Mnyama anaua mara moja binadamu anaua mara tatu

Mnyama anaua mara moja binadamu anaua mara tatu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,520
Reaction score
830,064
Tumewapa wanyama hadhi ya uhayawani kwakuwa hawana utashi wa kibinadamu... Lakini nina hakika tumewaonea Sana

Mnyama anaua tu pale anapohisi hatari kubwa na anafanya hivyo kwa njia ya kujitetea.. Akipata nafasi hukimbia.. Hana kisasi
Mnyama anaua tu pale anapoumwa njaa ili apate chakula. Na hana mbwembwe za kuweka viungo na kuchoma ama kukaanga

Mnyama hana majeshi na timu za siri za kuteka, kutesa na kuua...
Mnyama hana vyombo vya mapishi vikiwemo visu
Mnyama hana jela za siri alimofungia watu waliojaa majeraha na maumivu kwa ajili ya kuteswa
Watu hao kutwa kucha wamelala sakafuni hawajiwezi, hawajui kama ni usiku ama ni mchana
Hawajui kama ni Jumatatu ama ni Ijumaa
Binadamu mwenye utashi sasa.. Na anayeitwa mstaarabu Sana... Anaua hata kama hana njaa
Anaua kwa visasi
Anaua kwa roho mbaya
Anaua kisa madaraka

Mnyama akishaua anakula hapohapo.. Kilichouliwa hakina kupitia maumivu mengine tena.. Ndugu yangu na mie sasa.. Ataua, atamuandaa. Atampitisha kwenye kifo cha pili na cha tatu
Atamchuna maumivu mengine haya
Atamchemsha. Wengine watachoma na wengine watamkaanga maumivu mengine haya.. Kisha atamuunga na viungo mbalimbali halafu ndio amle .. Maumivu juu ya maumivu.. Hatua ya mwisho mabaki ya mifupa wapewe paka na umbwa

Hivi mpaka hapa ni nani hayawani kati ya mnyama na binadamu?
Mnyama hamiliki silaha za maangizi
Mnyama hamiliki teknolojia ya kuua
Mnyama hamiliki shule za mapishi
Ikitokea mnyama kakuua anakuacha hapo hapo na kuondoka.. Binadamu anakutesa mpaka anakuua kisha anaweza kukuficha ama kukutupa mbali usionekane tena!

Ni ujuha kiwango cha lami umekaa bar unasubiri mchemsho, amazing nyala choma na wakati huo unaangalia kipindi cha wanyama kwenye tv ukimlaani simba anayemuua swala.. Ni ujuha tuu
1751075056520.jpg
1751075052668.jpg
 
Napiga bapa langu nikisindikizia na huo ugali nyama choma 😇😇😇
 
Back
Top Bottom