Mnyika Mbunge wangu, ya wengine unayajua, yako je?

UBUNGO YETU

Member
Feb 19, 2015
35
6
Tumekuwa tukilaumu sana safari za J.Kikwete Ulaya na kusahau kutembelea na kutatua matatizo ya wananchi wake, hali hii napenda niifananishe na Mbunge wangu Mnyika yeye kila siku kimguu na njia ila mtaani kwetu haonekani.

Hatujakuchagua kuwa mbunge wa magazeti, kumbuka ni sisi wana Ubungo tuliokufanya ufikie hapo.

Nawasilisha na hii ni maalumu kwa wana Ubungo

Inafika wakati mtu unajuta kumchagua mtu fulani kuwa kiongozi wako,yaani unakaa muda wote huo huji hata kusikiliza kero zetu.Yapi uliyoahidi umetekeleza?

Nakuambia hivii,tutakutana kwenye sanduku la kura, sipigii chama napigia mtu kulingana na uwezo wake wewe naon umeshindwa.

Yani hata sasa hivi kuelekea uchaguzi mkuu umeshindwa kuja kujigonga? Tunakusikia mara mwanza mara Mtwara au hao ndio waliokuchagua.

Hivi unashindwa kuiga mfano wa Ndesamburo watu wa Moshi kwa raha zao,we kazi kupiga domo kwenye majimbo ya wengine.
 
Ninaishi Ubungo.Ingawa sikatai kunaweza kuwa na changamoto za hapa na pale zinazosababishwa na serikali lakini Mnyika amefanya kazi kubwa sana kwa kipindi cha miaka 4 ya Ubunge wake.Hakuna mbunge yeyote wa CCM ameweza kuyafanya haya kwa miaka yote iliyopita.

Ukitaka kujua wabunge vimeo fanya ziara ya siku moja katika jimbo la Ukonga na ukirudi Ubungo utamuamkia Mnyika Shikamoo.
 
Sisi tuko jimbo la mnyika lakini huku kwetu hakupitiki mvua zikinyesha
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Nyie mnaosema mnyka kafanya meng ubungo mbona hamuyataji? Mpuuz tuu hana lolote
 
Sisi tuko jimbo la mnyika lakini huku kwetu hakupitiki mvua zikinyesha

Njoo temeke na ilala huku tunakoogelea kama samak ndo utajua kua kwenu na kwetu kupi kuna nafuuuu......mshukurun mnyika maana hata hao waliokuepo kwa miaka hamsin hawakueeza kusogea hata mita moja angalau yy kwa miaka minne katembea mita 5
 
Nyie mnaosema mnyka kafanya meng ubungo mbona hamuyataji? Mpuuz tuu hana lolote
Mbona hata wewe husemi nini hajafanya? Ccm imekuwa na jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 50. Mnataka kumbebesha lawama MTU aliekaa kwa miaka 4 tu? Tumeona mnyika akifuatilia maji mguu kwa mguu, mi nyinyiem ndo mnaweka kauzibe
 
Tumekuwa tukilaumu sana safari za JK ulaya na kusahau kutembelea na kutatua matatizo ya wananchi wake, hali hii napenda niifananishe na mbunge wangu mnyika yeye kila siku kimguu na njia ila mtaani kwetu haonekani, hatujakuchagua kuwa mbunge wa magazeti, kumbuka ni sisi wana ubungo tuliokufanya ufikie hapo, nawasilisha na hii ni maalumu kwa wana ubungo

Mimi nashangaa watu mnaolalamikia wabunge waliokaa bungeni miaka minne, ninategemea wangelalamika watu wa jimbo la ISMAN ambao mbunge wao amekaa 15 years lakini ISMAN badala ya kuwa mji ndio inazidi kuwa kijiji.
Tuacheni Ujuha.
 
Back
Top Bottom