Mombasa Republican Council: Tukishindwa kupata haki yetu Kenya tutakwenda katika mahakama ya kimatai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mombasa Republican Council: Tukishindwa kupata haki yetu Kenya tutakwenda katika mahakama ya kimatai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 23, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2]Friday, 22 June 2012[/h][h=3][/h]

  [​IMG]

  Kundi la Mombasa Republican Council (MRC) linalopigania k
  itenga Pwani ya Kenya limesema kuwa, iwapo serikali ya nchi hiyo haitasikiza kilio chake basi litawasilisha malalamiko yake katika mahakama ya kimataifa (ICJ).C, Mohammad Rashid Mraja amesema kuwa kundi hilo linaendelea kupata nguvu siku baada ya siku na harakati zake za kutaka eneo la Pwani lijitenge zinaendelea kupata uungaji mkono kutoka kwa wakaazi wa mkoa huo. Mraja ameongeza kuwa uchaguzi mkuu ujao utasusiwa na idadi kubwa ya watu wa Pwani iwapo serikali haitatatua mapema mvutano ulioko kati yake na MRC.

  Hata hivyo msemaji huyo wa Mombasa Republican Council ameendelea kushikilia kwamba kundi lake haliwezi kuketi meza moja na serikali hadi pale litakapoondolewa katika orodha ya makundi yaliyopigwa marufuku. Hii ni katika hali ambayo tayari bunge la Kenya limeteua kamati mbili zitakazofanya mazungumzo na kundi hilo la MRC
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  ..wakienda kwenye mahakama ya kimataifa watashindwa.

  ..Sultani wa Zanzibar na Waziri Mkuu Shamte walipokea malipo na ku-transfer eneo hilo kwa Kenyatta.

  ..pia mwambao wa Kenya na bandari ya Mombasa ni tegemeo kwa nchi nyingine kama Uganda,Rwanda, na Burundi.
   
Loading...