Hivi tatizo la maji limeanza wakati wa uongozi wa Mnyika? Km ccm waliongoza jimbo hilo karibu miaka 50 na wao ndy serikali yao inakusanya kodi na hawakuweza kulitatua, je miaka 5 ya Mnyika na hujuma wanazofanyiwa wabunge wa upinzani na wakurugenzi wilaya ya kuzuia miradi ya maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani hamuoni???
Mwezi February ITV walirusha kipindi maalum kuhusu tatizo la naji Dar es salaam na hasa ubungo kwa waliofuatilia watajua tatizo sio mbunge, mnyika amefanya jitihada kubwa sana kutatua kero ya maji ubungo lakini tatizo liko ngazi ya wizara.
Lakini kwa waliomsikiliza pro.Maghembe jana wakati wanakabidhi vifaa vya kuchimbia visima watajua ratizo la maji ni la kisera na vipaumbele vya wanaokusanya kodi.
Suala sio tatizo lipo wapi, suala ni kuwa akiyatambua mazingira yote uliyosema Mnyika alisema wabunge waliopita hilo swala wamelishindwa kwa sababu hawakuwa na uchungu na wanaanchi na hawana mbinu mpya lakini yeye anayo dawa ya tatizo hilo.Na kuwa wananchi wana kazi moja tu ya kumpa kura kisha hayo matatizo ya naji yatakuwa historia ndani ya miaka mitano.
Hivyo hiyo ni ahadi ya Mnyika kwa wapiga kura wako.Wana haki kumdai maana ahadi ni deni.
Wakati anatoa ahadi alijua kuwa wabunge waliopita wameshindwa kwa sababu ya serikali, yeye aliahidi ahadi hiyo akiyajua mazingira yote hayo hivyo kama sio muongo basi tayari alikuwa anajua ata pamoja na changamoto hiyo talitatuaje hilo tatizo.Kaaminiwa ,akapewa kura hivyo huu ni mwaka wake sasa kuonyesha kuwa je anaaminika?je katimiza alichosema?
Wana haki kumhoji maana isije ikawa ndio ile ya kuongea mbali, kutenda mbali.Tunataka wanasiasa wanaoahidi wanachokiweza kutekeleza.Vinginevyo huo ni uongo ambao hakubaliki kwenye siasa za kisasa.
Nadhani hiyo ndio hoja ya mtoa mada.