Mleta mada anasema anakaa gongalaboto mara ubongo haeleweki..ni chzi fulani.
Halafu wewe nani mbugila au kitasa?sio mwehu ni juha
Mnyika alisema ataleta maji imekuwaje mbona mnakimbia hoja?Swala la maji dar siyo ubungo pekeyake, ni dar karibia yote. Huko Gongo la mboto alipopataja au Ukonga nzima haina maji ya bomba... Hapa tukubaliane tatizo ni serikali yetu, uliza wilaya au majimbo yote ya dar yana maji, au wewe shida yako ipi kwa mh Mnyika? ??
Maji yamemshinda sasa amehamia kwenye katiba..anatapatapa..atatukoma tunausongo nae yule tumbili we mwache tu![/QUOTE
Hayo yote msingi wake ni katiba, katiba ikiwa mbaya escrow utaendelea kuziona.
Nani unafikiri ukimchagua atakupa maji?
Ebu tutajie huyo mbadala wake mliyemuandaa,msije mkatuongezea vilaza bungeni
Mnyika alisema ataleta maji imekuwaje mbona mnakimbia hoja?
Pole sana ndugu sisi wananchi wa ubungo kwakweli tunajifunia kua na mbunge wa aina ya mnyika ambae haangalii masilahi ya ubungo pekee bali masilahi ya taifa kwa ujumla.Mnyika ni chaguo la mungu kijana huyu ameyatoa maisha yake hadi kuamua kusoma evening class kwaajili ya mabadiliko ya nchi hii kwakweli,hao watawala wanambania kuleta maendeleo ubungo hasa ya maji ambayo ndio kero kubwa ya maji sababu za kisiasa kwani wao kikubwa wanacho jali ni idadi ya uwakilishi bungeni na si maendeleo kwa taifa kwa ujumla wake,watu kariba ya mnyika ni wana
apinduzi ambao serikari yoyote yenye kuendekeza vitendo vya kifisadi hawapendi kumsapoti kisiasa hasa maendeleo jimboni kwake au kwa wapiga kura ili asionekane yeye ni mtu safi,nachelea kusema kwamba mimi kama mwananchi wa ubungo tena kimara namsapoti sana mnyika kuwa sio tu mbunge bali hata waziri au Raisi kabisa.
Paul Makonda....
Ndiyo chaguo la mleta uzi na wote wanaomuunga mkono kwenye uzi huu...
Tafakari...
Hukumbuki hata yule anayeongoza kwa uongo serikali mwaka 2012 bungeni alisema(william lukuvi) alimpa saluti kwamba kati ya watu anaowakubali wanaotumia akili bungeni ni pamoja na mnyika ? Leo ww tu unaye kesha barabarani na kofia ya kijani umchukie mnyika inawezekana ww ni chizzi
Mtoa mada yaelekea katumwa na iptl hana jipya na sisi hatuko tayari kupoteza jimbo.muheshimiwa wakati wa kampeni ya uchaguzi 2010 ulituahidi kuwa utamaliza kero ya maji ubungo, tukakupa kura zetu, tukakesha wote Mpale loyola kuhakikisha kura hazichakachuliwi, peoplez power tukalibeba na kulipindua gari la wizara ya mambo ya ndani wakati lilipolazimisha kuingia pale getini mimi Dar es salaam nimekuja mwaka 90 nilifikia gongo la mboto ambapo nakumbuka tulikuwa tunakunywa maji ya kisima na yenye chumvi, niliendelea kunywa maji ya chumvi mpaka mwisho wa miaka ya tisini ndiyo ilikuwa mwisho wa kunywa maji ya chumvi..leo karne ya 21 miaka 50 ya uhuru kwa maraya kwanza nakunywa maji ya chumvi....kweli tunasifu juhudi zako za kufichua maovu huko bungeni lakini kura zetu sahau....umeshindwa kusoma alama za nyakati kwamba wakuu wamekuundia zengwe ubungo pasipatikane maji ili uonekane hufanyi chochote......ungeweza hata kuleta maji ya kununua kwenye malori tunge appriciate uwajibikaji wako sasa huku maji hakuna hata ya kununua hakuna .....ukipata ubunge 2015 walahi natembea uchi......"maana tumechoka sasa"
Maji yamemshinda sasa amehamia kwenye katiba..anatapatapa..atatukoma tunausongo nae yule tumbili we mwache tu!
watu wa jimbo la ubungo punguzeni uoga. Unganeni muandamane kwenda makao makuu ya wizara ya maji yalipo hapo ubungo kwa lengo la kumwambia magembe na makala waamue moja, la kufungulia maji au wawape ruhusa ya kulitoboa bomba linalopita jimboni kwenu ili mjichotee bila malipo.
Mnyika mtamwonea bure kwani aliipeleka hoja binafsi ya kuitaka serikali iseme ni lini jiji la Dar litapata maji ya uhakika lakini ccm waliipoka hoja ile na kuifanya ya kitaifa.
Kukosa kwenu maji ni mbinu za ccm kumdhoofisha Mnyika kwani ni mwiba unaowachoma sana bungeni hata Makinda anamwogopa. Si ndiye aliyemwita mkulu dhaifu?. Dogo ni jembe acheni kumharibia, give him another chance na kayapasueni bomba mkinge maji ili magembe aumie kwa hatua mlizochukua.