MOI: Mgomo wa Madaktari Bingwa unaendelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MOI: Mgomo wa Madaktari Bingwa unaendelea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pius Kafefa, Sep 15, 2012.

 1. P

  Pius Kafefa Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Nianze kwa kuwapa pole wagonjwa wote waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili.
  Nilifika Muhimbili kwa mara ya kwanza siku ya Alhamis tarehe 13.09.2012, majira ya saa nne na nusu asubuhi. Baada ya kutoa maelezo kwa walinzi wakanishauri nisubiri hadi saa sita na nusu mchana ndiyo ningeruhusiwa kumwona mgonjwa niliyeenda kumjulia hali. Nikasubiri.

  Muda huo ulipofika nikaingia na kuongoza moja kwa moja hadi wodi ya Mwaisela, namba 2. Hapo nikakutana na kikwazo. Walinzi wawili na muuguzi mmoja walikuwa wanahakiki watu wote wanaopita hilo lango la kuingia wodini. Ilani ikatolewa wenye chakula tu ndiyo wanaoruhusiwa kuingia.

  Katika mchujo huo wote waliokuwa na juisi, maji, na matunda wakazuiliwa na hao walinzi. Kwangu mimi ambaye sikubeba chochote ilikuwa ni ngumu zaidi kueleweka. Akaja kijana mwingine aliyeonekana amevalia nguo nadhifu, mkononi kashika Biblia na kitabu cha maombi. Akasema amekuja muda huu kwa ajili ya kufanya maombi kwa Mungu kwa ajili ya mgonjwa wake aliyelazwa wodi hiyo. Akaambiwa "hakuna kuingia, huu ni muda wa chakula kwa wagonjwa, muda wa kuona wagonjwa ni saa kumi".

  Baada ya msongamano kupungua nikamfuata Mzee mmoja aliyeonekana anasaidiana na walinzi. Nikamwambia: "baba nina dharula, nahitaji kumwona mgonjwa wangu muda huu ili nijue mahitaji yake, siishi mji huu (Dar) na ninahitaji kufahamu mahitaji yake mapema kabla ya saa kumi." Mzee yule akaniambia nimweleze yule kijana mlinzi aliyenizuia, tena niseme kwa hisia zile zile kama nilivyokuwa namweleza yeye. Nikamsogelea tena yule mlinzi na kumweleza. Yule kijana akaniambia: "nenda, halafu kata kulia". Nikaingia.

  Nilipofika mlangoni nikaanza kuona wagonjwa waliolala chini, kwenye korido ya kuingia wodini. Nikasita kwa kudhani labda nimekosea. Nilipoenda mbele kidogo nikatokeza chumba cha kulaza wagonjwa. Wagonjwa walikuwa ni wengi sana. Wamejaa hadi wengine kulazwa chini. Nikaanza kuangaza huku na kule nikimtafuta mgonjwa wangu! Nikamkuta mahali akiwa amelala, chini. Vitanda vimejaa!

  Akiwa katika siku ya nne toka afike alikuwa bado hajaelezwa kama atapatiwa matibabu lini. Yuko MOI. Sehemu ya wataalamu bingwa wanaotegemewa kuokoa maisha yake. Hapa hayuko peke yake. Wapo wagonjwa wenzake wengi. Na wengine walikuwa wanalia kwa maumivu makali.

  Kwa nini nasema MGOMO BADO UNAENDELEA?
  1. Wagonjwa wameongezeka na kufikia hatua ya kulala hadi kwenye korido. Kasi ya kuwatibu ni ndogo.
  2. Wale wanaoweza kutoa rushwa wanalazimika kulipia operation kwa siri. Unaweza kulipia shilingi ngapi, lini, kwa nani ndicho kigezo kwa sasa. Siwasingizii madaktari.

  Ilipotimu saa nane kasoro dakika tano kengele ikalia ikiashilia muda wa kuwapa chakula wagonjwa umekwisha. Nikasubiri hadi dakika tano baadaye ndo nikainuka pale sakafuni nilipokuwa nimekaa. Nikaanza kutembea kurudi nilikotoka huku mawazo tele yameniandama.

  Baada ya kufika geti la kutokea nikaona maandishi "OFISI YA MAONI/MALALAMIKO YA WATEJA". Nikashtuka! Nikawa nahaingaika moyoni kama niende kutoa maoni au nisiende. Baadaye nikaamua kwamba sitaenda kutoa maoni yangu kwenye kile kiofisi. Nikajiuliza kwani maoni yangu:
  • atakayeyapokea ni nani?
  • atakayeyachambua ni nani?
  • atakayeandaa ripoti ni nani?
  • atakayepokea ripoti ni nani?
  • atakayefanyia kazi mapendekezo ya ripoti ni nani?

  Nikafikia uamuzi. "JAMIIFORUMS.COM". Sikuwa na kompyuta siku ile, na simu yangu ndo hizi za bei poa. No intaneti. Nikaondoka na kuchukua dala dala kuelekea Ubungo. Kichwani mawazo tele! Huu mgomo nani anaujua? Hivi sakata lenyewe liliishaje? Dr. Ulimboka yuko wapi? Dr. Mkopi anaendeleaje na kesi yake? Je, ana mashahidi wa aina gani watakaowezesha asipatikane na hatia? Serikali nayo je, imeweza kudhibiti mgomo au imeuahirisha tu? Je, madhara ni yapi?

  Lakini pia nikajiuliza hivi chakula hasa ni kitu gani? Je, Watanzania wanaelewa maana hasa ya chakula? FIKIRIA: maji tu, hapana. Machungwa mawili matatu, huingii wodini. Umebeba Juisi, No. Eti "NI KWA WALE WANAOPELEKA CHAKULA TU". Nikawafikiria pia viongozi wa kiroho ambao wanatumia Biblia. Imeandikwa kwamba neno la MUNGU ni CHAKULA cha uzima.

  Nikiwa wodini, hata hivyo, wagonjwa na ndugu zao wengi walikuwa wanawalaumu madaktari. Wagonjwa wengine walikuwa wanawalaumu ndugu zao ambao wameshindwa kuchangia HONGO ili wafanyiwe upasuaji kwa wakati. Kwa kweli neno serikali sikulisikia. Pia Mungu alikuwa ametawala kwenye vinywa vya wengi. Nami naungana nao kwa kumwomba Mungu awatie nguvu ya kuvumilia machungu yote wanayoyapata, huku wakitumaini wokovu wake. AMEEN!
   
 2. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  kwenye rangi nyekundu inaweza kuwa ndiyo lengo la uzi huu.
  Ngoja nirudie kuusoma
   
 4. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,232
  Likes Received: 817
  Trophy Points: 280
  Madaktari nao ni binadamu jamani......... Wana mahitaji na wana familia zao na midomo mingi tu inayowategemea wao.
  Mwisho wa siku pamoja na udaktari wake lazima ahakikishe mahitaji yake na familia yake na ya wanaomtegemea yote yametimizwa.
  Hapo MOI wagonjwa ni wengi sana, na watenda kazi ni wachache, ndio ukweli halisi; to make matters worse, motivation ya hao watenda kazi iko chini sana; Utakuta daktair mmoja anapiga part time hospitali hata tatu ili mahitaji ya familia yakae vizuri, na kwa patients load ilivyo kubwa hapo MOI, lazima kazi ifanyike hadi baada ya muda wa kazi ili kazi ionekane inafanyika...... Sasa nani atakubali kufanya kazi baada ya muda wa kazi kwa malipo kiduchu, tena yanayokuja kupatikana kwa kuchelewa sana?? mtu anaona bora akapige zake part time reagency au Agha Khan kwa wahindi.
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Subiri, yuna mpango wa kuongea na wazee wa daresalamu. Tutapata suluhisho la liwalo na liwe.
   
 6. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mwendo wa sasa ni watu kufanya kazi muda wa kazi tu, baada ya hapo, huwaoni tena...hakuna cha call wala nini.. anyway, taratibu tutafika.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ningeshauri tena na tena serikali ijipange upya kurudi mezani na madaktari!!ubabe kwa afya za walala hoi ndio utawakosesha kura nyingi sana na kumpa wakati mgumu sana mgombea wao hata kama wanategemea kura za unyonge za wanawake kwa mwanamke mwenzao haitasaidia kamwe!wasikimbilie mahakamani kwa suala nyeti kama la afya!najua madaktari wanasubiri hatma ya Rais wao na kesi yake ili wajue kama wanaliendeleza au la!nashauri wangerudi mezani wayamalize kwa manufaa ya ustawi wa taifa!!!
   
 8. M

  Moony JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Du,jitahidi uanze kutunga RIWAYA kwani unajua kuandika story vzr
   
 9. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sometimes, an elder can see far beyond while sitting than a youngster while standing on a chair...Mkuu Skills4Ever, u went way beyond tunavyotaka(esp. viongozi) kufikiria.. ni ngumu kurudi katika mazungumzo kwa kuwa "suala hili liko mahakamani".. sasa inabaki kuonyesheana ubabe kati ya serikali na madaktari KIMYA KIMYA na tunaoumia ni sisi.
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada umelonga kweli,mimi nna mgonjwa wangu yupo SEWAHAJI,NAPO UKIENDA UNAKUTA WATU WANALALA CHINI,,,BAADA YA KUNYOOSHA MKONO JAMAA WAMEKUBALI KUMFANYIA UPASUAJI,,,,,,
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  siamini,maana hakuna ushahidi wa kisayansi
   
 12. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Bajabiri, you are right..ni vizuri kujua tuko na watu ambao wanataka evidence based world, lakini kwa TZ naona ni shida na nduo maana tunatumia kauli za kisiasa tu!
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nikisoma thread zinazohusu madaktari huwa nabaki na maswali mengi kuliko majibu!!!
   
 14. H

  Haika JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mgomo mbona bado upo? Mgomo wa serikali kutoa huduma katika hospitali zake na kuwalipa stahili zao wafanyakazi wake.
  Mie ndugu yangu tumemtoa hapo kavunjika bega, hajatibiwa wiki anapewa paracetamol, bora aende kwa wahindi
   
 15. P

  Pius Kafefa Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Jogi,

  Niseme tu kwamba nimeandika bila kusukumwa na mtu isipokuwa kwa nia ya kuona tatizo linajadiliwa na hatimaye kupata ufumbuzi. Hebu fikiria imefikia mahali mgonjwa anajilaumu kwa nini amekosa pesa za kulipia matibabu yake kwa njia ya rushwa! Mgonjwa anajilaumu mwenyewe. Anamlaumu ndugu yake mwenye kauwezo kidogo lakini hajaonekana kipindi hiki cha shida. Mgonjwa anasema zingepatikana shilingi kadhaa kuna madaktari walikuwa tayari kunifanyia upasuaji. Mgonjwa analia kwa uchungu mwingi.

  Jogi,
  Ninaamini kwamba mgonjwa, na hata binadamu yeyote, akifikia hatua hii anakuwa kwenye kiwango cha juu kabisa cha utambuzi. Hachukulii matatizo yake yanatokana na wengine bali yeye mwenyewe. Hamlaumu mama yake, baba yake, serikali, wala mazingira. And at last this very person surrenders to God! He/she starts to prepare himself/herself for life after death!
   
 16. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Haika, POLE..lakini jambo hilo ndilo la kujiuliza, je unadhani MOI hakuna madaktari?Tiba(huduma)?..kama watu wanaweza kupeleka wagonjwa private sector sidhani kama wanashindwa kulipia huduma serikalini... Swali ni hili, Je, hata wakilipia hiyo/hizo huduma watapata?
   
 17. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sure thing Mkuu, unaweza kuwa na stress ajabu! ila cha msingi ni hekima ya kutumika.
   
 18. P

  Pius Kafefa Member

  #18
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Ukitoa rushwa kwenye hospitali ya umma unahudumiwa. Anayeenda kwenye hospitali ya umma anafuata huduma nafuu au madaktari bingwa. Mgonjwa mwingine aliniambia wenye bima za afya hawapati shida sana pale MOI. Wanafanyiwa upasuaji haraka.
   
 19. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Serikali ilishasema (JK) kwamba hawana kitu cha kuongea na madaktari, kama daktari haridhiki na achomoe aende atakako. Na kweli wengi sana wameenda nje kuhudumiwa mara saba ya hapa, wanawacheka waliobaki. Hao waliobaki ni kwa sababu hawataki kwenda nje ili waionyeshe serikali kwamba Tanzania sio ya wanasiasa tu, ni yetu sote. Halafu kumbuka Kayaanza mizengwe pita pinda kwamba liwalo na liwe na likawa. Madaktari wamezibwa midomo na kila atakayeongea analimbokiwa. Wote twataka kuishi, hakuna daktari mjinga wa kujining'iniza kamba shingoni wakati watu kibao wanamtegemea, na watoto wao huzaliwa uzeeni sababu miaka mingi wako shule. Waandishi umeona nao wakiisema serikali kwamba inatupeleka ndiko siko wanawadaudi. Kwa hiyo mambo kimyakimya, wananchi waendelee kuishabikia serikali yao maana imeona kwamba ndo inalipa.
   
 20. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Lakini mkuu, nini kifanyike? ...kwani hata wagonjwa unaowaona pale, wengine ni wa mikoani!! yaani wamepewa Referral tu kuja MNH or MOI sasa shida inaanzia kule kile yaani vifaa na huduma yenyewe!
   
Loading...