Mo Ibrahim 2010 wakosa mshindi

Lunanilo

JF-Expert Member
Feb 15, 2008
370
13
Hi Guys,

So No former African leader qualified for the Mo Ibrahim Money again this year. May be he should start to give it posthumously, he can get a couple of good presidents.
 
Hi Guys,

So No former African leader qualified for the Mo Ibrahim Money again this year. May be he should start to give it posthumously, he can get a couple of good presidents.

LOL!!!! Not even Benjamin or Daniel again?
 
Naye ana agenda zake za siri. Haiwezekani Marais wote wakawa vilaza kiasi hicho for 2 consecutive years!
 
Naye ana agenda zake za siri. Haiwezekani Marais wote wakawa vilaza kiasi hicho for 2 consecutive years!

Mheshimiwa Maarifa, wao wanaona kuwa hakuna hata mmoja ambae anastahili kupata hiyo tunzo; pengine kama wewe una jina la mmoja ambae wao wamemsahau tafadhali wasaidie!! Jinsi watawala wa Afrika wanavyolihujumu bara hili , kwavigezo vilivyowekwa na MO Ibrahim foundation sioni kama for the coming twenty years kuna mtu atapata hiyo tunzo!!
 
Kutokana na vitu vichache ninavyosoma kuhusu Mizengo Pinda ( nina pata picha kuwa siyo mpenda rushwa wala makuu kutokana na baadhi ya habari nilizosoma awali kuhusu M. Pinda) labda akistaafu anaweza kufikiriwa maana nadhani mawaziri wakuu nao wamo katika viongozi wanaofikiriwa kupata hilo tuzo.

Hivi hali ngumu ya uchumi duniani haijamkumba huyo bwana Ibrahim? Najua naweza kuwa aliweka pembeni hizo pesa lakini nahisi labda nazo hazizalishi faida ya kutosha. Just thinking loud.
 
Nothing changed hakuna rais aliyestaafu toka mwaka jana. waliostaafu wote waliopo ni wala rushwa.
 
Monday, 14 June 2010

ibrahim.jpg

Tuzo ya Mo Ibrahim

Sadick Mtulya

KWA mara ya pili mfululizo tuzo ya Mo Ibrahim, ambayo hutolewa kwa rais mstaafu aliyeongoza nchi kwa utawala bora, haitapata mshindi kutokana na wastaafu kutokidhi vigezo vinavyohitajika.

Kukosekana huko kwa mshindi kunatokana na kamati ya tuzo kushindwa kupata jina la rais mstaafu aliyekidhi vigezo hivyo ambayo huambatana na mabilioni ya fedha.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, kikao cha kamati ya tuzo kilichofanyika juzi kimeshindwa kuteua jina kutokanana kukosa rais mstaafu anakidhi vigezo vinavyohitajika mwaka huu.


Mwaka jana kamati ya tuzo ilitangaza kuwa itahakikisha kuwa mwaka huu inamtafuta kiongozi mwenye vigezo bora zaidi ikilinganishwa na tuzo zilizopita.


''Bodi ya Mo Ibrahim inaheshimu maamuzi ya kamati ya tuzo ya kutochagua mshindi wa mwaka 2010. Kamati hii ni chombo huru kutoka ndani ya bodi, kinajitegemea katika maamuzi yake.


''Hata kama kuna mshindi ua hakuna, madhumuni ya taasisi ni kuweka changamoto kwa viongozi wa Afrika na dunia ili kuboresha utendaji na kuhamasiaha utawala bora kwa viongozi.


''Vigezo vya kupata tuzo ni vingi, na idadi ya viongozi wanaostahili kushinda tuzo kila mwaka ni ndogo, hivyo ni rahisi kwa mwaka kukakosekana mshindi na inawezakana hata mwaka ujao akakosekana mshindi pia," inaeleza taarifa hiyo.


''Pamoja na kwamba takribani nchi 80 za Afrika zimeboresha utawala bora, zimeshindwa kumudu kuboresha uchumi wa nchi pamoja na maendeleo ya nchi zao."


Tuzo ya Mo Ibrahim hutolewa baada ya miaka mitatu kwa marais wastaafu ambao waliingia madarakani kwa njia ya kidemokrasia na waliachia madaraka kwa hiari yao mara baada ya kumaliza vipindi vya uongozi kwa mujibu katiba ya nchi zao.


Mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa ni rais mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano, mwaka 2007 ambaye alifuatiwa na rais mstaafu wa Botswana, Festus Mogae mwaka 2008.


Katika hatua nyingine taasisi hiyo imeanzisha mfuko wa mafunzo ya uongozi wenye lengo la kuawaandaa viongozi wapya wa bara la Afrika kwa kutumia taasisi mbalimbali.


Mpango huo unatarajiwa kuvutia idadi kubwa ya watu wenye taaluma na vipaji watakaoongoza taasisi kwa ajili ya kuboresha na kufikia malengo kadhaa ya Waafrika
.

"Kwa sasa taasisi ya Mo Ibrahim inashirikina na taasisi nyingine za Afrika kuweka utaratibu wa jinsi mpango utakavyofanya kazi.

Mpango huu utazinduliwa rasmi nchini Mauritius mwezi Novemba mwaka huu,'' inasema taarifa hiyo.


''Lengo la kuhakikisha Afrika inapata viongozi bora pamoja na kuwa na utawala bora ni muhimu kuliko kitu kingine. Haya yatasaidia Afrika kuwa na uchumi ulio imara utakaoboresha maisha ya kila mmoja,'' inasema taarifa hiyo.


Mo Ibrahim 2010 wakosa mshindi
 
uyu mo ibrahim ni mpenda sifa tu hana lolote, anawapa hela marais matajiri badala ya kupeleka hela kwa wakimbizi huko Darfur na kwa waarabu wenzie palestina huko, masifa tu anatafuta kutengeneza jina...hana maana, hapo ndo huwa nasema waarabu kweli hawapendani wao kwa wao...hana maana yoyote, hawa ndo watafuta sifa kama alivyo Mo Dewij wa tz.
 
hivi anafikiri marais wa africa wanafanya kazi wakianticipate hiyo bahati nasibu yake...hiyo ni akili fupi. ..ndo maana m7 alimwambia to hell is your billions...yeye hafanyi kazi kwaajili ya pesa, anafanya kazi kwaajili ya wananchi...waarabu bwana...dah!
 
hivi anafikiri marais wa africa wanafanya kazi wakianticipate hiyo bahati nasibu yake...hiyo ni akili fupi. ..ndo maana m7 alimwambia to hell is your billions...yeye hafanyi kazi kwaajili ya pesa, anafanya kazi kwaajili ya wananchi...waarabu bwana...dah! wanapenda kufanya jambo waonekane,...thawabu nzuri ni ile unayotoa roho za watu zikakushukuru ndo utapata baraka kwa Mungu..angetoa ayo mahela yake kwa wapalestina, kwa watu kule Darfur,kwa watu kule congo etc ni nyingi sana na wangemshukuru...yeye anatarget rais mmoja tena tajiri...hivi anafikiri marais wanafanya kazi kweli wakiweka mawazo ya iyo bahati nasibu yake?
 
uyu mo ibrahim ni mpenda sifa tu hana lolote, anawapa hela marais matajiri badala ya kupeleka hela kwa wakimbizi huko Darfur na kwa waarabu wenzie palestina huko, masifa tu anatafuta kutengeneza jina...hana maana, hapo ndo huwa nasema waarabu kweli hawapendani wao kwa wao...hana maana yoyote, hawa ndo watafuta sifa kama alivyo Mo Dewij wa tz.


Inawezekana huyo Mo Ibrahimu anatafuta sifa. Hata hivyo suala la tabia zake sidhani kama linaingilia mambo ya utoaji wa hii tuzo. Kwa hiyo mimi naiangalia habari kwa upande wa viongozi wetu zaidi kuliko personality ya huyo billionea!
 
Hi Guys,

So No former African leader qualified for the Mo Ibrahim Money again this year. May be he should start to give it posthumously, he can get a couple of good presidents.

That there are no takers for this award is very unfortunate and telling. Ni wazi kwamba majority of the leaders hata posthumously wako tainted na corruption, murder just to name a few.
We are in for a long wait. Eti a selfless African leader?!!! NKT Hajazaliwa bado.
 
huwa sizielewi izi tuzo na hao mabilionea wanaotoa hizi tuzo!!
 
Back
Top Bottom