Modem yangu ya tccl hataki ku-connect | JamiiForums | The Home of Great Thinkers
Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN
Modem yangu ya tccl hataki ku-connect
Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Jayfour, Sep 18, 2011.
1. Jayfour
Jayfour Senior Member
#1
Sep 18, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Modem ni ''huawei ec 122'' cdma, haina sim card ingawa ina sehemu ya kuweka sim card.
2. Kang
Kang JF-Expert Member
#2
Sep 18, 2011
Joined: Jun 24, 2008
Messages: 5,121
Likes Received: 616
Trophy Points: 280
Chomoa Stick, Uninstall software ya modem (Dashboard whatever) ,restaret pc, chomeka stick, install upya.
Kama hiyo dashboard in sehemu ya kudownload updates fanya hivyo.
3. donlucchese
donlucchese JF-Expert Member
#3
Sep 18, 2011
Joined: Mar 23, 2011
Messages: 9,375
Likes Received: 3,509
Trophy Points: 280
angalia kwenye internet settingz zako ipi umeweka kama default modem. mara nyingi unakuta imejiset kwenye agere kama default modem. kwaio weka hiyo yako kama default af tuambie umefikia wapi
4. Jayfour
Jayfour Senior Member
#4
Sep 18, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Nitajaribu kufanya hivyo umeme ukirudi saa tano usiku. Nashukuru.
5. Jayfour
Jayfour Senior Member
#5
Sep 18, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
sawa, lakini kwa sasa umeme umekatika, natumia simu. nitafuatilia maelekezo yako mara umeme utakaporudi. Asante.
6. Jayfour
Jayfour Senior Member
#6
Sep 18, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
nime-uninstall, restart na kuinstall upya. Hakuna sehamu ya kudownload updates. tatizo bado lipo. nimeweka ''ttcl modem 3g'' as default internet setting lakini bado.
Hapa kwenye dashboard sehemu ambayo huwa inaonesha signal ni plain na ile icon ya pc kuna alama ya x juu yake.
Modem yenyewe ina-blink rangi ya blue all the time na haijabadili rangi kuwa kijani kama zifanyavyo modems nyingine hata mara moja.
7. Jayfour
Jayfour Senior Member
#7
Sep 18, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
nimefanya hiyo setting lakini bado.
8. Jayfour
Jayfour Senior Member
#8
Sep 19, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Wakuu bado modem yangu haitaki kuconnect licha ya kufuata maelekezo yote niliyopewa hapo juu.
Msaada plz.
9. g
gomer Senior Member
#9
Sep 20, 2011
Joined: Nov 9, 2010
Messages: 109
Likes Received: 11
Trophy Points: 35
Nenda Kwenye device manager kupitia njia yoyote ile;
Angalizo : Modem yako iwe imeichomekwa.
Rightclick My Computer na bofya manage na utaiona device manager, ibofye na ione modem;
Bofya modem listed na ingia kwenye diagnostics na query modem,
Ikiitika, hakikisha username na password ziko sawa; na ina balance ya kutosha.
La sivyo hapa ndipo unaweza kufanya uninstallation kama zilivyo nukuliwa mwanzoni na siyo dashboard.
10. Jayfour
Jayfour Senior Member
#10
Sep 20, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Asante, nitayafanyiakazi maelekezo haya pia.
11. e2themiza
e2themiza JF-Expert Member
#11
Sep 20, 2011
Joined: Mar 29, 2011
Messages: 973
Likes Received: 49
Trophy Points: 45
na pia hakikisha dialing n.o ni sawa i think its #777
12. Jayfour
Jayfour Senior Member
#12
Sep 21, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
@gomer, nimefuatialia maelekezo yako yote lakini sikufanikiwa. Nilijaribu pia kureinstall lakini bado imekataa. Kitu pekee kilichobadilika ni error message.
Sasa ni ''error 678: The remote computer did not respond''
Kwenye device manager inaonesha iko sawa. Na nimeshindwa kuweka salio la kutosha kwa sababu ya kushindwa kurespond.
@e2themiza, hiyo #777 ipo lakini bado matokeo ni yale yale.
13. NEW NOEL
NEW NOEL JF-Expert Member
#13
Sep 21, 2011
Joined: May 21, 2011
Messages: 837
Likes Received: 110
Trophy Points: 60
Nenda kwenye settings hakikisha ziko sawa
1#777 ipo
2 073....@ttclmobile ipo
Password:ni namba zinazofuatia baada ya namba 4 za kwanza.
Kama yote unafanya na inakataa tazama window unayotumia kama ni window 7 au xp itakubali
14. Jayfour
Jayfour Senior Member
#14
Sep 21, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
nimeangalia setting, namba zote hizo zipo, nimefuta password na kuiandika tena upya yaani the last 6 digits. windows niitumiayo ni xp lakini bado imekataa, inaleta error sms #678: ''The remote computer did not respond''
15. g
gomer Senior Member
#15
Sep 21, 2011
Joined: Nov 9, 2010
Messages: 109
Likes Received: 11
Trophy Points: 35
Ingia Network Connections;
Chagua dialup icon yako;
Rightclick na chagua properties;
Kwenye General tab, bofya configure...;
kwa hardware features tick vibox viwili vya mwanzo na bofya OK;
tick show .... ;
kwenye security tab security options chagua typical na allow unsecure... bofya OK;
Angalizo : Hakikisha unapata signal za ttcll.
16. Jayfour
Jayfour Senior Member
#16
Sep 21, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
nimefanya yote hayo, lakini bado. Hii modem sijawahi kuona signal. ile sehemu ambayo huonesha signal, hakuna kitu pale ni plain. tatizo kubwa ndio hilo la signal. Modems nyingine huonesha signals hata kama ni weak yaani edge, lakini hii haijawahi kudisplay signal ya aina yo yote licha ya kimulimuli cha kibluu kuwaka wakati wote.
Hata kuongeza salio nimeshindwa kwani hakuna kinachorespond. Inakuwa kama naongeza salio simu isiyokuwa kwenye coverage.
17. g
gomer Senior Member
#17
Sep 22, 2011
Joined: Nov 9, 2010
Messages: 109
Likes Received: 11
Trophy Points: 35
Connect kupitia network connection kwa kubofya ZTE Wire.... icon;
Model ya modem,OS, Location?
18. JS
JS JF-Expert Member
#18
Sep 22, 2011
Joined: Sep 29, 2009
Messages: 2,065
Likes Received: 18
Trophy Points: 135
Simple solution: beba modem yako na laptop yako wapelekee ttcl wakutengenezee ukiwa unaona. Ikikataa wakupe nyingine. Kumbuka kubeba risiti kama walikupatia wakati unainunua.
19. LordJustice1
LordJustice1 JF-Expert Member
#19
Sep 22, 2011
Joined: Jan 19, 2011
Messages: 2,264
Likes Received: 10
Trophy Points: 0
Ni tccl au ttcl wandugu?
20. Jayfour
Jayfour Senior Member
#20
Sep 22, 2011
Joined: Feb 20, 2011
Messages: 115
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
hatimaye imekubali kwenye laptop! Nilichofanya nimetumia dashboard ya airtel. nilichomeka modem ya airtel huawei e153, na nikachomoa na kuchomeka ya ttcl. Sikuamini macho yangu nilipoona maandishi ''cdma'' pale kwenye sehemu ya kuonesha signal ambako siku zote palikuwa plain. Kwa kuwa hii imtokea kwenye d'board ya airttel, niliamua kurestart na kuclick icon ya ttcl. dashboard ya ttcl ikadisplay na yale maandishi ya ''cdma'' yakajitokeza kuashiria sasa signal inapatikana, na nilipojaribu kuconnect ikakubali.
Nakushukuru wewe na wote mlionisaidia katika kutatua tatizo hili. Nimejifunza mengi pia.
Modem ni ya ttcl, huawei ec 122; os ni windows xp; location: kigamboni-dar.
Asanteni sana.
Loading...