Mnyika atangaza maandamano tarehe 16 Machi

Mnyika atangaza maandamano tarehe 16 Machi

We majebere mkerewe nini! maana wakerewe nasikia ndio hawaelewagi mambo yanavyoenda, hivi vita vinatuhusu, hivi vita sio vya mnyika wala magufuli hivi vita ni vyangu mimi na wewe. hivi watu wengine mkojeee! Yaani mpaka kwenye kalenda mna andikiwa kuwa mtajikomboa wenyewe ili ukitizama kalenda ukumbuke kuwa unakubarua cha kujikomboa lakini bado unasubiri mnyika akukomboe

anyway,mie nadhani tuishukuru serikali hii dhalimu kwa kutufundisha somo kubwa sana ambalo watz hatukuwa nalo.somo hili litatusaidia sana hata kwa vizazi vingi vijavyo vitajifunza kutoka kwetu ya kuwa HAKI INADAIWA,HAITOKI BURE!Hivyo kuitwa RAIA ni cheo chenye majukumu mazito sana kuhakikisha haki yako na ya jirani yako zinalindwa kwa gharama yoyote ile.
 
Nani aliwaambIan mkakae sehemu hazijapimwa? Halafu unataka tukuletee maji huko ulikojichimbia...chimba kisima chako usitusumbue.
 
anyway,mie nadhani tuishukuru serikali hii dhalimu kwa kutufundisha somo kubwa sana ambalo watz hatukuwa nalo.somo hili litatusaidia sana hata kwa vizazi vingi vijavyo vitajifunza kutoka kwetu ya kuwa HAKI INADAIWA,HAITOKI BURE!Hivyo kuitwa RAIA ni cheo chenye majukumu mazito sana kuhakikisha haki yako na ya jirani yako zinalindwa kwa gharama yoyote ile.

MAKOFI MATATU KWA JUVEEEEE?

Na asiyekuwa na cha kuchangia abonyeze like tu hapo kwa juve kuliko kuwakatisha tamaa watu wanaotupigania
 
jeshi limejipanga vizuri kudhibiti hayo maandamano! hivyo muandae na uji wa kuletewa hospitali!
Pumbavu kabisa wanaacha kutumia jeshi kudhibiti makanisa yanayochomwa na mauaji ya mapadri wanaagiza FBI kwa mamilioni ya fedha halafu jeshi linatumika kupambana na raia anaepigania maji ya kuoga pumbavu.
 
ulikuwa ukipata ngapi kwenye somo la Civics sekondari?unaonekana hujui kazi za mbunge na wala hujui wajibu wa mwananchi.raia wa aina yenu mnaosubiri viongozi wawafanyie kila kitu ndio mnaosababisha ufisadi uendelee kutafuna nchi hii!uongozi unatoka chini kwenda juu na sio juu kwenda chini!wabongo bwana!wanajua kulalamika tuu na kwenda kwenye semina!
Wakati anatoa ahadi ya kuleta maji alifikiri yeye azam,kabla yakuniambia mimi juu la somo la civics waulize hao wanaosema watatatua matatizo yetu kama walielewa hilo somo
 
  • Thanks
Reactions: SQL
We majebere mkerewe nini! maana wakerewe nasikia ndio hawaelewagi mambo yanavyoenda, hivi vita vinatuhusu, hivi vita sio vya mnyika wala magufuli hivi vita ni vyangu mimi na wewe. hivi watu wengine mkojeee! Yaani mpaka kwenye kalenda mna andikiwa kuwa mtajikomboa wenyewe ili ukitizama kalenda ukumbuke kuwa unakubarua cha kujikomboa lakini bado unasubiri mnyika akukomboe
Sisi tunayajua matatizo yetu lakini anajitokeza kihere here mmoja na kusema atamaliza kero zetu sasa wewe unategemea wananchi wa ubungo walimpeleka huko bungeni kutembeza uzuri?amesema nichagueni mimi niwatatulie matatizo yenu tena na kusisitiza swala la maji ndio la kwanza. Sasa yuko wapi?
 
  • Thanks
Reactions: SQL
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?
Yaani wewe akili yako haina tofauti na w.Maghembe na Kawambwa...
 
Kamanda Mnyika big up kwa harakati zako. Dawa ya moto ni moto, tutakua nawe bega kwa bega kila hatua.. You deserve nobel prize for your efforts!
 
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?

mtajibeba safari hii kama mlizoea longolongo sasa bhasiiiiiiiiiiii...............we need delivarables not blah blah!mnyika anafanya kazi nzuri.
 
Tuko pamoja maana bila shuruti haya magamba kusikia hoja za wananchi ni ngumu,Tutapambana mpaka kieleweke!

Mkuu....kama sijamuelewa Mh. Mnyika utanisahihisha...mie nadhani ni maandamano ya wanajimbo wenye shida ya maji dhidi watendaji wabovu wenye mamlaka ya kutupatia maji....na si dhidi ya "Magamba".....ikiwa hivyo hadithi itakuwa ndefu sana....
 
Hakuna sababu ya maandamano; umefika wakati wananchi wa Ubungo wakiongozwa na Mbunge wao wakae chini na kuanzisha taasisi nje ya ile ya serikali kushughulikia tatizo la maji. Hapa inahitajika ubunifu na uongozi. Je wananchi wanaweza kujiletea maji safi karibu na kwenye majumba yao bila ya serikali? Jibu langu ni "ndiyo". Swali je jinsi gani hili linaweza kufanywa? Hapa inabidi kukaa chini na kufikiria ni jinsi gani "nguvu ya umma" inaweza kugeuzwa na kuwa mtaji wa umma kujileta maji.

Sample Concept Paper
UBUNGO PEOPLE'S WATER PROJECT **MAJI SAFI PROJECT**

​

Goal: To build a modern clean water supply system for Ubungo constituency and the surrounding areas. The project will result into a free and open access to clean water for citizens of Ubungo. The fundamental aim is to bypass the cumbersome bureaucratic facilities of the central government which over the years have failed to resolve the water crisis situation in the constituency. If this new model becomes successful other constituencies around the country might find it to the favor and adopt it.

MAJOR ELEMENTS OF THE PROJECT

· MAJI SAFI projects focus on local communities around Ubungo constituency with evident felt need for clean and affordable water. Providing or improving safe water availability should emerge as a priority in the community in the initial contacts and the assessment process.
· MAJI SAFI Projects should assure free and open access by all community members to the safe water resulting from the project.
· Careful assessment of the need and best practice solutions will help assure the success and sustainability of every project. The project will not be limited to wells digging but will include other ways of collecting and storing water.
· Ongoing monitoring and evaluation systems and plans will be included in project planning in order to insure adequate outcome results for the involved community. It is important to establish clear perimeters to ensure optimal outcome.
· Preferably each project should include a training component on pertinent issues impacting safe and available water and broader sanitation issues.
· Cleaning and Upgrading –if necessary replacing - of water supply infrastructure around the constituency.

TARGET AREAS
The project will target a number of areas to bring safe and clean water:
· Schools, community clinics, hospitals – goal to reach about 250,000 people within the first year
· Informal and planned residential areas - goal to reach about 1,000,000 people within 2 years
· Public facilities - such places like markets, public offices etc
MOBILISING RESOURCES
In order for the Maji Safi project to be successful and sustainable a myriad number of resources need to be mobilized and utilized. These will include human resources, machinery, technical know how and finances. The majority of these resources will be sourced within the constituency while others can be outsourced abroad.

….

Some of local patners;
Local small businesses operating in the constituency
Major Tanzanian business working withing Ubungo boundaries
International organizations, companies and institutions
Public and Private Schools and Colleges
Using the CHADEMA’S own mechanism and resources to mobilize resources within the party membership

ORGANIZATION
Office of the Member of Parliament
Board of Directors of Maji Safi Project
…

FINANCES
Estimated take off budget to make the project feasible and sustainable = 5.6 Billions Tsh
Overall projected cost in the next five years = 15 Billions Tsh of which 40% should come from within the community and the sixty percent from donors and financial institutions.

Sasa kitu kama hicho kitaonesha innovation na uthubutu wa kutatua matatizo ambayo yanawezekana. Uongozi wa serikali utatumika pale unapohitajika lakini lengo ni kuwapa watu wanafasi kutatua tatizo lao la maji wao wenyewe kwa kadiri wanavyoweza. Kama inabidi kuanzisa private company kufanya hili na kuwapa wananchi ownership (shareholding) basi hilo laweza kufanywa pale penye uongozi.

Point yangu nikuwa si lazima kuitegemea serikali kwa mambo ambayo imejithibitisha kuwa imeshindwa kufanya. SAsa pamoja na hili pia inaweka mfumo ambapo CDM ikiingia madarakani 2015 basi itaendeleza na kuboresha chini ya serikali yake.
 
  • Thanks
Reactions: SQL
Maji ya ----- na Virongo vinawatosha.
 
Matatizo ya wananchi nchini yanakuwa vigumu sana kuyapatia ufumbuzi mbadala kwa sababu SIASA inawekwa mbele sana kwa kila tatizo katika jamii na matokeo yake hata idara za serikali zinakuwa paralysed.

WanaSiasa wako busy kwenye ubunifu wa jinsi ya kufungana mabao ya kisiasa.
 
  • Thanks
Reactions: SQL
TUTAFANYA MAANDAMANO KWENDA WIZARA YA MAJI TAREHE 16 MACHI 2013; NIMESHAWASILISHA NOTISI, TUENDELEE NA MAANDALIZI

Tarehe 16 Machi 2013 nitaongoza maandamano ya amani ya wananchi kwenda kwa Waziri wa Maji kusimamia uwajibikaji kuwezesha hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar es salaam.

Wote mlioshiriki mkutano wa tarehe 10 Februari 2013 (Kwa wale ambao hamkushiriki mnaweza kutazama video hii: youtu.be/O0txSoHqfGY) , mtakumbuka tulimpa wiki mbili Waziri kujitokeza kwa wananchi kujibu hoja alizokwepa kujibu bungeni.

Tutakusanyika kata ya Manzese eneo la Bakhresa (jirani na daraja) saa 5 asubuhi na tutapita barabara ya Morogoro kuelekea kata ya Ubungo zilipo ofisi za Wizara ya Maji kufuatilia majibu ya ukweli na ukamilifu kuhusu hatua tisa za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka nilizopendekeza kwa niaba ya wananchi bungeni kupitia hoja binafsi na masuala mengine ambayo wananchi watataka yatolewe majibu siku hiyo.

Kila mmoja anaweza kuendelea na maandalizi ya kushiriki kwa kuwa tayari tarehe 4 Machi 2013 nimewasilisha notisi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni na Maafisa wa Polisi Wasimamizi wa Maeneo kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 43 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi Sura ya 322 (The Police Force and Auxiliary Service Act, Chapter 322).

Itakumbukwa kwamba baada ya kutoa wiki mbili Waziri alijitokeza mara tatu ndani ya wiki hizo; mbili kati ya hizo ikiwa ni kupitia mikutano ya CCM na mara moja ikiwa ni kwenye mkutano kati yake na wafanyakazi wa DAWASA na DAWASCO.

Katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Temeke mwisho tarehe 16 Februari 2013, Waziri hakutoa majibu badala yake alirudia tena maelezo yale yale potofu aliyoyatoa bungeni tarehe 4 Februari 2013.

Kwenye mkutano wa hadhara wa Goba tarehe 17 Februari 2013 ambapo aliahidi maji kutoka tarehe 20 Februari, 2013 ambayo hayakutoka. Tarehe 23 Februari 2013 nilifanya mkutano Goba na kutangaza namba zake za simu wananchi wamhoji ahadi hiyo na kutaka Manispaa, DAWASA na DAWASCO waweke kambi Goba mpaka maji yatoke.

Shinikizo hilo limesaidia baadhi ya maeneo ya Goba maji yameanza kutoka hata hivyo maeneo mengi bado hali ambayo inahitaji hatua za haraka nilizopendekeza bungeni kuhusu kata hiyo ziweze kutekelezwa.

Kupitia mkutano wake na DAWASA na DAWASCO tarehe 21 Februari 2013 (tofauti na maelezo yake bungeni) alikiri kwamba kuna upotevu wa maji ikiwemo kwa wizi, kuna biashara haramu yenye kuhusisha hujuma ya miundombinu, bei ya juu ya maji na kutozingatiwa kwa ratiba ya mgawo wa maji katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, zaidi ya wiki moja imepita Waziri wa Maji na Wizara kwa ujumla haionyeshi kwa matendo kuisimamia kwa karibu EWURA, DAWASA, DAWASCO na Manispaa ya Kinondoni kuchukua hatua za haraka ambazo nilizieleza kwenye hoja binafsi.

Hivyo, wote mlioahidi kupitia mkutano wa tarehe 10 Februari 2013 kushiriki maandamano na wote ambapo mnaguswa na matatizo ya maji katika kata mbalimbali za Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar Es salaam tukusanyike Manzese tarehe 16 Machi 2013 saa 5 asubuhi tuandamane kwenda Wizara ya Maji kwa mujibu wa Katiba ya Nchi Ibara za 8, 18, 20 na 21.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb)
05/03/2013

Source:
http://www.wavuti.com/4/post/2013/03/maandamano-kwenda-wizara-ya-maji-tarehe-16-machi-2013.html?utm_source=http%3A%2 F%2Ffeeds.feedburner.com%2Fwav uti&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+wavuti+%2 8Wavuti+%29#axzz2MjPV0ohf
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbona tunayo humu tangu jana..!?
 
We are tired of Maandamano. This country has a lot of things to do, and we can't afford to waste our precious time marching on the street just to fulfill the ambition of certain self-seeking politicians. There are lots of ways, apart from taking to the street, politicians can lead their people to carry out to make their grievances heard.
 
  • Thanks
Reactions: SQL
Sioni uhusiano kati ya kuandamana na maji kutoka.
 
Mkuu kama unaona kuweka namba za viongozi ni njia sahihi ya kuwawajibisha viongozi, weka na wewe za kwako ili tukuwajibishe kwenye maeneo ulioshindwa kwa sababu matatizo ya wanaubungo siyo maji tu;

Hata mimi nilikuwa najua maandamano ni ya amani, mbona unasema kila mmoja aendelee na maandalizi ya maandamano, tunajiandaa nini zaidi ya kuamka siku hiyo mapema na kuja darajani manzese? Ungefafanua kidogo haya maandalizi unayosema tufanye ni namna gani? ya kukabiliana na Polisi kama kawa?;

Mh. mbona unajidhalilisha kiasi hiki , hatukatai kututetea lakini hili la kutangaza namba za simu za viongozi naona kama ni ulimbukeni, utoto au uduni wa elimu vile? kwa nini usingeacha tukazitafuta hizi namba wenyewe. Kwa mtindo huu kweli Utabisha kuwa haukumtumia MWIGULLU ujumbe wa matusi na vitisho?;

Jamani wabunge wetu jitambueni na kujua kuwa mbali na kutafuta umaarufu wa kisiasa , pia kuna utu, maadili na kwamba mntakiwa kuwa mifano ya kuigwa katika jamii.
 
Last edited by a moderator:
We are tired of Maandamano. This country has a lot of things to do, and we can't afford to waste our precious time marching on the street just to fulfill the ambition of certain self-seeking politicians. There are lots of ways, apart from taking to the street, politicians can lead their people to carry out to make their grievances heard.

there you are, so tired.
 
Back
Top Bottom