Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,753
Kwanza nimpe kongole mdogo wangu John Mnyika kwa kuteuliwa kisha kupitishwa na Baraza Kuu Chadema kishika nafasi ya Ukatibu Mkuu Taifa wa chama hiko.
Anapokea kijiti kutoka kwa Vicent Mashinji ambaye alionekana ni mgeni kwenye Chama na siasa akitokea kwenye taaluma ya udaktari. Wadadisi wengi wa siasa walimuona Mashinji kama kijana wa aliyekuwa Mgombea Urais 2015 kupitia CHADEMA mhe. Lowassa ambaye sasa amerejea CCM.
Jina la John Mnyika halikupewa uzito sana katika nafasi hiyo ingawa watabiri wa siasa waliona uwezekano wa yeye kupokea kijiti kutoka kwa Mashinji ulikuwepo kidogo. Safari ya Mnyika kwenye siasa inaanzia tangu akiwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ambapo yeye na mwenzake Zitto walionekana ni vijana zao halisi la siasa wakilelewa na kuimarishwa upande wa Upinzani. Naweza kisema kwamba Mnyika ni mpinzani wa kweli kwa sababu hakuwahi kushiriki siasa za Chama cha CCM.
Wakati mwenzake Zitto akiungana na prof. Kitila Mkumbo na wenzake kutaka kumpindua Mbowe kwenye chaguzi za ndani CHADEMA, Mnyika hakuonekana kuunga mkono vuguvugu hilo huku akionyesha uaminifu wake kwa Mbowe na kundi lake.
John Mnyika anazifahamu siasa za upinzani, hivyo ni rahisi kwake kuimarisha ngome za CHADEMA katika kipindi chake cha Ukatibu Mkuu Taifa. Anajua kujenga hoja pia ni rahisi kwake kuwashawishi vijana kufuata mfano wake.
Nafasi aliyopewa, inamuweka karibu sana na Mbowe hivyo inawezekana CHADEMA wameona turufu ya Mnyika kuweza kuja kuwa kiongozi mkubwa wa CHADEMA siku za usoni.
Je una maoni gani kwenye hili la kumrithi Mbowe siku za usoni?
Sent using Jamii Forums mobile app