Mojtaba Khamenei achaguliwa kumrithi hayati baba yake…

Mojtaba Khamenei achaguliwa kumrithi hayati baba yake…

View attachment 3555242

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amelishukuru Baraza la Wataalamu kwa kumchagua mrithi wa Ali Khamenei licha ya "tishio la Trump la kulishambulia kwa mabomu", kwa mujibu wa mashirika kadhaa ya habari ya Iran.

Ali Larijani anasema "maadui" wa Tehran walifikiri nchi "ingefikia mkwamo" kufuatia kifo cha Ali Khamenei, lakini Baraza hilo hatimaye liliendelea na mchakato wa kumchagua Mojtaba Khamenei.

Mojtaba Khamenei, mwenye umri wa miaka 56, alionekana kuwa na ushawishi mkubwa nyuma ya pazia, na ameshutumiwa kwa kuingilia chaguzi za urais, kuongoza kundi la wanamgambo la Basij, na kudumisha uhusiano wa karibu na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Licha ya ripoti na uvumi kuhusu ushawishi wake mkubwa, hajawahi kushikilia wadhifa wowote rasmi ndani ya Jamhuri ya Kiislamu.

Baba yake, Ali Khamenei, pamoja na mtangulizi wake, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu Ruhollah Khomeini, wote walikuwa wamekosoa urithi wa madaraka wa kifamilia katika muktadha wa ufalme wa Pahlavi, ambao ulipinduliwa katika Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Mnamo mwaka 2019, Mojtaba Khamenei aliwekewa vikwazo na Marekani kama sehemu ya kundi la watu "walioteuliwa au waliofanya kazi kwa niaba ya" Kiongozi Mkuu wa Iran wa wakati huo, Ali Khamenei.
Ni kwamba Mojtaba amesaini hati ya kifo chake
 
Au huo ukoo umeamua kufa? Baba kauawa,mama kauawa,sasa mnamchagua Mojtaba Khamenei,huku ni kumwandalia kifo tu.Ingekuwa ni mimi Mojtaba na surrender na kusema sitaki vita
 
Ila kuna mambo yanaitaji courage and a lot of resilience, imagine unajua muda wowote unauliwa, na unawindwa kama swala porini.
Ukisha zaliwa katika familia za namna hiyo unakuwa trained katika psychology Yako kuweza kuona kuwa hicho ni kitu Cha kawaida , Hujawahi kuona watu wanajua fika kuwa madawa ya kulevya ni kitu hatari na ukikamatwa sehemu yoyote ile duniani ni msala mzito lakini Kuna watu wanayabeba na kupita nayo airport kama wewe unavyo pita na laptop Mbezi bus terminal
 
Back
Top Bottom