Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,153
- 892
Jana Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na vyombo vya habari, ametoa wito kwa watanzania kugoma kula lengo likiwa kumuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu. Kuna maswali ambayo yanastahili kuulizwa pale viongozi wa kisiasa wanapotoa wito kwa wananchi kuchukua hatua za kuonyesha mshikamano na viongozi wao. Mojawapo ni hili: Watanzania waliokataa hata kufuga nywele kwa ajili ya kuonyesha mshikamano na Tundu Lissu, leo hii mnawezaje kuwaomba wagome kula kwa ajili yake?
Kugoma kula si sawa na kuvaa alama ya mshikamano. Kutokula kunaweza kuathiri afya, kwa hiyo, wito wa aina hii unahitaji kupuuzwa kwa sababu ni kutaka kuwafanya watanzania wajinga.
Jiulize, leo hii John Mnyika anapotoa wito wa kutaka watanzania wagomee kula, je yeye na familia yake pia watagoma kula? Kuna tofauti kati ya kuunga mkono haki za Tundu Lissu na
kukubaliana na kila mbinu inayopendekezwa katika harakati za kudai haki hizo.
CHADEMA na viongozi wao wasiwafanye watanzania ni watoto wadogo na wajinga wa kufikiri, kwamba sasa maisha yao yaamuliwe na hisia za kisiasa, kwamba fanyeni hiki nao wanafanya, nyakati hizo hazipo tena.
Kama Watanzania hawakuwa tayari hata kufuga nywele kama ishara ya mshikamano na Tundu Lissu, leo wanapoombwa kushiriki mgomo wa kutokula wanawachukuliaje?
Hata Ilipotokea hamasa kwamba watu wafuge nywele kama Tundu Lissu pale CHADEMA viongozi wao wenyewe walikataa, aliyekubali kufuga nywele alikuwa Boni Yai na Sugu lakini haikuchukua hata wiki nao wakazikata.
Sasa leo wanaleta suala la watu wagomee kula, hii ni dhahiri inaonekana wameishiwa hoja na kilichobaki sasa badala ya kufanya siasa wanafanya komedi.