Mnyika amtetea vikali Dr.Slaa

Mnyika amtetea vikali Dr.Slaa

Kilichomkuta Dr. Slaa, ni kutaka kuwa na uhakika wa chadema kuwepo hata baada ya uchaguzi kitu ambacho Mbowe na wenzake hawakutaka kabisa kufikiria. Mbowe na wenzake walikumbwa na upepo wa Lowassa na kuamua kuungana naye bila kutafakari hatima ya chadema baada ya uchaguzi. Sawa na kujiunga na mdundiko bila kujua utaishia wapi. Kazi inakuwa kurudi nyumbani mdundiko ukiisha.

Tukifananisha ya Dr. Slaa na kisa Samson na Delila, maana yake mwisho wa chadema sio mzuri. Kumbuka baada ya Samson kunyolewa nywele alitobolewa macho. wakaendelea na sherehe wakiwa wamesahau kuwa nywele za Samson zinakua na baada ya nywele kukua Samson alimwomba Delila ampeleke kwenye nguzo kubwa ya katikati alipoifikia aliikumbatia na kitikisa. kilichotokea kila mmoja anajua, si samson, Delila na watesi wa Samson aliyebaki, maana nyumba iliwaangukia wote wakiwa ndani na hakuna aliyepona.

Tunasema kuna maisha hata baada ya uchaguzi. Baada ya uchaguzi, je? na mambo yakawa ndivyo sivyo, ni nani kati ya Mbowe na Dr. Slaa ambaye akisimama jukwaani wananchi watamwelewa
Mbowe ndo mchagga halisi. Anajua maana ya shilingi.
 
Mnyika amemtetea vikali Dr.Slaa na kupingana na wale wanaomkejeli na kumuona hana mchango CHADEMA.

Mnyika anasema Dr.Slaa anao mchango wake na yaliyomkuta ni mambo kama yaliyowahi kumkuta Samsoni kwa Delila.

Naomba kuisha hapa.
Kamanda saa zingine unakua unapotoka. Hili bandiko si la afya sana, ila pia halifafanui kayasema hayo wapi, lini na akiwa anafanya nini. Vitu vingine bora potezea tu Mkuu.
 
Vichwa vya habari vya Thread zilizoandikwa Na Waandishi WA Magazeti ya udaku utazijua Tu!
 
Kilichomkuta Dr. Slaa, ni kutaka kuwa na uhakika wa chadema kuwepo hata baada ya uchaguzi kitu ambacho Mbowe na wenzake hawakutaka kabisa kufikiria. Mbowe na wenzake walikumbwa na upepo wa Lowassa na kuamua kuungana naye bila kutafakari hatima ya chadema baada ya uchaguzi. Sawa na kujiunga na mdundiko bila kujua utaishia wapi. Kazi inakuwa kurudi nyumbani mdundiko ukiisha.

Tukifananisha ya Dr. Slaa na kisa Samson na Delila, maana yake mwisho wa chadema sio mzuri. Kumbuka baada ya Samson kunyolewa nywele alitobolewa macho. wakaendelea na sherehe wakiwa wamesahau kuwa nywele za Samson zinakua na baada ya nywele kukua Samson alimwomba Delila ampeleke kwenye nguzo kubwa ya katikati alipoifikia aliikumbatia na kitikisa. kilichotokea kila mmoja anajua, si samson, Delila na watesi wa Samson aliyebaki, maana nyumba iliwaangukia wote wakiwa ndani na hakuna aliyepona.

Tunasema kuna maisha hata baada ya uchaguzi. Baada ya uchaguzi, je? na mambo yakawa ndivyo sivyo, ni nani kati ya Mbowe na Dr. Slaa ambaye akisimama jukwaani wananchi watamwelewa

Watu wanaenda kuchukua Nchi ,wewe bado unawazia kuendelea kuwa mpinzani!?
 
Mwenzenu yuko USA kwenye honeymoon Mtoto wa Kihaya anaendesha Bike kubwa kubwa kama Star wa Hollywood baada ya kuchukua Mpunga wa Kutakata kutoka CCM ... Jamaa amekula maisha Uzeeni si kidogo ... Ndege ya Kukodi ilimtoa SA hadi Bongo ... Bata Mwanzo Mwisho .. Gwajima aliua, Ila Kubenea Alimzika Rasmi Slaa ...
 
Slaa, Rais wa mioyoni mwa bavicha: Naukumbuka sana msemo huu.

Bavicha na M4C walikuwa wanategemea nguvu ya umma na si pesa. Ndio maana kila baada ya mkutano yalikuwa yanapita mabox kwa ajili ya uchakavu. Sasa pesa ya Lowassa imeua mpaka M4C badala yake ile 4U movement aliyotoka nayo CCM ndio wanaotamba humu jf. Chezea fisadi papa wewe. tunasubiri uchaguzi uishe tukae mguu sawa
 
Kuwa na mchango ktk kujenga kitu hakuhalalishi kutonyooshewa vidole pale unapopotoka au unapohisiwa kusaliti ulichokijenga. Utaitwa msaliti tu.

Tatizo la Dr Slaa ni kuonesha mwelekeo wa kuanza kukibomoa chama alichokijenga. Alipokuwa kimya hakuna aliyemrushia mawe lkn alipofumbua kinywa chake kusema yasiyo kweli anastahili kujibiwa
 
Watu wanaenda kuchukua Nchi ,wewe bado unawazia kuendelea kuwa mpinzani!?

Yes, haijalishi. Upinzani wangu ni nchi kuchukuliwa na wezi. vile vidole viwili vilipokuwa juu ilikuwa ni chadema kweli. Lakini baada ya Mbowe kubadili gia angani vile vidole vimeangalia chini yaani ile ni alama ya wezi wa mfukoni. Hata wewe mwenyewe hapo ulipo, pandisha vile vidole viwili vya chadema ya zamani, kisha shusha chini mkono vidole viwili vingali vilevile. Haya niambie unapata alama gani sasa.
 
Mnyika amemtetea vikali Dr.Slaa na kupingana na wale wanaomkejeli na kumuona hana mchango CHADEMA.

Mnyika anasema Dr.Slaa anao mchango wake na yaliyomkuta ni mambo kama yaliyowahi kumkuta Samsoni kwa Delila.

Naomba kuisha hapa.

Unaonaje ukimalizia na limao?
 
Wanaosema lowasa ni fisadi labda ni walio ingia tz jn ila ukiulizwa fisadi nyangumi ni kikwete na riziwani walioingia ikulu kwa baiskeli.lkn wametoka na viwanda lukuki bgmy,ndege,sheli za mafuta,hoteli na rasilimali zt za tz wamewauzia wachina na usa.....dr slaa angekuwa mtu wa maana asingenunuliwa km peremende hvy..
FISIEM HOVYO..UKAWA DAIMA

Pamoja na ukweli huo wasichokielewa wengi ni kuwa kosa moja huondoa mazuri mengi uliyowahi kuyafanya. Nyerere akiwa hai aliwahi kuonya huwezi kuendesha ikulu kwa mawazo ya mkeo.Asichoelewa Mnyika na uzoefu wake wote ni kuwa ya Samson na mkewe Dellilah yalikuwa makusudio ya mungu kuwakumbusha waja wake kuwa niliwahi kuwaonyeni muishi kwa akili sana na hawa wenza wenu. Kwa hiyo kilichompata Samson ni mungu alitaka kuwakumbusha tena waja wake. Ukiwa mwanasiasa mwenye nafasi kama aliyokuwa nayo dr. Slaa unatakiwa uwe na ngozi ngumu na maamuzi ya vikao vya chama uyaheshimu bila kuwepo ushawishi wa rafiki au mkeo na bahati mbaya kwake alishiriki mchakato toka mwanzo wa zoezi hadi maafikiano ya vikao. Mkewe hakuwa mjumbe wa vikao hivyo.Tena ujue miaka miwili nyuma chadema walishapitisha sheria kuwaonya viongozi wao kuwaonya wake zao kutoingilia masuala ya chama nadhani walishaona mwenendo wa mke wa Slaa. Kama mtakavyokumbuka madhumuni ya vyama vinne kuungana na kuunda ukawa yalikuwa mawili. Kwanza kutetea katiba bora ya wananchi bunge la katiba. Pili ni kuiondoa madarakani ccm na mfumo wake kwa kumsimamisha mgombea uraisi mmoja miongoni mwa wanachama wa vyama shiriki,hadi ngazi ya ubunge na udiwani. Walijua yanaweza kujitokeza mapungufu fulani kwenye vyama shiriki lakini wote walikubaliana kurekebisha kasoro hizo baada ya zoezi. Hivyo haipo sababu itakayotolewa na yeyote alieshiriki makubaliano iwe kwa Lipumba wala Slaa. Fahari za u-first lady za mkeo zikusababishe uende kinyume na makubaliano ni usaliti kwa ukawa na wanachama wake na wapenda maendeleo wote nchini . Tutakuweka pembeni na utasahaulika tu. LOWASSA MABADILIKO MABADILIKO LOWASSA.
 
Ipo siku wata mjua slaa kama ni zaidi ya mbowe, ila kwaku kiuza chama ni halali kwani anachotaka mbowe ni pesa zaidi sasa pesa ndio iliwekwa mesani! Hata wengi wetu hapa tuna ongea tu ila mamilion yakiwekwa mezani lazima ubadili msimamo, ubaya utaonekana baada ya uchaguzi ila mtu kaishabakia Tajiri zaidi
 
Dr Slaa ameiimarisha sana CDM bahati mbaya kwenye hiyo safari ya "train ya wanasiasa" ameshukia Tabora kabla ya kufika Kigoma
 
Back
Top Bottom