Mnyika hakika wewe ni Mtanzania Mzalendo na Kiongozi wa Kuigwa

huyu dogo mimi nilijua nalamba dume kwa kumpa kura yangu ili awe mbunge wangu,,,,,,,atawashangaza wengi ambao walikuwa hawamfahamu kabla... kwa ujumla ni kiongozi kwa vigezo vyote na taratiiiiiiiiiiiiibu anajijengea himaya ya kutawala jimbo la ubungo milele. Nawashauri tume ya uchaguzi kuligawanya jimbo la ubungo kama wanataka mgombea wa CCM katika jimbo hilo
 
Hakika Mnyika ni chachu ya kweli katika kuleta mabadiliko hapo Ubungo. Endelea ivyo ivyo mkubwa. Na pia wanaUbungo muungeni mkono kamanda huyo kwa michango ya hali na mali.
 
nia njema.
But kuna konokono wanajipanga kuzuia maendeleo yote yaliyoahidiwa na Mnyika kwa kipindi hiki cha miaka mitano.

Hawa ni watu wa CCM ambao tuliwasikia wakipita mitaani huku wakilopoka maneno hayo na kuonyesha kuwadharau waliomchagua na kuwatisha kuwa watakiona cha moto coz hawatanufaika na misaada au huduma toka Serikalini kwa kuwa tu wamemchagua Mnyika.

Mimi naona hayo ni mawazo mgando...go ON Mnyika, GO.

Wao wanaotuambia hatutapata maendeleo kisa tumekuchagua wewe, tuliwauliza wao walituletea maendeleo gani kwa miaka 48?
Tangu enzi ya Halfan Mng'ago, Ading'oka, Ngula, mpk Keenja je wametuletea maendeleo gani?

Hawakujibu.
matokeo yake wakatujibu ''sawa tutaona''....
Sasa sisi tuko na wewe Mkulungwa jipange ili uweze kutufikisha nchi ya kanani.
 
PINDA NA MNYIKA: MASIKINI WA KIFEDHA, MABILIONEA 'MOYO WA KUJITOLEA':

John Mnyika, kijana Mwenzetu, and Peter Kayanza Pinda Mtoto wa Mkulima tu kama nilivyo mimi hapa, NAWAPENDA SANA TENA SANA!! NanyiRegnald Mengi, na Marehemu Abbas Gulamali, hatujawasau katika hili.

Nionavyo mimi, viongozi wazuri huongoza kwa kuonyesha matendo mema yasioleta maswali mengi katika jamii kama ambavyo mnavyoonyesha. Hakika, kwangu mimi mtu ni UTU na wala si cheo, dini, kisomo, wala nini alichonacho.

Naomba nirudie kwamba awapenda SANA si tu kwa sababu mchango mliotoa hadi sasa bali kikubwa zaidi ni KILE KILICHOWAKUNA MPAKA MKAFIKIA MAAMUZI MAZITO kama hayo ya kujipunguzia mkate wa familia ili Wa-Tanzania wenzenu tusiokua na kitu walau nasi tupate japo ka-tulia. Viongozi wachache watakaogundu siri iliopo nyuma ya 'Moyo wa Kujitole' kamwe kuleta maendeleo kwake hakutokua shida kubwa sana. Hii ni kwa sababu siku ukituomba nasi tukachangi maendeleo yetu fulani wala hautohitaji kuja na bazi wa nyumba kumi wa mwenyekiti wa kijiji wakakamate kuku wangu ndio nipate kufanya hivyo. Nitakua wa kwanza kukukimbilia na japo kidogo nilichonacho ili niwe nami nimetia mguu katika ramani ya maendeleo yetu.

Nanyi vijana wenzangu, bila shaka mtakubaliana nami ya kwamba kama kuna kitu cha thamani kubwa sana ambacho Wa-Tanzania kwa ujumla wetu tumeupoteza mpaka dakika hii, ni MOYO WA KUJITOLEA. Si siri tena ya kwamba hivi sasa ukarimu wa Mtanzania umebakia tu kwenye tabasamu za kinafiki tu. Kwa mantiki hiyo, nanikati yetu hapa angetegemea kuona ule ukarimu wa kihistoria hasa wa Msukuma kule vijijini kwamba siku moja ungegeuka ukatuzalia Gwiji la Ufisadi kutoka katika hilo eneo la watu wenye moyo safi kiasi cha kukutana na FISADI aliekubuhu ambaye kwake rushwa wa hadi Dola milioni moja za Ki-Marekani kwake ni vijisenti tu kwenye akaunti za nchi za nje???

Kwa wadadisi wa mambo, tunasimuliwa kwa miaka ingi sasa kwamba Msukuma, ambaye anadaiwa kuwa ndiye chapa halisi ya ukarimu wa Ki-Tanzania, ukiwatokea majumbani kwao na bahatti tu ukute watu wanakula ni SHARTI KWANZA UKANAWE NA KUJIUNGA MOJA KWA MOJA KWENYE SHUGULI YA KULA PEUPE BARAZANI na kwamba maelezo ya kwamba umetokea wapi na unayo shida gani zote zitasikilizwa tu baadaye. Isitoshe, kwa wanaowafahamu kiundani zaidi kabila hili husemekana siku zote wao huona fahari kubwa sana watu kula makwa na kwamba hata wakiwa ni mke na mume tu lakini ugali utapikwa wa kutosha kabisa ili hata wakitokea wengine watatu ghafla tu wala hawana kazi ya kutenga chungu cha pili. Jamani, hata kiusalama tu hamuoni mgeni asiyefahamika vema ukitangulia kumjulia tumbo lake vizuri ni saa ngapi tena akageuka akakudhuru hata kama mtu alikua amemtuma akafanye hivyo kwako???

Na wengine huongezea kwamba Msukuma usiposhiriki kula kwake hapo ndio uhesabu kukosa kupata wa kukusikiliza hapo baadaye kidogo. Leo hii UFISADI ni ufahari na watu kujigambiana juu ya hili JANGA LA TAIFA. Siku hizi Watanzania tumeanza kula kwenye vyumba vyetu pa kulala na wala si sebuleni wala barazani tena.

Ajabu zaidi, siku hizi mtu anatoka na gari peke ya tangu Tunduma mpaka Namanga bila kubeba hata mtu njia. Hivi kweli hamuoni kwa nini mtu ukipata ajali njiani na wanakijiji cha karibu siku hizi hutokea kuwa ni watu wenye uwezekano mkubwa sasa kukumalizia kabisa uhai wakachukue kidogo ulichonacho hata kama hali yako haikua mbaya sana???

Kama mtu ataona huo ni ushamba leo hii basi NDIO MJUE KWAMBA NDIPO UMOJA WETU WA DHATI NA, UPENDO BILA UNAFIKI NA MOYO WA KUJITOLEA kama taifa ndipo tulipoizikia hiyo lulu.

Na kama hauamini basi ukweli wa mambo nikwamba ni hapo hapo penye kuonekana mshamba ndipo tunakopotezea hazina yetu hiyo na UFISADI kujaza nafasi yake. Hiyo ndio maana siku hizi watu tukaanza kuangaliana kwa jicho la uchoyo na kutokuaminiana tena. Hivyo tukija kuwa wazee nasi wala tusione aibu kuwasimulia watoto wetu jinsi sisi kama taifa maskini duniani tulivyowahi KUJIKUSANYIA HESHMA LUKUKI KWA DHANA TU YA UPENDO NA KUAMINI KWAMBA BINADAMU WOTE DUNIANI NI NDUGU ZETU na kwamba kwa mikono yetu wenyewe tulishiriki kutowesha kabisa hiyo hali nzuri..

Myika, Pinda na sisi vijana, tunafarijika kutambua kwenu ukweli kwamba taifa letu la Tanzania LITAJENGWA NA WENYE MOYO KAMA NYINYI (amba zama zihi ni watu hadimu mno) NA KUZIDI KUTAFUNWA NA WENYE MENO kama akina Rastam Aziz na Edward Lowassa ambao sasa hivi wamezagaa kila pembe ya nchi na idara zote za serika na hata vyombo vya habari, ulinzi na usalama, sawa sawa na magugu shambani!!!

HAKI YA KWELI, BASI TU!!!
Pinda muondoe kwenye orodha hiyo please. Hatuhitaji kuwapa sifa viongozi ambao ni nusu mzungu na nusu mwafrika.
 
huyu dogo mimi nilijua nalamba dume kwa kumpa kura yangu ili awe mbunge wangu,,,,,,,atawashangaza wengi ambao walikuwa hawamfahamu kabla... kwa ujumla ni kiongozi kwa vigezo vyote na taratiiiiiiiiiiiiibu anajijengea himaya ya kutawala jimbo la ubungo milele. Nawashauri tume ya uchaguzi kuligawanya jimbo la ubungo kama wanataka mgombea wa CCM katika jimbo hilo

wakigawa jimbo, uswahilini apewe mswahili swahili design hivi, huku juu tubaki na Mnyika wetu
 
hii ni chachu kwa wabunge wengine kuweza kuhamasisha wananchi wao kuondokana na utegemezi na kujiletea maendeleo yao wenyewe kwa faida yao na vizazi vyao.
Kuna mjumbe mmoja amesema ubunge ni zaidi ya kuongea bungeni,kutoa mshahara wake nk. Lakini muhimu ni mbunge kweza kuwahamasisha wananchi wake kujitambua na kujiletea maenndeleo wanayo yahitaji.
Mwanzo mzuri mh. Mnyika endelea kuibua mikakati.mimi nasema endelea kuibua vipaji.
 
Nashukuru, lakini hukuniahidi mgao wa mshahara wako, kama mpiga kura.

Mwisho wa siku tutaulizana ulichoahidi kwa Ubungo.

Kwa hiyo, kumbuka, mkataba wetu uko pale pale.
 
Gurudumu uyasemayo ni kweli kweli kabisa lakini Mbunge pia kujitolea asilimia fulani ya mshahara wake ni MUHIMU ili kuonyesha kujali kwake mambo ya maendeleo vinginevyo kazi itakuwa ngumu sana kwani ujue hata wananchi wengine tutakaombwa kuchangia miradi pia tutato fedha kwenye mishahara/vimiradi vyetu ambazo hata sisi tunazitegemea kujikimu. Ninakubaliana nawe wasimamie vyema yale mapato mengine na vyanzo mbali mbali vya mapato za halmashauri zao. Wabunge wengine waonyesha moyo huo pia wa kuchangia sio kutuhamasisha tu sisi wananchi kila mtu na viongozi waonyeshe mfano. Hongera Mh. Myika



Nugu Gurudumu ninaungana nawe katika hilo angalizo lizingatiwe, lakini pia naamini Mh yuko smart kwani mchango wa kutoa asilimia fulani ya mshahara huwa hasa inalenga mradi ambao unagusa watu wote ambacho ndichoamakifanya Mnyika kwani amechangia elimu ambao mradi huo tayari ni mchango wake kwa wananchi wote wa jimboni kwake na tanzania nzima kwa muda wa miaka 5. Hii ina maana yeye kila siku kwa muda wa miaka 5 yeye anachangia kwani kila mwezi atakuwa anatoa hiyo asilimia. Sasa yeye anahaki sasa ya kufanya kazi ya kuwahamasisha watu wengine kuchangia na pia ameongeza uwezo wake wa kukemea ufisadi na hii itampa uchungu endapo atatokea mtu wa kuhujumu miradi, naamini hata wabadhirifu hawatajaribu kwani Mbunge mwenyewe amejitolea sana na kujinyima. Sasa sisi tunaojua kuwa kutoa pia kunazingatia uwezo tusaidie kuwaelimisha wale ambao watakao kuwa na mawazo Mbunge ana hela za kutoa kila mradi. Kwa hili sasa alilolifanya Mheshimiwa Mnyika ni ujumbe tosha kwa mafisadi wanaohujumu mapato na miradi ya halmashauri. Sasa ni zamu yetu na wengine katika jimbo (na hata inje ya jimbo) kuchangia na sisi kutoka katika miradi/mishahara yetu. Kwa mwendo huu unaanza kuwaona watu watakao kuwa mawaziri kwa serikali itakayoongozwa na CDM 2015

Hivi majukumu ya Mbunge kwa mujibu wa Katiba ni nini? Sipingi moyo wa kujitolea wa Mnyika. Nachokonoa jambo la msingi kabisa ambalo watanzania tumekataa kulifuatilia. Je, mbunge akiacha rasilimali zetu zinafujwa na pengine yeye mwenyewe akashiriki kufuja halafu akatusaidia hela kidogo kwenye mradi fulani, huyu mbunge ndiye anayetufaa? Hoja yangu ni kwamba mapato ya Manispaa ya Kinondoni pamoja na yale yanayotoka serikali kuu kama ruzuku ni makubwa mno kuwepo matatizo ya elimu, maji na afya katika manispaa hii. Tumwache Mnyika atumie mshahara wake kujikimu na kujiwezesha kufuatilia hizo pesa zetu. Na sisi turidhike na jinsi alivyotuhabarisha kuhusu mapato yetu na namna alivyotushirikisha kuyasimamia kutatua matatizo yetu. Tusishabikie vizawadi kidogo kutoka kwa mbunge, tabia ambayo ndiyo iliyowafanya wabunge wa ccm kuifikisha hii nchi hapa ilipo. Ni tabia hii ndiyo inayotuelekeza nani ni kiongozi mzuri wakati wa uchaguzi. Ni yule anayetoa vizawadi visivyo na mantiki kisha kuingia madarakani kupora rasilimali zetu zote katika ngazi ya taifa na halmashauri.

Tujadili hiyo dhana tafadhali, na madhara yake katika maendeleo yetu. Tujadili majukumu ya Mbunge siyo moyo wake wa kujitolea. Tusibobee kushabikia anavyojitolea tukasahau kumtuma atuletee taarifa za mapato na matumizi ya manispaa na ushiriki wetu katika mipango. Tukiendelea kushabikia vijizawadi, Chadema itageuka kama ccm kututupia vifulana wakati wa uchaguzi ili tupige kura, na wabunge wa Chadema watakuwa hawana tofauti na wale wa CCM.
 
Ubungo ni jimbo lenye kipato ukilinganisha na majimbo mengi ya TANZANIA. 20% ya mshahara wa mbunge its just a drop in an ocean kwa ubungo. Sidhani kama wananchi wanatakiwa kulala na kutosimamia mapato yao kwa ajili ya maendeleo na kusubiri 20% ya Mnyika. This is another cheap politics ambayo in a liberal economy and competitive one leo huwezi kuwanyanyua watu kwa namna hiyo. Ni njia njema ya kusaidia but not noly the best way. Kazi ya mbunge ni zaidi ya kutoa fedha, ni zaidi ya kuzungumza bungeni, ni zaidi ya kutazama halmashauri zikijikongoja na ni zaidi ya kuimba na kucheza ngoma wapendazo wananchi

Unapoongea toa na mifano, Mnyika ni msikivu hapa ameshaona post yako lakini hajaelewa unataka kumwambia nini, dema sasa afanye nini zaidi au ndio nyie msiojua kupongeza kwa lolote?
 
Nimikukubali Mnyika kwa moyo wa kujitolea. Na hasa kwa kuwa kujitolea huku ni kwa kuibua miradi mipya. Ni kama vile umeonyesha njia na wengine wafuate.
Lakini bado sikubaliani na huu utaratibu wa wabunge kuwa wafadhili maana kazi yao ni zaidi ya hiyo. Unatakiwa kuwa mfuatiliaji na usimamizi mzuri wa resources za manispaa na kuahakikisha zinatumiwa kama zilivyopangwa na kuwa muibuaji wa miradi mipya ya maendeleo ya manispaa ya jiji. Hapo utakuwa umecheza ngoma nzuri.
 
Nashukuru, lakini hukuniahidi mgao wa mshahara wako, kama mpiga kura.

Mwisho wa siku tutaulizana ulichoahidi kwa Ubungo.

Kwa hiyo, kumbuka, mkataba wetu uko pale pale.

Taso, Naweza kusema kuwa Mnyika si tu kama Mbunge, bali pia kama mkaazi wa jimbo la Ubungo (si kama Keenja aliyekuwa anaishi viktoria kinondoni) ametoa 20% ya kipato chake kuanzisha na kuendeleza kituo cha elimu, mimi na wewe pia tunapaswa kuchangia kidogo tulicho nacho kwa ajili ya maendeleo ya Ubungo.
 
Taso, Naweza kusema kuwa Mnyika si tu kama Mbunge, bali pia kama mkaazi wa jimbo la Ubungo (si kama Keenja aliyekuwa anaishi viktoria kinondoni) ametoa 20% ya kipato chake kuanzisha na kuendeleza kituo cha elimu, mimi na wewe pia tunapaswa kuchangia kidogo tulicho nacho kwa ajili ya maendeleo ya Ubungo.
Ni kweli, lakini maendeleo hayaletwi kwa hela na mali. Zaire ya Mobutu ilikuwa na mali kama au kuliko South Afrika lakini bado ni dampo la umaskini.

Nataka kusikia Mnyika ameanza kufanyia kazi, kutekeleza, ahadi zilizofanya apewe kura, zaidi ya kutumwagia mahela yake.
 
Ni kweli, lakini maendeleo hayaletwi kwa hela na mali. Zaire ya Mobutu ilikuwa na mali kama au kuliko South Afrika lakini bado ni dampo la umaskini.

Nataka kusikia Mnyika ameanza kufanyia kazi, kutekeleza, ahadi zilizofanya apewe kura, zaidi ya kutumwagia mahela yake.

amekumwagia pesa au ameahidi/kutoa pesa kwa ajili ya kutekeleza mojawapo ya ahadi zake wakati wa kampeni? Hivi unadhani kuna ahadi itatekelezeka bila pesa?
 
Kila kitu kina nafasi yake! Mi naona Mnyika hapa anataka kupalilia culture ya kujitolea! Kama Watanzania tungekuwa tunachangia kwenye maendeleo badala ya HARUSI aisee tungekuwa mbali!
 
Hivi majukumu ya Mbunge kwa mujibu wa Katiba ni nini? Sipingi moyo wa kujitolea wa Mnyika. Nachokonoa jambo la msingi kabisa ambalo watanzania tumekataa kulifuatilia. Je, mbunge akiacha rasilimali zetu zinafujwa na pengine yeye mwenyewe akashiriki kufuja halafu akatusaidia hela kidogo kwenye mradi fulani, huyu mbunge ndiye anayetufaa? Hoja yangu ni kwamba mapato ya Manispaa ya Kinondoni pamoja na yale yanayotoka serikali kuu kama ruzuku ni makubwa mno kuwepo matatizo ya elimu, maji na afya katika manispaa hii. Tumwache Mnyika atumie mshahara wake kujikimu na kujiwezesha kufuatilia hizo pesa zetu. Na sisi turidhike na jinsi alivyotuhabarisha kuhusu mapato yetu na namna alivyotushirikisha kuyasimamia kutatua matatizo yetu. Tusishabikie vizawadi kidogo kutoka kwa mbunge, tabia ambayo ndiyo iliyowafanya wabunge wa ccm kuifikisha hii nchi hapa ilipo. Ni tabia hii ndiyo inayotuelekeza nani ni kiongozi mzuri wakati wa uchaguzi. Ni yule anayetoa vizawadi visivyo na mantiki kisha kuingia madarakani kupora rasilimali zetu zote katika ngazi ya taifa na halmashauri.

Tujadili hiyo dhana tafadhali, na madhara yake katika maendeleo yetu. Tujadili majukumu ya Mbunge siyo moyo wake wa kujitolea. Tusibobee kushabikia anavyojitolea tukasahau kumtuma atuletee taarifa za mapato na matumizi ya manispaa na ushiriki wetu katika mipango. Tukiendelea kushabikia vijizawadi, Chadema itageuka kama ccm kututupia vifulana wakati wa uchaguzi ili tupige kura, na wabunge wa Chadema watakuwa hawana tofauti na wale wa CCM.

Alichokifanya Mh. Mnyika kwa maneno mengine ni KUWEKA JIWE LA MSINGI ili wadau wengine nao waendelee, ukitaka kwa namna nyingine Mbunge ni Facilitator. Wala hili sio jambo geni kwa viongozi makini. Mandela akiwa Rais alitoa moja ya tatu (asilimia 33.3) ya mshahara wa kila mwezi kwa muda wa miaka 5 kwa ajili ya kuanzisha kile kilichokuja kuitwa "The Nelson Mandela Children's Fund". Kwa hiyo alipotoa ahadi yake hiyo kazi haikukamilishwa na Mandela watu wengine walihamasika na kukamilisha maono aliyokuwa nayo. Wakati mwingine ni ngumu sana kuhamasisha wengine bila kutoa mfano. Kazi za Mbunge tunazifahamu pamoja na yote anayopaswa kuyafanya ni pamoja na hilo alilofikiri kufanya. Kwa upande wa Nyerere shuhuda mmoja anaripoti kama ifuatavyo "The period of campaigning for independence was a very difficult time for Julius and Maria. Julius refused to take any salary from TANU. He said that the party needed all its funds to gain independence. At the same time Oscar Kambona took a salary to support himself and his family. Maria opened a small duka ("shop") to sell soap, sugar, salt, cooking oil etc. in their small home in Dar es Salaam to earn a little money to support the family. She also had a heavy burden of cooking for the many African visitors that came to visit Julius. It is the custom to cook a meal for all visitors. In his position as President of TANU he received many visitors every day. Julius one day told me that any other woman other than Maria would have left him long ago, but Maria stayed during this very difficult time" kiongozi bora ni kama rafiki wa kweli ni vigumu kumpata, haiwezekani kumuacha na kamwe hasahauliki.
Naona watu wanauliza kazi za Mbunge, tuliwahi kufanya utafiti hapa nchini ngoja nidonoe kakipande kadogo kutoka kwenye ripoti yetu.
In practice not all people clearly understand the role of legislators. Through research it emerged that some people in rural areas and even urban areas think that MPs are supposed to personally implement development projects such as road construction, bridges, constructing water projects and establishment of irrigation schemes. This observation underlies the common problem in rural areas where the electorate is tricked into voting for MPs who promise to implement certain projects that are not within their powers to implement resulting in empty promises. Instead the implementation might be the responsibility of local authorities, government agencies or development support agencies while the legislator might only have the power to inquire about progress on the projects or simply facilitate the implementation of projects that benefit their people.
Legislative representation simply put entails the duty of Members of Parliament in servicing and taking care of the interests of their constituencies either in the House of Parliament, at government level or at public forums or wherever the legislator can advance the aspirations and needs of his/her people. It is understood as a reflection of the views, values and principles of constituencies by elected or appointed individuals. The elected individuals are mandated by the people to relay their interests and values to the government.
The main function of legislators is to make laws, representing constituencies and acting as a constraint on executive power by exercising a degree of oversight. Furthermore, they have a control function which entails the control of how national resources are allocated and used.
Therefore, the role of the legislator demands active engagements with the constituency in order to guage its interests, expectations and problems and articulate them in parliament, thus transforming people's views into law. The expectation of every constituency is that their elected Member of Parliament would represent, consult, play an oversight role and make laws that fulfill their specific interests. In effect he/she is expected to convince other MPs and the government that the interests and values of his/her constituency are of
paramount importance and should be given national attention and priority. These values or interests can be economic, social, political or environmental.
 
Back
Top Bottom