The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 2,334
- 3,567
Nilikuwa nasikiliza kipindi cha maoni kinachorushwa na DW, ndipo nikamsikia huyu mtu anaitwa Mohamed Said akitoa maoni yake kuhusu miaka 60 ya uhuru, ingawa kabla nimewahi kusoma makala zake kadhaa, sikufikiri kwamba kwa ukubwa wa changamoto tulizonazo leo pamoja na mabadiliko makubwa ya kielimu na kimfumo bado atakuwa na mawazo kwamba waisilam wanabaguliwa.
Ninapata shida kumwelewa kwa sababu kwa taifa letu lilipofikia ningeweza kusema kama ni ubaguzi unaopaswa kupambana nao ni ule unaopendelea chama tawala.
Ubaguzi anaosema waisilam wanabaguliwa ni wa kufikirika sana. Sijui kama huyu ndugu amefanya utafiti kujua wakristo na waisilam wanaosota na kubaguliwa kwa sababu wao sio CCM!!.
Akiwa anasema hayo wapo viongozi wa kiisilam wengi tu wanaoshiriki uharamia wa kuwabagua ndugu zao ilimradi tu sio CCM.
Nashauri aache mambo ya kukaririshwa kwamba waisilam wanaonewa hizo hoja zilishapitwa na wakati. Isitosha zinafanya waisilam waonekane wanyonge na watu wa kuhurumiwahurumiwa tu.