Mnyeti: Tanga Cement irudi kuwa Mali ya Serikali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

ALEXANDER MNYETI ATAKA TANGA CEMENT IRUDI KUWA MALI YA SERIKALINI

Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Alexander Pastory Mnyeti tarehe 04 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishw akwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji

"Ukiunganisha kiwanda cha Twiga Cement na Tanga Cement ushindani hautakuwepo, bei atakuwa anajipangia. Leo kule Mwanza tunanunua saruji hadi shilingi 25,000 kwa mfuko, sasa Twiga Cement akiununua Tanga Cement na kuamka asubuhi aseme leo mfuko sh. 40,000 na hakuna wakushindana, sisi walaji tutafanyaje. Naomba serikali muangalie namna ya kuokoa changamoto hii ili watumiaji wa mwisho wa saruji waweze kuipata kwa gharama nafuu" Alexander Mnyeti, mbunge wa jimbo la Misungwi

"Kwanini tunashindwa kuweka wazi, kiwanda hiki kilikuwa ni miongoni mwa vilivyokuwa viwanda vya serikali. Kule Tanga kuna viwanda viwili vya chuma ambavyo wawekezaji walishindwa kuviendeleza na serikali imevichukua, najiuliza swali dogo sana kwanini hiki kiwanda (Tanga Cement) kwa masharti hayo hayo kisirudi serikalini?" Alexander Mnyeti, mbunge wa jimbo la Misungwi

FvSyxSPXsAAoLvG.jpg
 
NILIWAHI KUGUSIA SEHEMU HILI SAKATA LA TWIGA KUNUNUA TANGA CEMENT. Nianze kusema kuwa hii sekta ya Cement ni non regulated sector japo ni sector muhimu sana kwa ujenzi wa Taifa.Cement ni moja kati ya mahitaji muhimu kwa kwa ujenzi wa nchi hii na kuna mahali haina mbadala(Substute).Unaporuhusu watu wachache watawale soko nanuzalishaji wa cement ni hatari sanaa, uuzwaji wa Tanga kwa Twiga Cement Unamaanisha kwamba unapunguza wazalishaji sokoni kuwa wachache zaidi hivyo kupelekea umiliki wa soko hulia,Maana yake ni kwamba TWiga atakua anaamua azalishe kiasi gani kwa muda gani maana viwanda ni vyake.Tanzania tunaviwanda vikubwa vinne.Dangote cement,Twiga,Mbeya na Tanga Cement.Kuruhusu Twiga kununua Tanga Cement ni shida kubwa inamaana Tanga itakua chini ya Twiga na wazalishaji watakua watatu sio wanne tena,Hatari ya Upangaji Bei itatokea.Upangaji Bei utaiweka nchi katika wakati mgumu na kuathiri shughuli za kiujenzi kwa serikari na wananchi moja mmoja.VIpi Dangote akiinunua Mbeya Cement? Ikumbukwe kuwa Tanga Cement Ndio Kiwanda pekee chenye malighafi kubwa zaidi na nyingi kuliko vyote katika ukanda wa afrika mashariki,Najiuliza Unakuaje anapata hasara?Hapa kuna harufu ya usimamizi mbovu
 
Hakuna Serikali ya TZ itaweza kurun hizi mambo na kuleta ufanisi zaidi ya blah blah na matatizo tu, hapo kila siku serikali itapeleka kodi za wananchi kama ruzuku wakati Kaburu hapo walikuwa wanapiga profit..

Kaburu AFRISAM group ameshapiga hesabu zake zimekataa na hayuko tayari kupump more money kucountebalance mtaji, kinachofanyika ni engineering maneuverbility aendelee kukusanya hela kwa kutumia mtambo mbovu huku akisuburi TWIGA au mtu mwingine aingie kichwakichwa amuuzie jumba bovu atembee...

Wanasiasa wengi wa Tanzania, they are not well informed na hawako tayari kuzama deep kupata A,B,C, D za mambo mbalimbali ndio maana wanakuwa kama "headless chicken" wanapojadili critical issues
 
Hakuna Serikali itaweza kurun hizi mambo na kuleta ufanisi zaidi ya blah blah na matatizo tu, hapo kila siku serikali itapeleka kodi za wananchi kama ruzuku wakati Kaburu hapo walikuwa wanapiga profit..

Watu wenye akili nzuri ni wachache sana na miongoni mwao wapo wchache zaidi wanaoitumia kwa ufanisi.
Mbaya zaidi, wasio na akili hawajui kuwa hawana na hivyo kujiweka mbele na kubebwa na halaiki ya majuha (changamoto kubwa katika siasa zetu)
 
Hakuna Serikali itaweza kurun hizi mambo na kuleta ufanisi zaidi ya blah blah na matatizo tu, hapo kila siku serikali itapeleka kodi za wananchi kama ruzuku wakati Kaburu hapo walikuwa wanapiga profit..

Kaburu AFRISAM group ameshapiga hesabu zake zimekataa na hayuko tayari kupump more money kucountebalance mtaji, kinachofanyika ni engineering maneuverbility aendelee kukusanya hela kwa kutumia mtambo mbovu huku akisuburi TWIGA au mtu mwingine aingie kichwakichwa amuuzie jumba bovu atembee...

Wanasiasa wengi wa Tanzania, they are not well informed na hawako tayari kuzama deep kupata A,B,C, D za mambo mbalimbali ndio maana wanakuwa kama "headless chicken" wanapojadili critical issues

Mkuu Uko Sahihi kabisa
Kwa Sisi Tuliowaho Kufanya Kwenye Hivyo Viwanda Vyote TUNAYAJUA HAYA!
Raisi Dr.Mama Samia Suluhu Hassan Anatakiwa Apewe taarifa Sahihi za Kii intelligence
sababu Utakuja Kutokea Mfumuko wa bei za Cement na Hivyo Kuondoa Ushindani!Kwanini wanataka Twiga Awe Monopoly Kwenye Soko?
Kiukweli Sekta ya Saruji Ndio Moyo wa Uchumi kwa maana ya Ujenzi wooote!
Angalalia Wenzetu China wanajenga Madaraja na Flyover kwa bei nafuu kabisa!
Huku kwetu ni mara 3 za bei zao!
Unajua kwanini?
Sababu Ni kuwa kule kwao Serikali Inamiliki Viwanda Vya Cement!
Makampuni ya Cement,Serikali ina Share kunwa mnoo
makampuni kama SINOMA state owned company.
Sisi Huku eti Ki flyover cha Nusu Kilometer Gharama yake duuu
Ujenzi ni backborne ya Uchumi!siku hizi Cement inatumika Mpaka kwenye ujenzi wa Barabara!
Ukiona Hivyo ujue Labda kuna wakubwa wanataka hilo Dili!
Hawaangalii Nchi wanawaza Mgao wao wakifanikisha tuu?
 
Je sababu za serikali kubinafsisha kipindi hicho zimebadilika?

Niliwah sema humu, serikal zote duniani ni incompetent kufanya biashara.

Aje na mifano hata mitatu tu ya investment ya serikal inayofanya vizur... mimi nitampa 1000 nikianza na ATCL, TTCL, UDA, TPB, NBC, NICOL, Tanzania Posta na Simu etc

Ku privatize na serikal kuwa na hisa humo is the best Idea ever...

Hizi akili za ujamaa ndio ziliua viwanda vyote hapa Tanzania.
 
Kwa Siasa za kwetu bila logics sisi wengine ambayo siyo wataalam hatuwezi kuelewa yupi yupo sahihi!
 
Hizi ni international business na kila kitu kinafanywa realistically sio kupiga ramli kama tulivyozoea, Mmiliki Afrisam alishapiga hesabu zoote za kitalaam kuanzia engineering, procurements, financial issues nk, amefanya mpaka forecast siajabu hata ya 20yrs vs profit yake na stability yake ameshaona giza.

Wasiojua na labda hata Mnyeti na hawa headless chicken wengine, pale kuna madeni mengi sana likiwemo deni la mchina Sinoma, suppliers nk... plant moja ni mbovu with frequent breakdowns, plant moja ya mkopo na imeshamature deni linalipwa huku warrant pia ikiwa imeisha na plant yenyewe ni mbovu (Chinese type)... ukinunua unanunua na madeni.

Tahadhari: hawa wanasiasa wengine waangaliwe makini sana, isije ikawa chezo na tayari mifuko imeshatuna, ili GOT iingie kichwakichwa inunue kiwanda na madeni na kaburu Afrisam akimbie zake akiwa ametuachia mimba...

TWIGA ameshapiga hesabu kubwa pale na nina uhakika bado hii dili haijafungwa maana wote wamekutana Sungura, Twiga kama amenunua basi tambua kuna mahala ameshalalia ambapo ni very weak point na huwa ni GOT, nina wasiwasi na zile hisa za GOT, kodi yetu kwenye mauziano, kodi yetu baada ya mauziano na namna madeni yatakavyomalizwa kwa kafara ya kodi za Watz..

Tunahitaji watu wenye akili sana hasa na hizi International business, wazalendo kwelikweli na uchungu na nchi yao kudeal na hili jambo kwa siri na undani sana na si hawa wapiga ramli, waganga njaa, headless chicken, wabinafsi na pumbavu wanaowaza leo ya famili yao na sio kesho ya Taifa lao ambalo limewapa dhamana kulitumikia na uaminifu na heshima kubwa.
 
ALEXANDER MNYETI ATAKA TANGA CEMENT IRUDI KUWA MALI YA SERIKALINI

Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Alexander Pastory Mnyeti tarehe 04 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishw akwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji

"Ukiunganisha kiwanda cha Twiga Cement na Tanga Cement ushindani hautakuwepo, bei atakuwa anajipangia. Leo kule Mwanza tunanunua saruji hadi shilingi 25,000 kwa mfuko, sasa Twiga Cement akiununua Tanga Cement na kuamka asubuhi aseme leo mfuko sh. 40,000 na hakuna wakushindana, sisi walaji tutafanyaje. Naomba serikali muangalie namna ya kuokoa changamoto hii ili watumiaji wa mwisho wa saruji waweze kuipata kwa gharama nafuu" Alexander Mnyeti, mbunge wa jimbo la Misungwi

"Kwanini tunashindwa kuweka wazi, kiwanda hiki kilikuwa ni miongoni mwa vilivyokuwa viwanda vya serikali. Kule Tanga kuna viwanda viwili vya chuma ambavyo wawekezaji walishindwa kuviendeleza na serikali imevichukua, najiuliza swali dogo sana kwanini hiki kiwanda (Tanga Cement) kwa masharti hayo hayo kisirudi serikalini?" Alexander Mnyeti, mbunge wa jimbo la Misungwi

View attachment 2610852
Mnyeti Mzee wa ukuta wa mererani enzi za jiwe 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom