Mo Dewji amrejesha Simba Barbara Gonzalez kama Mjumbe wa Bodi

Mo Dewji amrejesha Simba Barbara Gonzalez kama Mjumbe wa Bodi

Mo kaamua kuinawa simba SC ndiyo maana hatuoni usajili wa kutisha, mwekezaji kaamua kuondoa shilingi
 
Ni wakati wa,Mangungu kujiuzulu na wajumbe wake wote ili wapatikane wapya. Simba imekuwa inavuja upande ule wa wanachama na kupitia kwa watu kama kina Salim. Bila wale kubadilishwa, Simba itaendelea kutetereka.

Juzi Mangungu anakomaa kuwa management ya Simba na Bodi haihusiki na uvujaji wa jezi na kwamba eti wao hawajaziona jezi hadi zilipokuwa zinatambulishwa, yaani anaonyesha uongo wa kitoto kabisa na dharau za wazi kwa wanasimba kwamba hawana akili.
 
Rais na Mwekezaji wa Simba SC ametangaza mabadiliko makubwa ya kiuongozi ndani ya klabu hiyo, akibaki na nafasi yake ya Rais lakini akikabidhi Uenyekiti wa Bodi kwa kiongozi mpya kutokana na majukumu yake mengine na kutokuwepo mara kwa mara nchini.
View attachment 3465011
Kupitia taarifa rasmi, amesema ni muhimu Simba ipate mwenyekiti ambaye yupo karibu na shughuli za kila siku za klabu. “Nitaendelea kubaki kama Mwekezaji na Rais wa Simba SC, lakini nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi sasa inakabidhiwa kwa kiongozi mpya,” ameeleza.

Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Katiba na Kanuni za Kampuni (MEMARTS) ya Simba Sports Club Company Limited, Ibara ya 41, amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC.
View attachment 3465012
Aidha, ametangaza wajumbe wapya wa Bodi upande wa Mwekezaji ambao ni, Barbara Gonzalez aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Simba mwaka 2020, na kuwa kama CEO wa kwanza mwanamke katika historia ya klabu hiyo

Safu ya Wajumbe wa Bodi ni:
• Barbara Gonzalez
• Hussein Kitta
• Azim Dewji
• Rashid Shangazi
• Swedi Mkwabi
• Zuly Chandoo
• George Ruhango


View attachment 3465001
'Try again' out?
 
Barbra anaandaliwa agombee uenyekiti upande wa wanachama
 
Back
Top Bottom