Mnyika umesema, wao wamethibitisha!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika umesema, wao wamethibitisha!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Jun 29, 2012.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Leo tunashuhudia siku ya saba watanzania wakitaabika kwa kukosa huduma ya matibabu. Je, wenye dhamana wanasema nini? – tumefanya kila jambo imeshindikana, hatuwezi kusema lolote jambo hili liko mahakamani, tume imeundwa…. Udhaifu huu wanaounesha viongozi wetu ni mkubwa kuliko alivyosema Mnyika.

  Techinicalities and protocol aside watu wanakufa jamani - haitoshi kutupa majibu haya yasiyo na mshiko hivi mmetaarifa magonjwa yasubiri kwani jambo hili liko mahakamani.

  Kwa hili nasema mihimili yote sasa imethibitisha udhaifu mkubwa na kutokujali wananchi wake - mbunge wangu naomba jibu kama jambo liko mahakamani nimwambie nini mgonjwa wangu?
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Sisi Watanzania tunaongoza kwa "umbumbumbu". Kwa hili suala la Madaktari hasa baada ya mbinu kandamizi za kutaka kuua viongozi wa madaktari tulitakiwa tuonyeshe kwa vitendo kutokubaliana na kinachoendelea. Ajabu naona WATU wanaendelea na shuguli zao Kama kawaida. Du umbumbumbu hatari unaenda kazini wakati hujui ukipata tatizo utatibiwa wapi.....ajabu na kweli. Unapanda boda boda kweli hii leo...mmmh umbumbumbu umetujaaa. Mbunge unazunguka na kiti bungeni wakati hospital imefungwa...du haya ni maajabu.
   
 3. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jibu Serikali dhaifu, Raisi Dhaifu na waoemu dahifu
  majibu yamepatikana
   
 4. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kwa 100%.

  Nafikiri Taifa hili liko chini ya laana! Kuna mambo yanayotukia katika nchi hii ambayo kwa nchi za wenzetu MOTO UNGELIKUWA UNAWAKA lakini kwa Mitanzania imenyamaza tu kama mikondoo! Hii ni laana ya CCM ambayo imesababisha taifa hili kuwa la majuha ambao hawajui wanafanya nini na kwanini wapo hapa duniani tena kwenye nchi iliyojaliwa utajiri usiomithilika.

  Hili swala la mgomo wa Madaktari na kufuatia KUTEKWA NA KUTAKA KUULIWA KWA KIONGOZI WA MADAKTARI ingekuwa ni nchi za wenzetu watu wangelikuwa walishaandamana nchi nzima kupinga ujinga huu.

  Watanzania wamelishwa kilevi au madawa ya kulevya yanayoitwa UPENDO,AMANI NA MSHIKAMANO. Yote haya ni mambo ya kufikirika tu wala hayapo miongoni mwetu. Hivi unategemea Serikali inayoweza kumteka na kumwua raia wake kwa vile tu hakubaliani nayo kwenye maswala ya msingi ni serikali yenye dhamira ya upendo,amani na mshikamano wa kweli???

  Jibu ni a BIG NO!
   
 5. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wamepoliziwa mapepo, hawajitambui, wakipewa kanga na fulana na kofi kwishney, Kazi kukimbiza mwenge tu.
   
 6. The Bleiz

  The Bleiz JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 3,643
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Watanzania ni dhaufu we normally sit there n wait kundi fulani au chama fulani kije kutatua matatizo yanayotukabili ,kwa staili hii tutangoja milele. Ccm itatuburuza mpaka cku tukiwa na gut ya kusimama sisi kama sisi wananchi.
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Jk ni dhaifu sana

  pinda ni mnafiki sana na ni dhaifu
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa jibu lako hili unataka kutudhibitishia kuwa hata sisi wapiga kura tunaoisimika serikali ni DHAIFU sana
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Watu wamekaa vijiweni jua kali wanapiga akili kwa nguvu zao zote namna ya kupata mlo wa ugali utumbo na mchicha halafu ukawatibue eti wanatakiwa kuwaunga mkono madaktari??

  Hii haitatokea kirahisi hata siku moja.

  Kwanza mtanzania average anamuonea wivu kila mwenye ajira.
  Kupata ajira tu kwake ni upendeleo unao zidi kipimo.

  Sijui ni vipi mtu huyu avearage atatoka kwenda kumuunga mkono mtu anayedhani ame pata upendelea unazidi kipimo??

  Madaktari si wana siasa ni watu wanao operate mambo yao kwa common logic.
  Wakati wanasisa huchukua kile watu wa ushwazi wanachoamini na kukifanya big deal

  Common logic huko ushwazi hazina nafasi kabisa.

  Swali kubwa kwa mtanzania average kila siku ni kujua katika dakika ile yeye atafaidika vipi.
  Ndiyo maana masinia ya wali na finyango za nyama yana effect kubwa kuliko madai ya kuibana serikali iboreshe mazingira ya Hosipitali zetu.
  Cha ajabu huyu mtanzania average hudai apewe mlo in real time na hadai apewe choo ili real time.
  Karibu kila mahali Tanzania watu wakisha shiba utawahurumia jinsi wanavyo haha kutafuta mahali pa kwenda kuachia mashonde yao.

  Kama nilivyo wahi kusema expectation zetu as a nation are very low below the lowest possible regular human being can think.

  kura nimekura pa kurara je?
   
 10. mkwatis

  mkwatis JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 336
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  Mimi kwa Mtazamo wangu rais dhaifu serikali dhaifu,vyama dhaifu,wananchi dhaifu na mawazo,fikra,mshikamano na umoja dhaifu hivyo ni ngoma droo,hakuna wa kulaumiwa
   
 11. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Mwambie mgonjwa wako mhamie aga khan.
  Au kama vipi panda sea express umpeleke mnazi mmoja.
   
 12. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ....waajiri wao ni dhaifu zaidi i.e wananchi...
   
 13. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Chadema bana mhh..!!walijaribu maandamano haikuleta majibu,occupy unga limited ikafeli,yaani kila kitu kibounce.mgomo wa madaktari nao unaelekea kushindwa kufikia malengo yakisiasa waliotarajia kina mnyika NDO MAANA MNYIKA KITI CHA BUNGENI ANAKIONA CHA MOTO.HATULII KILA DAKIKA .MUONGOZO.ili apenyeze suala la mgomo lijadiliwe.
   
 14. j

  jigoku JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  HAKIKA WATANZANIA HAWAJITAMBUI,Mleta mada umenifanya nifikirie sana,tena kwa utulivu mkubwa na kisha nimeamini watanzania hawajitambui,waliosoma na wasio soma wako kwenye level moja tu.

  NIMEJIULIZA SWALI MOJA TU,HIVI TUNATOKA MAJUMBANI MWETU KWENDA KWENYE SHUGHULI MBALIMBALI,ZA AJIRA SERIKALINI,KWENYE SCTOR BINAFSI,UJASIRIAMALI,KUBEBA ZEGE,KUUZA MBOGA MBOGA,KUSAFIRISHA ABIRIA NK,HIVI LEO UKIWA KWENYE SHUGHULI ZAKO BAHATI MBAYA UKAUMIA UTATIBIWA WAPI?HIVI UKAUGUA UTATIBIWA WAPI?
  Eti leo wananchi wanajiita wajanja watu wa DAR,tupo tunaendelea na mambo yetu,kweli waTZ hatujitambui.
  Nilidhani tungelikuwa tunaidai serikali huduma za afya zirejeshwe.

  Ila hata Mibunge yetu nayo hakuna kitu,hasa ya Magamba,maana ndio wanaopinga hoja hiyo isijadiliwe bungeni,hivi wanawezaji kuzunguka kwenye viti wakati waliowachagua hawana huduma?hivi kazi yao ni kuisimamia serikali na serikali hiyo imeshindwa kutoa huduma wao wako kimya tu,hivi wingi wa wabunge wa CCM wakiweka shinikizo hoja hii haitajadiliwa?suluhu si itapatikana?
  Kweli wa TZ hatujitambui
   
 15. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni athari za umasikini uliokithiri kwenye nchi, kiasi kwamba umegeuka kuwa mtaji wa viongozi na CCM kuendelea kuwepo madarakani!
   
 16. H

  Hebron Caleb JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 237
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema kuwa atatoa tamko la serikali jana lakini jana hakufanya hivyo. Aliahidi wakati yeye kama Kiongozi wa nafasi juu serkalini akijua kuwa alikuwa anaingilia muhimili mwingine. Ni ajabu kuwa na viongozi wanaotupeleka mahali ambapo hawapajui. NASIKITIKA SANA!!!
   
 17. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hii serikali ni ya kise-nge inafikiri magonjwa yatasubiri mambo ya mahakama?? huyo naibu waziri wa michezo aliyepata ajali angevunjika miguu angesubiri uamuzi wa mahakama??
   
 18. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Makoye na Wana JF,
  Tanzania tunajivunia Msingi mizuri iliyowekwa na watangulizi wetu.
  Sasa basi tusipoiendeleza hii misingi mizuri, mwisho wa siku itatoweka.
  My Take: Kuna tofauti kubwa kati ya Amani na Uvumilivu. Amani Ikitoweka na Uvumilivu ukitushinda matokeo yake ni Mashafuko.
  Nawakilisha   
 19. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kijana huyu Mnyika ameonesha siku zote uzalendo wa hali ya juu -haikubaliki wewe kupeleka suala nyeti kama mgomo wa madaktari mahakamani ili ukwepe kuwajibika na uzuie suala hili kujadiliwa bungeni eti kwa sababu suala liko mahakamani. Ndiyo maana unaona kila mwenye nia njema na nchi hii anahaha kulitafuatia jibu suala hili. kwa bahati mbaya hili ni swali gumu na haliwezi kujibiwa na majibu mepesi ya viongozi wetu, Pinda alikua mkweli alikiri kuwa amefanya kila kitu ameshindwa, hii vizuri japo alipata kigugumizi juu ya hatua ya kiungwana inayofuatia, yaani kuachia ngazi ili upishe wengine nao watende.Kwa mkuu yeye amebaki na majibu mepesi kuwa kama daktari hutaki kazi achia ngazi - hili anajua ni jibu jepesi na la kinyonge na pia litaendeleza tu vifo kwa watanzania waliokosea kufikiri anawajali. Ukisikia kauli za viongozi wadini leo inakuambia kila mwenye nia njema na mtanzania anaumizwa na hali hii isipokuwa wenye dhamana
   
 20. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tz tulipata uhuru bila ya tone la damu kumwagika na mkoloni mweusi ccm ataondoka 2015 bila kupenda .
   
Loading...