KERO Mochwari Muhimbili nao wanakula kwa urefu wa kamba?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Andrew123

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
7,861
9,963
1. Majuzi nilipata msiba wa Kaka yangu hapo Muhimbili basi akapelekwa Mochwari.

2. Siku ya kutoa maiti kwa ajili ya ibada na Maziko (mhudumu anataka TSH 200,000) mbali na zile gharama ambazo tulililipia na kupewa risiti halali.

3. Wale wahudumu kama hujatoa pesa ya chai utashinda kutwa nzima hapo uking'aa sharubu na tena unafukuzwa kama Mbwa na jeneza ulilokuja nalo.

4. Hakika, Mochwari Hospitali ya Taifa (Tanganyika) mnastahili tuzo ya Nobel ili dunia itambue mchango wenu na Prof wa Milo miwili kwa wiki
 
1. Majuzi nilipata msiba wa Kaka yangu hapo Muhimbili basi akapelekwa Mochwari.

2. Kimbembe siku ya kumtoa kwa ajili ya ibada na Maziko.

3. Wale wahudumu kama hujatoa pesa ya chai utashinda kutwa nzima hapo uking'aa sharubu na tena unafukuzwa kama Mbwa.

4. Hakika Mochwari Hospitali ya Taifa (Tanganyika) mnastahili tuzo ya Nobel.
Kwanza kabisa. Pole Mkuu kwa Msiba wa kaka yako. Muumba akuongezee nguvu katika wakati mgumu.

Kweli mochwari kuna changamoto. Aisee. Hili ni buzi lisilo na kamba.
 
Ni mikoa yote tu, miaka kadhaa nyuma, kuna huyo mwingine tuli mtaarifu mchana kuwa tuna tegemea kupokea maiti ya ndugu yetu inaingia usiku kutoka Dar, katika wilaya moja ya Mkoa wa iringa. Akatuambia yeye hata kuwepo zamu yake inaisha saa tisa na nusu kwa hiyo akampigia ambae atakuwa zamu akampa taarifa kuwa kuna maiti inategemea kuingia ule usiku akasema sawa. Tukafanya malipo ya siku mbili kwamba akifika atakaa huo usiku na kesho yake. Tuna tegemea kuzika kesho kutwa yake.

Sasa baada ya maiti kuingia huo usiku pamoja na msafara tumefika mochwari, hakuwepo kwa sababu tulikuwa tumepewa namba yake mchana ikabidi tumpigie kwa kujua labda alikuwa maeneo yaleyale ya hospital, cha kushangaza tuna mpigia simu anasema ni kweli yuko zamu ila kuna sehemu ameenda kwa hiyo tumtoe katika jeneza tumu weke kwenye sakafu ya mochwari, kwa sababu kuna baridi sana maiti haita haribika yeye atakuja kumhifadhi asubuhi. Ndugu na jamaa waliyo kuwepo pale mochwari, walichukia sana kusikia ndugu yao awekwe kwenye sakafu akae mpaka asubuhi ndo aje kuhifadhiwa.

Tuka muomba sana, atuelekeze alipo kwa sababu tuko na magari tumfuate ule usiku ila alikataa katakata kutuelekeza alipo, na mwisho wa siku alituzimia simu, kwa hiyo tukapata adhabu yakukaa na maiti ikiwa kwenye jeneza hadi asubuhi na ile baridi mpaka alivyorudi saa 12 asubuhi. Kuja kuongea nae vizuri ni kama alitaka hongo ili aje kumhifadhi halafu aendelee na mambo yake.
 
Pole Sana.
 
Wakati mawaziri wanachukua Dola milioni kwa kuuza bandari ambayo siyo Mali Yao, Kuna shida gani kumshikisha mortuary attendant msimbazi mmoja atengeneze maiti vizuri. Halafu wale akili zao sio nzuri hata wafanyakazi wa TAKUKURU wakifika pale wanakuwaga wapole na wanaacha Asante.

Bila hivyo maiti itakua haitizamiki. Kipindi mkuu wa Muhimbili Ni yule mama wa Mewata Kuna siku kidogo wamtoe upepo. Kumbe wale wajinga hata mkurugenzi wao hawamjui.
 
1. Majuzi nilipata msiba wa Kaka yangu hapo Muhimbili basi akapelekwa Mochwari.

2. Kimbembe siku ya kumtoa kwa ajili ya ibada na Maziko.

3. Wale wahudumu kama hujatoa pesa ya chai utashinda kutwa nzima hapo uking'aa sharubu na tena unafukuzwa kama Mbwa.

4. Hakika Mochwari Hospitali ya Taifa (Tanganyika) mnastahili tuzo ya Nobel.
Binadamu wa ajabu sana. Hivi unawaonea wivu hata hawa watu wa MOTUARY? Watu wanaosetiri miili ya ndugu zetu?

Tuwe serious jamani na mambo mengine, siyo lazima tuandike humu. Hivi wewe mtoa mada unaweza kufanya ike kazi hata ukipewa mshahara kama CEO wa Muhimbili?

Nakusihi utubu tu kwa kuwa hujui maiti yako itadhalilika vipi ukishakufa
 
Ni mikoa yote tu, miaka kadhaa nyuma, kuna huyo mwingine tuli mtaarifu mchana kuwa tuna tegemea kupokea maiti ya ndugu yetu inaingia usiku kutoka Dar, katika wilaya moja ya Mkoa wa iringa. Akatuambia yeye hata kuwepo zamu yake inaisha saa tisa na nusu kwa hiyo akampigia ambae atakuwa zamu akampa taarifa kuwa kuna maiti inategemea kuingia ule usiku akasema sawa. Tukafanya malipo ya siku mbili kwamba akifika atakaa huo usiku na kesho yake. Tuna tegemea kuzika kesho kutwa yake.

Sasa baada ya maiti kuingia huo usiku pamoja na msafara tumefika mochwari, hakuwepo kwa sababu tulikuwa tumepewa namba yake mchana ikabidi tumpigie kwa kujua labda alikuwa maeneo yaleyale ya hospital, cha kushangaza tuna mpigia simu anasema ni kweli yuko zamu ila kuna sehemu ameenda kwa hiyo tumtoe katika jeneza tumu weke kwenye sakafu ya mochwari, kwa sababu kuna baridi sana maiti haita haribika yeye atakuja kumhifadhi asubuhi. Ndugu na jamaa waliyo kuwepo pale mochwari, walichukia sana kusikia ndugu yao awekwe kwenye sakafu akae mpaka asubuhi ndo aje kuhifadhiwa.

Tuka muomba sana, atuelekeze alipo kwa sababu tuko na magari tumfuate ule usiku ila alikataa katakata kutuelekeza alipo, na mwisho wa siku alituzimia simu, kwa hiyo tukapata adhabu yakukaa na maiti ikiwa kwenye jeneza hadi asubuhi na ile baridi mpaka alivyorudi saa 12 asubuhi. Kuja kuongea nae vizuri ni kama alitaka hongo ili aje kumhifadhi halafu aendelee na mambo yake.
🙄🙄🤔
 
Back
Top Bottom