Mnyika hakika wewe ni Mtanzania Mzalendo na Kiongozi wa Kuigwa

UWEZO_WAKO

Member
Nov 17, 2010
39
4
Mnyika ajitolea mshahara wake Send to a friend Sunday, 12 December 2010 21:14 0diggsdigg

Geofrey Nyang’oro
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, ametoa asilimia 40 ya mshahara wake kwa kipindi chote cha ubunge wake kuchangia mfuko wa elimu na kituo cha elimu kinachotarajia kuanzishwa jimboni humo.

Akizungumza kwenye kongomano la lililoandaliwa na Kamati ya Mafunzo ya Elimu ya Juu ya Chadema kutoka vyuo vikuu vya Jiji la Dar es Salaam, Mnyika alisema tayari ameanza kutekeleza ahadi hiyo.
Mnyika alisema ametoa asilimia 20 ya mshahara uliopita na kwamba, lengo ni kutunisha mfuko huo.
Kuhusu ujenzi wa kituo cha elimu, Mnyika aliahadi kutoa asilimia 20 ya posho ya ubunge kila mwezi hadi ujenzi utakapokamilika, mradi huo unalenga kuimarisha elimu kwa watu mbalimbali jimboni humo.

Alisema taratibu za kushughulikia kituo hicho zitaanza na ndani ya miezi mitatau na taarifa itatolewa kwa wananchi.
Mradi huo uliibuliwa jana kwenye kongamano hilo na wawasilisha mada ya elimu waliodai kitasaidi kukutanisha wasomi kutoka maeneo mbalimbali kujadili masuala ya elimu.

Kuhusu utekelezaji wa ahadi zake, Mnyika alisema Januari anatarajia kukutanisha wataalamu mbalimbali, watendaji wa serikali na wanaharakati kujadili kwa pamoja jinsi ya kutatua tatizo la maji.

Mnyika alisema hali hiyo imelenga kutumia wataalamu wa aina zote kuhakiisha utatuzi wa kudumu wa kero ya maji jimboni humo inapatikana.
Kongomano hilo liliwakutanisha wanafunzi na wanaharakati toka asasi mbalimbali ikiwamo ya Haki Ardhi, mada saba ziliwasilishwa na kujadiliwa.
 
Tungekuwa na Wabunge/viongozi wote Kama Mnyika hakika Tanzania Ingebadilika. Zidumu fifkra zako Mh. Mnyika, tunaomba wengine waige mfano wako. Sasa ni zama za kuchangia maendleo ya wananchi, zama za kuwaibia wananchi zimepitwa na wakati. Kwa mtindo huo kura kipindi kijacho tena ni kwako (endapo utagombea?).
 
PINDA NA MNYIKA: MASIKINI WA KIFEDHA, MABILIONEA 'MOYO WA KUJITOLEA':

John Mnyika, kijana Mwenzetu, and Peter Kayanza Pinda Mtoto wa Mkulima tu kama nilivyo mimi hapa, NAWAPENDA SANA TENA SANA!! NanyiRegnald Mengi, na Marehemu Abbas Gulamali, hatujawasau katika hili.

Nionavyo mimi, viongozi wazuri huongoza kwa kuonyesha matendo mema yasioleta maswali mengi katika jamii kama ambavyo mnavyoonyesha. Hakika, kwangu mimi mtu ni UTU na wala si cheo, dini, kisomo, wala nini alichonacho.

Naomba nirudie kwamba awapenda SANA si tu kwa sababu mchango mliotoa hadi sasa bali kikubwa zaidi ni KILE KILICHOWAKUNA MPAKA MKAFIKIA MAAMUZI MAZITO kama hayo ya kujipunguzia mkate wa familia ili Wa-Tanzania wenzenu tusiokua na kitu walau nasi tupate japo ka-tulia. Viongozi wachache watakaogundu siri iliopo nyuma ya 'Moyo wa Kujitole' kamwe kuleta maendeleo kwake hakutokua shida kubwa sana. Hii ni kwa sababu siku ukituomba nasi tukachangi maendeleo yetu fulani wala hautohitaji kuja na bazi wa nyumba kumi wa mwenyekiti wa kijiji wakakamate kuku wangu ndio nipate kufanya hivyo. Nitakua wa kwanza kukukimbilia na japo kidogo nilichonacho ili niwe nami nimetia mguu katika ramani ya maendeleo yetu.

Nanyi vijana wenzangu, bila shaka mtakubaliana nami ya kwamba kama kuna kitu cha thamani kubwa sana ambacho Wa-Tanzania kwa ujumla wetu tumeupoteza mpaka dakika hii, ni MOYO WA KUJITOLEA. Si siri tena ya kwamba hivi sasa ukarimu wa Mtanzania umebakia tu kwenye tabasamu za kinafiki tu. Kwa mantiki hiyo, nanikati yetu hapa angetegemea kuona ule ukarimu wa kihistoria hasa wa Msukuma kule vijijini kwamba siku moja ungegeuka ukatuzalia Gwiji la Ufisadi kutoka katika hilo eneo la watu wenye moyo safi kiasi cha kukutana na FISADI aliekubuhu ambaye kwake rushwa wa hadi Dola milioni moja za Ki-Marekani kwake ni vijisenti tu kwenye akaunti za nchi za nje???

Kwa wadadisi wa mambo, tunasimuliwa kwa miaka ingi sasa kwamba Msukuma, ambaye anadaiwa kuwa ndiye chapa halisi ya ukarimu wa Ki-Tanzania, ukiwatokea majumbani kwao na bahatti tu ukute watu wanakula ni SHARTI KWANZA UKANAWE NA KUJIUNGA MOJA KWA MOJA KWENYE SHUGULI YA KULA PEUPE BARAZANI na kwamba maelezo ya kwamba umetokea wapi na unayo shida gani zote zitasikilizwa tu baadaye. Isitoshe, kwa wanaowafahamu kiundani zaidi kabila hili husemekana siku zote wao huona fahari kubwa sana watu kula makwa na kwamba hata wakiwa ni mke na mume tu lakini ugali utapikwa wa kutosha kabisa ili hata wakitokea wengine watatu ghafla tu wala hawana kazi ya kutenga chungu cha pili. Jamani, hata kiusalama tu hamuoni mgeni asiyefahamika vema ukitangulia kumjulia tumbo lake vizuri ni saa ngapi tena akageuka akakudhuru hata kama mtu alikua amemtuma akafanye hivyo kwako???

Na wengine huongezea kwamba Msukuma usiposhiriki kula kwake hapo ndio uhesabu kukosa kupata wa kukusikiliza hapo baadaye kidogo. Leo hii UFISADI ni ufahari na watu kujigambiana juu ya hili JANGA LA TAIFA. Siku hizi Watanzania tumeanza kula kwenye vyumba vyetu pa kulala na wala si sebuleni wala barazani tena.

Ajabu zaidi, siku hizi mtu anatoka na gari peke ya tangu Tunduma mpaka Namanga bila kubeba hata mtu njia. Hivi kweli hamuoni kwa nini mtu ukipata ajali njiani na wanakijiji cha karibu siku hizi hutokea kuwa ni watu wenye uwezekano mkubwa sasa kukumalizia kabisa uhai wakachukue kidogo ulichonacho hata kama hali yako haikua mbaya sana???

Kama mtu ataona huo ni ushamba leo hii basi NDIO MJUE KWAMBA NDIPO UMOJA WETU WA DHATI NA, UPENDO BILA UNAFIKI NA MOYO WA KUJITOLEA kama taifa ndipo tulipoizikia hiyo lulu.

Na kama hauamini basi ukweli wa mambo nikwamba ni hapo hapo penye kuonekana mshamba ndipo tunakopotezea hazina yetu hiyo na UFISADI kujaza nafasi yake. Hiyo ndio maana siku hizi watu tukaanza kuangaliana kwa jicho la uchoyo na kutokuaminiana tena. Hivyo tukija kuwa wazee nasi wala tusione aibu kuwasimulia watoto wetu jinsi sisi kama taifa maskini duniani tulivyowahi KUJIKUSANYIA HESHMA LUKUKI KWA DHANA TU YA UPENDO NA KUAMINI KWAMBA BINADAMU WOTE DUNIANI NI NDUGU ZETU na kwamba kwa mikono yetu wenyewe tulishiriki kutowesha kabisa hiyo hali nzuri..

Myika, Pinda na sisi vijana, tunafarijika kutambua kwenu ukweli kwamba taifa letu la Tanzania LITAJENGWA NA WENYE MOYO KAMA NYINYI (amba zama zihi ni watu hadimu mno) NA KUZIDI KUTAFUNWA NA WENYE MENO kama akina Rastam Aziz na Edward Lowassa ambao sasa hivi wamezagaa kila pembe ya nchi na idara zote za serika na hata vyombo vya habari, ulinzi na usalama, sawa sawa na magugu shambani!!!

HAKI YA KWELI, BASI TU!!!
 
tofauti ni kuwa pinda yuko tayari kuona mafisadi wakiogelea bila kuguswa wakati mnyuka anawakemea na kutumia kidogo alicho nacho kwa manufaa ya wananchi. Mnyika is an inspiration. Umepata taarifa za Godbless Lema, je za nyerere huko musoma hakika vijana wetu wamejipanga kisawasawa
 
Hongera Mhe. Mnyika. Mimi kama mwanaUbungo, 2nategemea mengi toka kwako kaka. Big U
 
kuna mkuu mmoja hapa jamvini aliwahi kumwambia mnyika anampa kura lakini asivimbishe kitambi, nadhani yule ndugu anafarijika sasa! Big up mnyika
 
Ni mfano mzuri sana kwa kweli. Siyo tu kujitolea kwake sehemu ya mshahara wake, bali tu kwamba ameanza kazi ya kushirikiana na wananchi kujadili na kutatua matatizo yao. Tumezoea wabunge wengi wakishachaguliwa wanatokomea.

Nitoe angalizo wakati tukifurahia hiki kitendo kizuri cha Mnyika kujitolea sehemu ya mshahara wake. Matatizo yako mengi sana katika jimbo lake. Utaratibu wa kujitolea mshahara unaweza kumkosanisha na wananchi ambao hatamudu kuchangia miradi ambayo ni kipaumbele zaidi kwao. Pia mshahara wake ukiisha kutikokana na kuchangia miradi, ataanza kukwepa mialiko ya wananchi. Ina maana kwamba moyo wake huu mzuri wa kujitolea unaweza kumkosanisha na wananchi, pengine kupelekea kutochaguliwa Tena 2015.

Sasa Kama hatachangia matatizo yatatatuliwaje? Aungane na Mdee kupitia mipango rasmi ya manispaa ya kinondoni kwa miaka iliyopita na ijayo (strategic plan). Wapitie mapato na matumizi. Bora wakose vikao vya bunge kuliko vya baraza la madiwani. Kisha wahakikishe kero zote za wananchi zinaingizwa kwenye mipango ya manispaa na kuhamasisha wananchi kusimamia utekelezaji. Hii Ina maana kwamba manispaa ya kinondoni Ina uwezo wa kutatua matatizo yote na mbunge akatumia mshahara wake kujikimu na kusimamia utekelezaji.

Mbunge siyo "strong room" ya jimbo! Tukimtaka kujitolea sana pesa, mafisadi watapitia hapo hapo. Tusijekuwa kama wale wazazi ambao humpenda mtoto asiye na shughuli yoyote rasmi lakini anawasaidia sana wazazi, pesa nyingi. Siku wakisikia mtoto wao kapigwa risasi kwenye tukio la wizi, hudai mtoto wao amelogwa! Kwani mnafikiri ilikuwaje Lowasa na Chenge wakapokelewa kishujaa majimboni mwao baada ya kutuhumiwa ufisadi?
 
nakuhakikishia mh. mnyika siku ukitatua tatizo la maji huku mbezi mshikamano, na ukaweza kumleta said mwema au kova tukajipanga kuhusu ulinzi huku, hutakuwa na haja ya kupunguza mshahara wako, sisi walala hoi, tutabeba mikokoteni na kuchanga mia tano mia tano hadi kero zote ziishe, utaingia kwenye kitabu cha giumness. MAJI YANAPITA KIMARA NA MBEZI TOKA RUVU KWENDA KWA AKINA PATEL KULE MJINI, SIYE TUNABAKI WALINZI WA HAYO MABOMBA YA AKINA PAATEL
 
Ni mfano mzuri sana kwa kweli. Siyo tu kujitolea kwake sehemu ya mshahara wake, bali tu kwamba ameanza kazi ya kushirikiana na wananchi kujadili na kutatua matatizo yao. Tumezoea wabunge wengi wakishachaguliwa wanatokomea.

Nitoe angalizo wakati tukifurahia hiki kitendo kizuri cha Mnyika kujitolea sehemu ya mshahara wake. Matatizo yako mengi sana katika jimbo lake. Utaratibu wa kujitolea mshahara unaweza kumkosanisha na wananchi ambao hatamudu kuchangia miradi ambayo ni kipaumbele zaidi kwao. Pia mshahara wake ukiisha kutikokana na kuchangia miradi, ataanza kukwepa mialiko ya wananchi. Ina maana kwamba moyo wake huu mzuri wa kujitolea unaweza kumkosanisha na wananchi, pengine kupelekea kutochaguliwa Tena 2015.

Sasa Kama hatachangia matatizo yatatatuliwaje? Aungane na Mdee kupitia mipango rasmi ya manispaa ya kinondoni kwa miaka iliyopita na ijayo (strategic plan). Wapitie mapato na matumizi. Bora wakose vikao vya bunge kuliko vya baraza la madiwani. Kisha wahakikishe kero zote za wananchi zinaingizwa kwenye mipango ya manispaa na kuhamasisha wananchi kusimamia utekelezaji. Hii Ina maana kwamba manispaa ya kinondoni Ina uwezo wa kutatua matatizo yote na mbunge akatumia mshahara wake kujikimu na kusimamia utekelezaji.

Mbunge siyo "strong room" ya jimbo! Tukimtaka kujitolea sana pesa, mafisadi watapitia hapo hapo. Tusijekuwa kama wale wazazi ambao humpenda mtoto asiye na shughuli yoyote rasmi lakini anawasaidia sana wazazi, pesa nyingi. Siku wakisikia mtoto wao kapigwa risasi kwenye tukio la wizi, hudai mtoto wao amelogwa!

Gurudumu uyasemayo ni kweli kweli kabisa lakini Mbunge pia kujitolea asilimia fulani ya mshahara wake ni MUHIMU ili kuonyesha kujali kwake mambo ya maendeleo vinginevyo kazi itakuwa ngumu sana kwani ujue hata wananchi wengine tutakaombwa kuchangia miradi pia tutato fedha kwenye mishahara/vimiradi vyetu ambazo hata sisi tunazitegemea kujikimu. Ninakubaliana nawe wasimamie vyema yale mapato mengine na vyanzo mbali mbali vya mapato za halmashauri zao. Wabunge wengine waonyesha moyo huo pia wa kuchangia sio kutuhamasisha tu sisi wananchi kila mtu na viongozi waonyeshe mfano. Hongera Mh. Myika
 
Safi sana Mh. Mnyika na ningekuwa VC wa UDSM Ningekupa PHD ya ukweli. Hivi Malechela, Mramba na wengineo wangekuwa wanatoa asilimia 20 ya Mishahara yao toka walipoanza kuwa wabunge na mawaziri leo wananchi wao wangekuwa na shida kubwa kweli?
 
Ni mfano mzuri sana kwa kweli. Siyo tu kujitolea kwake sehemu ya mshahara wake, bali tu kwamba ameanza kazi ya kushirikiana na wananchi kujadili na kutatua matatizo yao. Tumezoea wabunge wengi wakishachaguliwa wanatokomea.

Nitoe angalizo wakati tukifurahia hiki kitendo kizuri cha Mnyika kujitolea sehemu ya mshahara wake. Matatizo yako mengi sana katika jimbo lake. Utaratibu wa kujitolea mshahara unaweza kumkosanisha na wananchi ambao hatamudu kuchangia miradi ambayo ni kipaumbele zaidi kwao. Pia mshahara wake ukiisha kutikokana na kuchangia miradi, ataanza kukwepa mialiko ya wananchi. Ina maana kwamba moyo wake huu mzuri wa kujitolea unaweza kumkosanisha na wananchi, pengine kupelekea kutochaguliwa Tena 2015.

Sasa Kama hatachangia matatizo yatatatuliwaje? Aungane na Mdee kupitia mipango rasmi ya manispaa ya kinondoni kwa miaka iliyopita na ijayo (strategic plan). Wapitie mapato na matumizi. Bora wakose vikao vya bunge kuliko vya baraza la madiwani. Kisha wahakikishe kero zote za wananchi zinaingizwa kwenye mipango ya manispaa na kuhamasisha wananchi kusimamia utekelezaji. Hii Ina maana kwamba manispaa ya kinondoni Ina uwezo wa kutatua matatizo yote na mbunge akatumia mshahara wake kujikimu na kusimamia utekelezaji.

Mbunge siyo "strong room" ya jimbo! Tukimtaka kujitolea sana pesa, mafisadi watapitia hapo hapo. Tusijekuwa kama wale wazazi ambao humpenda mtoto asiye na shughuli yoyote rasmi lakini anawasaidia sana wazazi, pesa nyingi. Siku wakisikia mtoto wao kapigwa risasi kwenye tukio la wizi, hudai mtoto wao amelogwa! Kwani mnafikiri ilikuwaje Lowasa na Chenge wakapokelewa kishujaa majimboni mwao baada ya kutuhumiwa ufisadi?

Nugu Gurudumu ninaungana nawe katika hilo angalizo lizingatiwe, lakini pia naamini Mh yuko smart kwani mchango wa kutoa asilimia fulani ya mshahara huwa hasa inalenga mradi ambao unagusa watu wote ambacho ndichoamakifanya Mnyika kwani amechangia elimu ambao mradi huo tayari ni mchango wake kwa wananchi wote wa jimboni kwake na tanzania nzima kwa muda wa miaka 5. Hii ina maana yeye kila siku kwa muda wa miaka 5 yeye anachangia kwani kila mwezi atakuwa anatoa hiyo asilimia. Sasa yeye anahaki sasa ya kufanya kazi ya kuwahamasisha watu wengine kuchangia na pia ameongeza uwezo wake wa kukemea ufisadi na hii itampa uchungu endapo atatokea mtu wa kuhujumu miradi, naamini hata wabadhirifu hawatajaribu kwani Mbunge mwenyewe amejitolea sana na kujinyima. Sasa sisi tunaojua kuwa kutoa pia kunazingatia uwezo tusaidie kuwaelimisha wale ambao watakao kuwa na mawazo Mbunge ana hela za kutoa kila mradi. Kwa hili sasa alilolifanya Mheshimiwa Mnyika ni ujumbe tosha kwa mafisadi wanaohujumu mapato na miradi ya halmashauri. Sasa ni zamu yetu na wengine katika jimbo (na hata inje ya jimbo) kuchangia na sisi kutoka katika miradi/mishahara yetu. Kwa mwendo huu unaanza kuwaona watu watakao kuwa mawaziri kwa serikali itakayoongozwa na CDM 2015
 
Safi sana,kweli jamaa amejipanga vizuri kuhakikisha jimbo hilo halipotezi!!
 
Ubungo ni jimbo lenye kipato ukilinganisha na majimbo mengi ya TANZANIA. 20% ya mshahara wa mbunge its just a drop in an ocean kwa ubungo. Sidhani kama wananchi wanatakiwa kulala na kutosimamia mapato yao kwa ajili ya maendeleo na kusubiri 20% ya Mnyika. This is another cheap politics ambayo in a liberal economy and competitive one leo huwezi kuwanyanyua watu kwa namna hiyo. Ni njia njema ya kusaidia but not noly the best way. Kazi ya mbunge ni zaidi ya kutoa fedha, ni zaidi ya kuzungumza bungeni, ni zaidi ya kutazama halmashauri zikijikongoja na ni zaidi ya kuimba na kucheza ngoma wapendazo wananchi
 
Back
Top Bottom