Moja ya vitu ambavyo directors wa action movies wanafeli

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,379
105,217
Mazungumzo mafupi kati ya Jambazi aliyeshilia mateka na Starling anayetaka kumuokoa mateka

Jambazi: "Weka silaha yako chini, ukisogea hatua moja namuua huyu"

Starling: "Sawa nimekubali naweka silaha chini"
1686911663418.png

Jambazi ambaye kamuwekea silaha kichwani mateka na kumuamuru starling ambaye kamnyooshea silaha kuwa aweke silaha chini vinginevyo mateka atauwawa, halafu starling anatii amri ya Jambazi.

Hii scene iko mbali sana na uhalisia.

Katika hali ya uhalisia kwa kama situation hiyo silaha ndio kitu muhimu. Ukipoteza silaha umekubali kupoteza maisha ya mateka na yako mwenyewe.

Directors wanaweza kukuletea hii scene katika namna nyingi, wanaweza kukuletea scene inayomuonesha Polisi dhidi ya mwalifu aliyeshikilia mateka.

Halafu baadae huyo polisi unamuona anaenda kutii amri ya jambazi kwa kusalimisha silaha yake chini kwakitisho cha kuuliwa huyo mateka iwapo ataendelea kumnyooshea jambazi silaha.

Kwenye mafunzo ya upolisi unafunzwa kuwa usikubali kusalimisha silaha yako, kwasababu ukifanya hivyo nafasi ya wewe kupona inashuka na kuwa zero.

Lakini kingine ni kuwa Starling tayari alikuwa amemuweka kwenye target Jambazi tayari alikuwa yupo kwenye perfect angle ya kuweza ku shoot.

Sasa Directors wanatuaminisha kwamba ule muda ambao Starling anavuta trigger kumshoot Jambazi kutakuwa na nafasi ambayo Jambazi naye ataipata ya kumshoot mateka baada ya kupigwa risasi na Starling kitu ambacho hakiwezi kuwa realistic.
 
Fikilia mtoto wako mpendwa wa pekee amewekewa siraha kichwani, na sharti la muharifu uweke siraha chini we utafanya nn?.
Ukiweka silaha chini umekubali kumpoteza na kupoteza maisha yako pia.

Ule wakati ambao Jambazi ameweka silaha kwenye kichwa cha mateka ndio muda mzuri wa wewe kum-shoot adui

Ukimpiga risasi ya kichwa hapo umemaliza mchezo, ila kuweka silaha chini ni kukubali kupoteza maisha ya watu wote wawili
 
Nope....

Aliyeteka motive yake ni kutoroka na sio necessarily kuua...

Ukiweka silaha chini unaonge time ya what might happen huenda akamuachia akishafika mbali au ukapata upenyo wa better target au mwenzako akapata chance ya better target

Ukiambiwa ushushe silaha ukakataa badala ya ku-negotiate game over; na wewe kama polisi utashitakiwa kwa kuweka hatarini maisha ya aliyetekwa....

Ukishoot ukamiss au akamuua aliyetekwa game over kwako na utashitikiwa kwa kusababisha kifo cha aliyetekwa...

Hivyo basi in this scenario it makes perfect sense logically within the premise of the story
 
Ukiweka silaha chini umekubali kumpoteza na kupoteza maisha yako pia.

Ule wakati ambao Jambazi ameweka silaha kwenye kichwa cha mateka ndio muda mzuri wa wewe kum-shoot adui

Ukimpiga risasi ya kichwa hapo umemaliza mchezo, ila kuweka silaha chini ni kukubali kupoteza maisha ya watu wote wawili
Wewe jamaa uwezo wako wa kufikiria ni mdogo sana. Unadhani majambazi yanavyoteka Bar na kulazimisha watu wote kutii ni kwamba pale Bar wote hawana bastola? Unafikiri kumlenga mtu risasi ya kichwa ni kitu kirahisi sana?
 
Nope....

Aliyeteka motive yake ni kutoroka na sio necessarily kuua...

Ukiweka silaha chini unaonge time ya what might happen huenda akamuachia akishafika mbali au ukapata upenyo wa better target au mwenzako akapata chance ya better target

Ukiambiwa ushushe silaha ukakataa badala ya ku-negotiate game over; na wewe kama polisi utashitakiwa kwa kuweka hatarini maisha ya mateka....

Ukishoot ukamiss au akamuua mateka game over kwako na utashitikiwa kwa kusababisha kifo cha mateka...

Hivyo basi in this scenario it makes perfect sense logically within the premise of the story
Akitoroka akakuacha mzima wakati tayari ushamjua sura unafikiri atakuwa na comfortable ya usalama wake?

Hakuna kesi kwa polisi kwa kukataa amri ya adui ya kuweka silaha chini.

Ngoja nikukumbushe kitu.

Mwaka 1963 mapolisi wawili wa L.A.P.D walisimamisha gari ambalo walikuwa wanalishuku kuwa na majambazi wawili ambao recently walikuwa wametoka kufanya robbery.

Majambazi hao walikuwa ni Smith na Powell.

Baada ya Polisi kusimamisha gari, wale majambazi wakawa wamestukia mchongo wakati polis anafungua mlango kuwaamuru watoke nje, polisi akawekwa chini ya ulinzi.

Wakati polisi yupo chini ya ulinzi na bunduki imekwekwa kwenye kichwa chake, yule polisi mwenzake akaambiwa aweke silaha chini kisha aipige teke iende kwa maadui.

Polisi akatii agizo.

Wale wakachukua ile silaha kisha wakampiga risasi yule polisi aliyesalimisha silaha, akafa.

Yule mwingine aliyekuwa chini ya ulinzi akafamikiwa kukimbia huku risasi nyuma zikimiminika.

Baada ya hapo 1968 kwenye academy za Sheriff Los Angeles, mchunguzi wa hilo tukio kubaini kilichotokea kwenye lile tukio ikaundwa sheria rasmi ya kutosalimisha silaha kwa adui kwasababu yeyote ile.

Kwa hiyo kusema utakuja kuhukumiwa na polisi kwa kuvunja sheria unakuwa unakosea kwasababu sheria ndio inayompa mamlaka ya kutosalimisha silaha.
 
Wewe jamaa uwezo wako wa kufikiria ni mdogo sana. Unadhani majambazi yanavyoteka Bar na kulazimisha watu wote kutii ni kwamba pale Bar wote hawana bastola? Unafikiri kumlenga mtu risasi ya kichwa ni kitu kirahisi sana?
Gun point sio sawa na robbery ambayo mwenye silaha ni mmoja dhidi ya majambazi wenye silaha.
 
hizi scenes nakuwa sizipendi kweli yaani,
kuna baadhi ya films (chache mnooo), star anagoma, anamlenga anamshoot villain kichwani,
Na zipo zingine unakuta jambazi kamuwekea kisu shingoni mateka halafu starling ana bastola na anaambiwa aweke silaha chini afu ana tii
 
Ukiwangalia 24 utagundua vingi saa nyingine mateka ana umuhimu kwa pande zote mbili kupata information
Kwenye 24 hrs kuna wakati jack bauer anakubali kuweka silaha chini ili kumuokoa mateka na anachukuliwa yeye kwenda kuteswa lakini huko huko kwenye mateso anapata information zaidi kutoka kwa maadui.

Sometimes kusurrender ni muhimu zaidi ili kuokoa wengine. Afterall starring hauwawi, akiuawa ujue movie imeisha au inaelekea kuisha!
 
Only kwenye movies in reality it's crazy idea to think a bad guy would have a mercy on you
 
Ukiwangalia 24 utagundua vingi saa nyingine mateka ana umuhimu kwa pande zote mbili kupata information
Kwenye movies tu na ndio maana nimeandika kuonesha tatizo

Kwasababu lengo la movies ni kusimulia matukio kwa kuhusisha na uhalisia.

Na ndio maana Bongo Movies ilipata ukosoaji kwenye scene ambayo jambazi alionekana kuvua viatu mlangoni wakati akienda kufanya robbery.

Hiyo ilipingwa kwa kuangalia uhalisia wa matukio kama hayo yakifanyika huwezi kuona jambo kama hilo.

So kwenye situation ya adui kumuwekea mateka silaha kisha kumuamuru Polisi aweke silaha chini na polisi kutii amri, ni ujinga wa kiwango cha juu.

Kwasababu kwanza umempa imani mwalifu kuwa atafanya kile alichokuahidi (kutompiga risasi mateka)

Na pili una amini pia hata wewe atakuacha huru, wakati mpaka anachukua silaha kuja kufanya tukio kama hilo alikwisha jipanga kufanya lolote.
 
Kisa kingine hiki.

December 22 Mwaka 1978 California Highway Patrol (CHP) Polisi wawili wakiwa kwenye patrol, William M. Freeman akiwa na umri wa miaka 35 na Roy P. Blecher akiwa na umri wa miaka 50.

Pichani hapa chini ni William M. Freeman (35)

1687171718650.png

Pichani hapa chini ni Roy P. Blecher (50)
1687173191162.png

Maofisa hao walisimamisha gari walilokuwa wanalishuku kuwa na mhalifu.
Ndani ya lile gari kulikuwa kuna mhalifu anayeitwa Luis Valenzuela Rodriguez aliyekuwa na miaka 23.

Punde tu baada ya maofisa hao kusimamisha gari na kushuka kuanza kulifuata, yule suspect akatoka haraka kwenye gari na kumuweka mateka polisi mmoja.

Baada ya hapo akatoa amri kwa polisi mwingine kuwa aweke silaha chini kisha aipige teke ije kwake vinginevyo mwenzake aliyewekwa mateka atauawa.

Ofisa akasalimisha silaha yake, yule mwalifu akachukua pingu na kuwafunga wote mikono nyuma kisha akawalaza kifudifudi halafu akawapiga risasi wote na kuwaua.

Baada ya uchunguzi walipata ushahidi kupitia redio za maofisa zilizo kwenye gari zilizokuwa zina rekodi sauti wakati wa tukio.

Luis Valenzuela Rodriguez alihukumiwa kunyongwa hadi kufa lakini mwaka 1991 adhabu ikapunguzwa na kuwa kifungo cha maisha jela

Alhamisi ya April 14 mwaka 2016 Luis Valenzuela Rodriguez alifariki gerezani akiwa na umri wa miaka 60 kwa kifo cha asili (natural death)

*********

Polisi na mamlaka za kiusalama waliweka sera ya kutosalimisha silaha kwa adui kamwe haijalishi sababu gani.
 
Ukiweka silaha chini umekubali kumpoteza na kupoteza maisha yako pia.

Ule wakati ambao Jambazi ameweka silaha kwenye kichwa cha mateka ndio muda mzuri wa wewe kum-shoot adui

Ukimpiga risasi ya kichwa hapo umemaliza mchezo, ila kuweka silaha chini ni kukubali kupoteza maisha ya watu wote wawili
Sio rahisi kama unavyodhani.
 
Back
Top Bottom