View: https://youtu.be/DIC_ozvSnF0?si=_mnodMkKoiaxJMuU
➡Ofisi ya Msajili wa vyama siasa imeendelea kujaribu kuendelea kuichokonoa CHADEMA kwa kumtaka katibu mkuu kujibu hoja za yule mwanachama wa CHADEMA aliyelelamika kwamba kikao cha Baraza Kuu kilichothibitisha uteuzi wa
katibu mkuu, manaibu katibu mkuu (Tanganyika na Zanzibar) na wajumbe wateule wa kamati kuu uliofanywa na Mwenyekiti Tundu Lissu hakikuwa na akidi inayotakiwa ya 75% ya wajumbe wote na hivyo katibu, manaibu makatibu hao na wajumbe wateule hao wa kamati kuu ni batili, si halali....
➡Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika ktk video hiyo anamjibu mwanachama huyo na msajili wa vyama vya siasa kupitia vgombo vya habari kwa kuwa yeye msajili naye katoa madai yake hayo kupitia njia hiyo hiyo...
➡Aidha Katibu Mkuu John Mnyika, amemtaka MsajilI wa vyama vya siasa aeleze umma wa Watanzania amechukua hatua gani kwa CCM ambacho kimevunja katiba yake waziwazi huku wanachama wake wakilalamika kwa kitendo hicho cha kumpitisha Bi Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea u - Rais 2025 na Dr Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wake kinyume cha taratibu na katiba yao....
➡Na mwisho, amemtaka Msajili wa vyama vya siasa aueleze umma wa Watanzania hatua alizomchukulia Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Amosi Makalla kwa kitendo chake cha kuropoka uongo hadharani kuwa CHADEMA kupitia kampeni yake ya TONE TONE ina mpango wa kutumia fedha hizo kwenda kununua virusi vya Ebola na M- POX na kuviingiza nchini....
➡Amesema, kauli hii ya Amos Makalla ni uongo wa kijinga, kipuuzi na unahatarisha usalama wa taifa kwa sababu umezua taharuki kwa wananchi na kwa wageni wanaingia nchini kwetu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo utalii, biashara nk
➡Mwisho, Katibu Mkuu John Mnyika amewataka wanachama na wana CHADEMA na wapigania mabadiliko kutokukubali kuondolewa na kuhamishwa kutoka kwenye focus ya mapambano ya kupigania mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi kupitia katiba, sheria na kanuni ili kuhakikisha nchi inakuwa na katiba, sheria na kanuni bora na za haki kwa watu wote ktk kuhakikisha tunakuwa na chaguzi za WAZI, HAKI, HURU na za KUAMINIKA ili kila mwanachi aone kura yake ina thamani, inahesabikia na inahesabiwa ktk kuchagua viongozi wao...
Mtazame na msikilize ☝🏻☝🏻☝🏻