJUA MORE DETAILS JUU YA HIKI CHAMA TAFADHALI ATUJUZE .

Nimeweka picha hapo chini ni testimonies za watu mbalimbali wakimshukuru bhana Herry Samir Sovi..
 

Attachments

  • IMG_20180318_180758_369.JPG
    IMG_20180318_180758_369.JPG
    97.2 KB · Views: 182
  • IMG_20180318_180901_538.JPG
    IMG_20180318_180901_538.JPG
    121.6 KB · Views: 158
  • IMG_20180318_180925_902.JPG
    IMG_20180318_180925_902.JPG
    92.4 KB · Views: 149
  • IMG_20180318_180937_492.JPG
    IMG_20180318_180937_492.JPG
    108.2 KB · Views: 149
  • IMG_20180318_180954_262.JPG
    IMG_20180318_180954_262.JPG
    91.2 KB · Views: 134
  • IMG_20180318_181004_765.JPG
    IMG_20180318_181004_765.JPG
    122.9 KB · Views: 132
  • IMG_20180318_181018_346.JPG
    IMG_20180318_181018_346.JPG
    92.3 KB · Views: 136
  • IMG_20180318_181029_191.JPG
    IMG_20180318_181029_191.JPG
    80.5 KB · Views: 132
  • IMG_20180318_181046_976.JPG
    IMG_20180318_181046_976.JPG
    87.2 KB · Views: 136
  • IMG_20180318_181105_262.JPG
    IMG_20180318_181105_262.JPG
    81.1 KB · Views: 119
  • IMG_20180318_181156_021.JPG
    IMG_20180318_181156_021.JPG
    102.8 KB · Views: 126
  • IMG_20180318_181239_428.JPG
    IMG_20180318_181239_428.JPG
    82.7 KB · Views: 124
  • IMG_20180318_181221_789.JPG
    IMG_20180318_181221_789.JPG
    78.1 KB · Views: 129
  • IMG_20180318_181255_250.JPG
    IMG_20180318_181255_250.JPG
    106.7 KB · Views: 124
  • IMG_20180318_181206_917.JPG
    IMG_20180318_181206_917.JPG
    111.2 KB · Views: 127
  • IMG_20180318_181306_702.JPG
    IMG_20180318_181306_702.JPG
    99.1 KB · Views: 129
  • IMG_20180318_181318_032.JPG
    IMG_20180318_181318_032.JPG
    77.6 KB · Views: 143
Back
Top Bottom