Mnyika is the most brilliant lawmaker!


Kwani Zitto ni mbunge?
 
Si sahihi ili uwe mtunga sheria lazima uwe na degree na hata wewe kama mwanasheria hujui kigezo cha kikatiba cha mtunga sheria kinasemaje ili apate sifa ya kuwa mtunga sheria. Tuache ushabiki kwenye jema lazima tupongezane .
mkuu amesahau kua hata huyo bibi yake anayesimamia wabunge pale bungeni ni mweupe kupita maelezo linapokuja suala la kanuni na sheria
 

Mfuas wa zzt utawajua tu
 
Hotuba unaweza kuipata kwenye website ya bunge, labda ulitaka kusema nini, why can't you be straight?

Jinga lingine hili,kwenye hotuba ya JJ amelizungumzia kwa undani sakata la escrow na hata bungeni alipambana sana wakati Zitto akijitahidi kumwokoa Saada Nkuya na gavana maana bila Zitto wasingechomoka,jiulize fedha zimetolewa BOT bila waziri na gavana kuwajibika!
 

Tunao viongozi wengi wa aina ya Mh J Mnyika, tatizo kubwa la nchi yetu ni unafiki na watu kupenda kutawala bila kuleta maendeleo tarajiwa,wabunge wengi kwa unafiki wao wameweka akili zao pembeni na kujaa ushabiki wa vyama, watu kila kukicha wanapanga mipango ya nani atakuwa rais na ni vipi watashinda uchaguzi! hoja za msingi za kuliendeleza taifa zinaachwa zikielea hewani kisa katoa mpinzania, hii nchi itasonga mbele pale watu watakapojitambua hasa wananchi, wakati wa uchaguzi hakikisha unachagua mtu makini sio mtu katoka chama gani! watu kama Myika, filikunjombe na wengine wengi wanamawazo ya kimaendeleo na ndio tunapaswa kuwachagua warudi bungeni.
 

Huyo ZZK ni mtu mwongo ajabu,alisema anayo majina ya walioficha fedha Uswisi na atawataja soon,alipobanwa mbele ya kiapo kwa aibu akasema hana jina hata moja,CDM haiwezi kuvumilia ujinga huu,tuambie jina hata moja alilotaja ZZK!
 
Watunga sheria wanaitwa learned brothers and Sisters huyo mnyika hata degree hana.Acha kudhalilisha fani ya wanasheria.

Afadhali umeonesha Ujinga wako tukuelimishe. Watunga Sheria ni Wabunge ambao huwa referred as Lawmakers,unaowaita Learned Brothers and Sisters ni Lawyers (LL.B Holders). Usichanganye madesa.
Kwa taarifa tu, Mnyika ni kijana ambaye akiamua kumalizia Degree yake anaimaliza muda wowote, ni very talented person when it comes to Academic. Uwezo huo ndo unaomtofautisha yeye na Maprofessor na Wafoji vyeti wengi walioko CCM.
 

Jana kasisitiza wale walioingiziwa fedha kupitia Stanbic wafichuliwe ilhali zitto na kamati yake hawakuwakomalia,huyu jamaa amezidisha mahaba kwa zito
 

Kuwa Mwenyekiti wa PAC sio kwamba yeye ndiye kafanya kazi peke yake, yeye ni msemaji tu wa kamati, hapo iliyofaya vizuri ni kamati nzima, kuhusu hizo issue za Escroe, Richmonduli na mengine yote yalianza tangu enzi za akina Dr Slaa, so ni mwendelezo tu wa vyama vya upinzani kuibana serikali ya ccm,na sio kwamba Zitto i mahiri sana kuliko wabunge wote, Zitto yeye ni mbinafsi na huwa anataka kuonekana yeye ndiye ametenda jambo flani kwa manufaa ya umma na sio teamwork!
 
Mbona maji hajaleta Ubungo kazi kubwabwaja tu!

Yeye ndo anaekusanya kodi..? Mtafute Maghembe anaetoa ahadi kila siku.. Mada ya hapa ni uwezo mkubwa wa John katika kujenga hoja.. Mapimbi kuielewa hii ni ngumu sana..
 

Umeshasema PAC, hiyo ni kamati ndugu,si Zitto peke yake, wale 19 wangegoma hakuna kilichofanyika. Hoja ya Escrow bila wabunge wote wa Upinzani ingekuwa mvuke na ingepotea hewani,jifunze uelewe na kuelimika. Report mbalimbali za mashirika yanayotathmini mabunge, zinamtaja Mnyika kuwa Mbunge pekee mwenye Mchango Mkubwa Bungeni kuliko mbunge mwingine yeyote,na sio kwa idadi ya hoja tu,bali hoja zenye Maslahi mapana kwa Taifa hili. Zitto ana Mchango wake na Unaheshimika,lakini je!ndiye mbunge pekee aliyefukuzisha Mawaziri?
Pamoja na mahaba uliyonayo kwa Zitto, huna budi kukubaliana na Ukweli uliopo, na uwe reasonable.
 
Huyo ZZK ni mtu mwongo ajabu,alisema anayo majina ya walioficha fedha Uswisi na atawataja soon,alipobanwa mbele ya kiapo kwa aibu akasema hana jina hata moja,CDM haiwezi kuvumilia ujinga huu,tuambie jina hata moja alilotaja ZZK!

Kwa akili yako katika kipindi kile Zitto alivyokuwa kwenye misukosuko na chama chake ungetegemea tena ajiongezee maadui wengine? Aliyekuwa anaomba hayo majina si ndio Mwanasheria mkuu Werema aliyejiuzuru kwa issue ya ESCROW ambaye amepost kwenye instagram akifurahia Zitto kuvuliwa uanachama?

Kwa akili ya kawaida tu, kwa wakati ule ilikuwa sahihi kabisa kwa Zitto kusema kuwa hana majina hata kama alikuwa nayo, wewe unadhani angewataja wao wangekaa kimya!
 
Si sahihi ili uwe mtunga sheria lazima uwe na degree na hata wewe kama mwanasheria hujui kigezo cha kikatiba cha mtunga sheria kinasemaje ili apate sifa ya kuwa mtunga sheria. Tuache ushabiki kwenye jema lazima tupongezane .

@DIZEPA

Jamaa kanishangaza sana.
 

Kutukana ni tabia ya wafuasi wa CHADEMA siwezi kushangaa, huko kupambana kwa Mnyika kwenye ESCROW unakokuongelea labda ulikuona wewe mwenyewe lakini jamii inamjua Kafulila ambae CDM waimfukuza na kumwita sisimizi lakini kwa sasa Mbowe amemteua kuwa waziri kivuli
 

Ni kwa sababu watu wanaamua tu kukaa kimya. Lakini ukweli ni kwamba Zitto anasema uongo hadi watu wanaojua wanaogopa. Kusema uongo ili kujikweza ni jambo la aibu sana kufanywa na mtu yeyote anayetaka kuwa kiongozi.
 
Kama ungeweka hapa hizo ripoti za mashirika zinaomtaja Mnyika kama mbunge pekee mwenye mchango mkubwa bungeni ingekuwa vizuri saana. Otherwise wewe ndio unatakiwa kuwa reasonable badala ya kuniambia mimi maana unaongea maneno ya kusikia kwenye vijiwe vya kahawa na magazeti ya udaku!
 
Kuhusu Escrow; Sehemu ya hotuba ya Mnyika, mwaka jana Bunge la Bajeti....

Ufisadi katika akaunti ya Escrow


Mheshimiwa spika, kutokana na mgogoro wa IPTL na TANESCO ilifunguliwa akaunti inayojulikana kwa jina la "Escrow". Akaunti hii ilifunguliwa ili fedha ambazo Tanesco ilipaswa kuilipa IPTL kwa ajili ya Capacity Charge ziwekwe kwenye akaunti hiyo hadi pale mgogoro huo utakapomalizika, kwa mjibu wa taarifa zilizopo akaunti hii ilikuwa na Dola milioni 122 ambazo ni zaidi ya billion 200 pesa ambazo ni zaidi ya zile zilizoko kwenye kashifa nyingine ya EPA ambazo sasa zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa mjibu wa taarifa ya Gavana wa benki kuu ya Tanzania aliyotoa katika kikao cha kamati ya uchumi ya bunge kilichofanyika Bagamoyo, Gavana huyu alikiri kuwa alibanwa na viongozi wa juu kiasi cha kushindwa kufurukuta.

Kwa maneno yake anasema "mnanionea bure, kulikuwa na presha kubwa sana kuhusu fedha hizi…ukweli ni kwamba IPTL inabadilishwa tu rangi na watendaji ni walewale" Ikumbukwe kuwa Tuhuma dhidi ya Gavana wa Benki kuu zinatolewa kwa kuwa hawezi na hana mamlaka ya kuingia Bungeni kujitetea kwa sababu wanajua kuwa fedha ile ilishaliwa na wajanja wachache.


Tayari viongozi waandamizi wa serikali na shirika la umeme nchini kwa nyakati tofauti wameshatoa kauli mbalimbali zenye nia na malengo tofauti pia, serikali kupitia kwa waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa mfano gazeti la mwananchi Tanzania lilikuwa na habari inayosema Muhongo aongeza utata wa mabilioni IPTL .


Katika muendelezo wa kile kinachoonesha kuwa watendaji wa serikali hii ya chama cha mainduzi hawana nia njema na Taifa hili kama ambavyo historian a mazingira ya IPTL yameonesha tangia mwanzo, katika sakata hili pia, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema fedha hizo hazikuwa za Serikali. Waziri amenukuliwa na vyombo vya habari akisema


"Hizo fedha hazikuwa za Serikali, Tanesco ilitakiwa kulipa Capacity Charge (gharama za uwekezaji) kwa IPTL kama inavyolipa karibu Sh27 bilioni kwa kampuni nyingine zinazozalisha umeme,"


Profesa Muhongo alisahau kuwa Tanesco iliyoweka fedha hizo ni shilika la umma na hivyo ni fedha za serikali, pili madhumuni ya fedha hizo hayajafikiwa na Tanesco wenyewe wanasema kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano Tanesco Makao Makuu, kuwa hukumu kati ya Tanesco na IPTL inasema: "Mahakama hiyo (ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji) haikutangaza aliyeshinda wala kushindwa.


"Ilichofanya ni kutoa muda wa miezi mitatu kwa pande zote mbili, (Standard Charted Bank Hong Kong (SCB-HK)) na Tanesco kwenda kukubaliana nje ya Mahakama… kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu taratibu za kukokotoa gharama halisi.


Mheshimiwa spika
, huku nyuma tayari mafisadi wa Taifa hili wameshakwapua fedha hizo, mbaya zaidi hakuna anayekanusha kuhusu kuibiwa kwa fedha hizo isipokuwa mkazo unatiliwa kuliaminisha taifa kuwa fedha hizi hazikuwa za serikali, ni lazima watanzania tukumbuke kuwa viongozi waandamizi wa serikali ya chama cha mapinduzi huwa na kawaida ya kauli hizi pale wanapokuwa wamefanya ufoisadi, kwa mfano katika kasata la kashfa ya rada, mwanasheria wa serikali alisema hakukuwa na mazingira ya rushwa lakini baadaye sote tulishuhudia chenji za rada, pili katika sakata la Richmond sote tulishuhudia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ikikanusha kuwepo kwa mazingira ya rushwa na hivyo TAKUKURU ikashidwa kufanya kazi yake, hali siyo tofauti pia katika sakata hili la bilioni zaidi ya 200.

Mheshimwa spika kambi rasmi ya upinzani bungeni inalitaka bunge hili kuunda tume kuchunguza kashfa hii, kamati hii kwa kuwa itakuwa na uwezo wa kujua mbivu na mbichi dhidi ya sakata hili ambalo inasadikika wezi wa fedha za Escrow wako ndani ya bunge hili tukufu.

Mheshimwa spika maelezo yoyote kuwa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU ifanye uchunguzi haitaungwa mkono na kambi ya upinzani bungeni kutokana na historia ya TAKUKURU kutumika kusafisha sakata la Richmond, kwa upande wingine ofisi ya CAG nayo ilihusika katika kumsafisha sakata la aliyekuwa katibu mkuu Jairo.

Aidha historia inaonesha kuwa magavana wanapokuwa na taarifa kama hizo hupotea katika mazingira ya utatanishi kama ilivyokuwa kwa Balali, kambi rasmi ya upinzani bungeni inatoa angalizo la kutojirudia kwa hali hiyo


 
Mama yako huwa anapenda sana hako kakichwa kengine huwa analia kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…