Majuto ni mjukuu, Unapokuwa na raisi kama Kikwete anaingiza maigizo na propaganda kwenye taaluma ni ufedhuri na mkasa mkubwa.
Unapokuwa na chama cha mafisadi kama ccm ni kuiba, kudhulumu na kuendekeza siasa za maji taka, udin, ukabila na ukanda ni mkasa kwa taifa.
Unapokuwa na vijana taifa la leo vilaza wanaoshindwa kuitetea nchi yao japo kwa maandishi, wakitumikia umaimuna wa ccm kuvichafua vyama vingine kwa misingi ya udini na ukabila ni janga lingine.
Tanzania tunabalaa kule magogoni, kiongozi mwenye hekima na busara angewaita madakitari na hata walimu, angetoka hadharani kuwaomba na si kuwalazimisha, kuwanasihi na si kuwakejeli na angetumia uwezo wake wote kuona kwamba watanzania wanapata matibabu na elimu bora.
CCm, Kikwete na vilaza wanaotumika kumtetea yeye na chama chake ni hatari kwa afya ya watanzania kama taifa kielimu, kijamii na kimatibabu.