Mnyika atangaza maandamano tarehe 16 Machi

Mnyika atangaza maandamano tarehe 16 Machi

junpyo

Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
50
Reaction score
9
TUTAFANYA MAANDAMANO KWENDA WIZARA YA MAJI TAREHE 16 MACHI 2013; NIMESHAWASILISHA NOTISI, TUENDELEE NA MAANDALIZI

Tarehe 16 Machi 2013 nitaongoza maandamano ya amani ya wananchi kwenda kwa Waziri wa Maji kusimamia uwajibikaji kuwezesha hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar es salaam.
Wote mlioshiriki mkutano wa tarehe 10 Februari 2013 (Kwa wale ambao hamkushiriki mnaweza kutazama video hii:

Mtakumbuka tulimpa wiki mbili Waziri kujitokeza kwa wananchi kujibu hoja alizokwepa kujibu bungeni.

Tutakusanyika kata ya Manzese eneo la Bakhresa (jirani na daraja) saa 5 asubuhi na tutapita barabara ya Morogoro kuelekea kata ya Ubungo zilipo ofisi za Wizara ya Maji kufuatilia majibu ya ukweli na ukamilifu kuhusu hatua tisa za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka nilizopendekeza kwa niaba ya wananchi bungeni kupitia hoja binafsi na masuala mengine ambayo wananchi watataka yatolewe majibu siku hiyo.

Kila mmoja anaweza kuendelea na maandalizi ya kushiriki kwa kuwa tayari tarehe 4 Machi 2013 nimewasilisha notisi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni na Maafisa wa Polisi Wasimamizi wa Maeneo kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 43 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi Sura ya 322 (The Police Force and Auxiliary Service Act, Chapter 322).

Itakumbukwa kwamba baada ya kutoa wiki mbili Waziri alijitokeza mara tatu ndani ya wiki hizo; mbili kati ya hizo ikiwa ni kupitia mikutano ya CCM na mara moja ikiwa ni kwenye mkutano kati yake na wafanyakazi wa DAWASA na DAWASCO.

Katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Temeke mwisho tarehe 16 Februari 2013, Waziri hakutoa majibu badala yake alirudia tena maelezo yale yale potofu aliyoyatoa bungeni tarehe 4 Februari 2013.

Kwenye mkutano wa hadhara wa Goba tarehe 17 Februari 2013 ambapo aliahidi maji kutoka tarehe 20 Februari, 2013 ambayo hayakutoka. Tarehe 23 Februari 2013 nilifanya mkutano Goba na kutangaza namba zake za simu wananchi wamhoji ahadi hiyo na kutaka Manispaa,DAWASA na DAWASCO waweke kambi Goba mpaka maji yatoke.

Shinikizo hilo limesaidia baadhi ya maeneo ya Goba maji yameanza kutoka hata hivyo maeneo mengi bado hali ambayo inahitaji hatua za haraka nilizopendekeza bungeni kuhusu kata hiyo ziweze kutekelezwa.

Kupitia mkutano wake na DAWASA na DAWASCO tarehe 21 Februari 2013 (tofauti na maelezo yake bungeni) alikiri kwamba kuna upotevu wa maji ikiwemo kwa wizi, kuna biashara haramu yenye kuhusisha hujuma ya miundombinu, bei ya juu ya maji na kutozingatiwa kwa ratiba ya mgawo wa maji katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo, zaidi ya wiki moja imepita Waziri wa Maji na Wizara kwa ujumla haionyeshi kwa matendo kuisimamia kwa karibu EWURA, DAWASA, DAWASCO na Manispaa ya Kinondoni kuchukua hatua za haraka ambazo nilizieleza kwenye hoja binafsi.

Hivyo, wote mlioahidi kupitia mkutano wa tarehe 10 Februari 2013 kushiriki maandamano na wote ambapo mnaguswa na matatizo ya maji katika kata mbalimbali za Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar Es salaam tukusanyike Manzese tarehe 16 Machi 2013 saa 5 asubuhi tuandamane kwenda Wizara ya Maji kwa mujibu wa Katiba ya Nchi Ibara za 8, 18, 20 na 21.

Wenu katika uwakilishi wa
wananchi,
John Mnyika (Mb)
05/03/2013
 
Last edited by a moderator:
Tuko pamoja kamanda Mnyika hata ukisema tuanze saa kumi na mbili asubuhi tuko tayari tumechoshwa na ubabaishaji wa hawa magamba
 
Tuko pamoja maana bila shuruti haya magamba kusikia hoja za wananchi ni ngumu,Tutapambana mpaka kieleweke!
 
Tena wananchi wa ubungo kwa msisitizo wekeni kambi pale na mh Mnyika hadi mtapopigiwa simu na wenzenu maji yanatoka kote kama masaki!

Wakikata tena nitawapa mbinu kali funga mwaka muone kama hawajatoa ratiba ya kueleweka
 
mkifunga pale ubungo mataa na kupafanya Taharir Square kwa masaa sita, watafungulia hayo maji.
 
tuko nyuma yako kamanda maana tukiendelea kuwachekea hawa magamba watatuumiza....
 
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?
 
RC meck sadick kasema,maji hakuna watakaondamana wanapoteza muda
 
Hiyo ndio dawa iliyobakia. Serikali hii bila maandamano hakuna atakayekujali wala kukusikiliza. Tuko pamoja kamanda wetu.
 
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?

Maandamano yanasaidia kuamsha waliolala,wewe unafikiri bila maandamano nchi za kiarabu zingefanya mapinduzi.Wewe wa Masaki nini unataka tuendelee kuumia sie wa Kiluvya huku.Kama mheshimiwa Mbunge alitaka kuleta hoja bungeni ikaondolewa na wanaCCM wako dawa ni kuandamana maana hata akieanda kumuona peke yake haisaidii by the waya sauti ya wengi ni sauti ya Mungu wewe kama hutaki uukalishe nyumbani kwako ambako mbunge wako yeye anaongea na mawaziri halafu kila kitu kinakuwa safi
 
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?

Sijuhi nikuweke kundi gani? Waliopata zero au 4 maana wote failure.
 
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?

Relax dada uone kazi, kuwa mpole tu
 
Maandamano ni hatua ya mwisho kabisa ya watawaliwa kumwonesha mtawala kuwa wamechoka.mnyika kapambana muda mref bungen
 
Anataka kupoteza muda wa watu tu huyu, kazi imemshinda sasa anakimbilia kwa wananchi.2015 hana lake tena, anitafute nimpe kazi ya udereva.
 
Mkuu natamani haya maandamano ungeyaunganisha na umeme tunaanzia wizara ya maji halafu tunavuka barabara tu pale kuingia Tanesco!
 
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?

ulikuwa ukipata ngapi kwenye somo la Civics sekondari?unaonekana hujui kazi za mbunge na wala hujui wajibu wa mwananchi.raia wa aina yenu mnaosubiri viongozi wawafanyie kila kitu ndio mnaosababisha ufisadi uendelee kutafuna nchi hii!uongozi unatoka chini kwenda juu na sio juu kwenda chini!wabongo bwana!wanajua kulalamika tuu na kwenda kwenye semina!
 
Msisahau kubeba na ndoo zenu wakati wakudai maji,
haki haiombwi inadaiwa tena kwa nguvu!
 
jeshi limejipanga vizuri kudhibiti hayo maandamano! hivyo muandae na uji wa kuletewa hospitali!
 
Mbunge kazi yake ni kutumikia wapiga kura wake lakini huyu mchovu anaomba wapiga kura wamfanyie kazi yake, nenda wewe kwa waziri, pambana ili wananchi wako wapate maji, sasa kama maandamano ndio yatawaletea maji wewe unafaida gani. Haya ndio matatizo ya wanasiasa wa Tanzania,unatoa ahadi ya maji wakati huna hata tanker la maji?

We majebere mkerewe nini! maana wakerewe nasikia ndio hawaelewagi mambo yanavyoenda, hivi vita vinatuhusu, hivi vita sio vya mnyika wala magufuli hivi vita ni vyangu mimi na wewe. hivi watu wengine mkojeee! Yaani mpaka kwenye kalenda mna andikiwa kuwa mtajikomboa wenyewe ili ukitizama kalenda ukumbuke kuwa unakubarua cha kujikomboa lakini bado unasubiri mnyika akukomboe
 
Huwa najiuliza hivi kwanini nalipa maji katika mji huu, hayo kidogo yenyewe tunayogomba nayo ni machafu hayafai hata kupigia deki.
 
Back
Top Bottom