Mnasema wanaume ni "never mind"? Hapana, Wanawake wana msaada sana

Mnasema wanaume ni "never mind"? Hapana, Wanawake wana msaada sana

Katika kila tatizo kuna mtu atajitokeza tu wa kukusaidia. Unachotakiwa kujua ni kwamba, mwanamke sio wa kumuamini kama ndugu yako, wana maamuzi ya kushitukiza (papo kwa papo).
 
Ni kweli mkuu nimetoka ktk hayo matatizo wke mbili zilizopita marafiki wa kiume sio kwa upande wng kuna baadhi walishafanya shereke kwakuwa nimepotea ila nashukuru niko uraiani kwa kupiganiwa na wife
Bora umetoa ushuhuda mkuu naendelea na utafiti
 
Duuh! Haya kama mnazo pesa Mfanyage tu japokuwa naiona haina tofauti na kutia mkono kizani hiyoo.

Japokuwa kwa mbaali nawaza ni Ke wangapi ambao wana akili za kuomba kufunguliwa biashara au hata kuwa na mawazo hayo hasa wakiwa na Me wenye kuwapa pesa ya maana zaidi ya kufanya mambo ya kujionyesha onyesha ikiwemo kuvaa na vitu vingine visivyo na faida.
Dada siku zote uko +ve!
 
Juzi nimekutana na jamaa yangu mmoja mfanyakazi wa shirika moja la umma lenye ukwasi mkubwa huku na yeye akiwa ni mtu mwenye uwezo wake na anapenda kujirusha sana na mpenda totoz.

Rafiki yangu huyu alikuwa amepata matatizo kazini na akafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi iliyofanya akae ndani(mahabusu) karibu mwaka na nusu. Bahati nzuri ameshinda kesi na sasa yupo katika kufatilia taratibu za ama kurudishwa kazini au apewe chake asepe.

Katika maongezi yetu akaniusia "Mdogo wangu hakikisha wapenzi wako unawasaidia kwa kila hali. Ukiweza wafungulie biashara, usihonge sijui elfu ngapi, mpe mwanamke wako hela ya maana."

Akaniambia kama ukipata milioni 30 mpe hata milion kumi, wanawake wanakumbuka fadhila sana na wana msaada katika matatizo.

Anasema hata ndugu wanaweza wasikusaidie kwenye matatizo pamoja na kuwa umewahi kuwasaidia sana. Kanambia katika kipindi chote alichokaa ndani wanawake zake wamemsapoti sana kwa kumtia moyo, kumhurumia na kumhudumia kwa mambo mbalimbali na alikuwa anahisi kabisa hisia zao za huruma ni za kweli kabisa tofauti na marafiki zake wanaume.

Aliponichosha ni pale aliponitajia majina ya marafiki zetu kadhaa wanaume wenzetu kauli alizoambiwa kuwa walikuwa wanazitoa dhidi yake baada ya yeye kupata matatizo. Wengine walikua wanasema akome sasa anajifanya anazo, wengine walitamani afungwe kabisa eti mademu zao walikuwa wanamshobokea, na wapo waliofurahia tu yeye kupata matatizo.

Mimi nathibitisha kuwasikia jamaa tena aliokua nao karibu kwenye kula bata wakimsema kwa ubaya.

Hapa natafakari usia na kauli hii ya rafiki yangu na nahisi kama ina kaukweli fulani hivi ila naendelea kufanya utafiti wa kina nione kama naweza kuipitisha na mimi niitumie kama msimamo na mtazamo wangu rasmi.
Mmmhhh!!! Mkuu hii ngumu kumeza sana kwangu hawana maana hawa viumbe, bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi utakuja liwa na Simba...Ukichalala wanakukimbia hao wanaenda kwa bwana mwenye hela
 
Back
Top Bottom