Mnasema wanaume ni "never mind"? Hapana, Wanawake wana msaada sana

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,561
19,056
Juzi nimekutana na jamaa yangu mmoja mfanyakazi wa shirika moja la umma lenye ukwasi mkubwa huku na yeye akiwa ni mtu mwenye uwezo wake na anapenda kujirusha sana na mpenda totoz.

Rafiki yangu huyu alikuwa amepata matatizo kazini na akafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi iliyofanya akae ndani(mahabusu) karibu mwaka na nusu. Bahati nzuri ameshinda kesi na sasa yupo katika kufatilia taratibu za ama kurudishwa kazini au apewe chake asepe.

Katika maongezi yetu akaniusia "Mdogo wangu hakikisha wapenzi wako unawasaidia kwa kila hali. Ukiweza wafungulie biashara, usihonge sijui elfu ngapi, mpe mwanamke wako hela ya maana."

Akaniambia kama ukipata milioni 30 mpe hata milion kumi, wanawake wanakumbuka fadhila sana na wana msaada katika matatizo.

Anasema hata ndugu wanaweza wasikusaidie kwenye matatizo pamoja na kuwa umewahi kuwasaidia sana. Kanambia katika kipindi chote alichokaa ndani wanawake zake wamemsapoti sana kwa kumtia moyo, kumhurumia na kumhudumia kwa mambo mbalimbali na alikuwa anahisi kabisa hisia zao za huruma ni za kweli kabisa tofauti na marafiki zake wanaume.

Aliponichosha ni pale aliponitajia majina ya marafiki zetu kadhaa wanaume wenzetu kauli alizoambiwa kuwa walikuwa wanazitoa dhidi yake baada ya yeye kupata matatizo. Wengine walikua wanasema akome sasa anajifanya anazo, wengine walitamani afungwe kabisa eti mademu zao walikuwa wanamshobokea, na wapo waliofurahia tu yeye kupata matatizo.

Mimi nathibitisha kuwasikia jamaa tena aliokua nao karibu kwenye kula bata wakimsema kwa ubaya.

Hapa natafakari usia na kauli hii ya rafiki yangu na nahisi kama ina kaukweli fulani hivi ila naendelea kufanya utafiti wa kina nione kama naweza kuipitisha na mimi niitumie kama msimamo na mtazamo wangu rasmi.
 
Last edited by a moderator:
Duuh! Haya kama mnazo pesa Mfanyage tu japokuwa naiona haina tofauti na kutia mkono kizani hiyoo.

Japokuwa kwa mbaali nawaza ni Ke wangapi ambao wana akili za kuomba kufunguliwa biashara au hata kuwa na mawazo hayo hasa wakiwa na Me wenye kuwapa pesa ya maana zaidi ya kufanya mambo ya kujionyesha onyesha ikiwemo kuvaa na vitu vingine visivyo na faida.
 
Ndio naangaza angaza nimpate wifi yako mmoja kwanza, ila usiyapeleke kwa mama basi
Hahahahaha me naona heri upate mwanamke ambae unaona huyu utakua nae bega kwa bega mtengeneze maisha yenu ndio ufanye hivo vinginevyo kaka kama una pesa sana kasaidie hata wale watoto wanaoishi mazingira magum asee, mama simwambii mana najua mnaweza gombana bure
 
Japokuwa kwa mbaali nawaza ni Ke wangapi ambao wana akili za kuomba kufunguliwa biashara au hata kuwa na mawazo hayo hasa wakiwa na Me wenye kuwapa pesa ya maana zaidi ya kufanya mambo ya kujionyesha onyesha ikiwemo kuvaa na vitu vingine visivyo na faida.
Wengi Ke huwa wanataka vitu vya luxury na Me hua wanaona sawa tu wanawapa hivyohivyo, lakini wote wngekua wanajiongeza wangweza fanya mambo yenye faida na kuendelea
 
Hahahahaha me naona heri upate mwanamke ambae unaona huyu utakua nae bega kwa bega mtengeneze maisha yenu ndio ufanye hivo vinginevyo kaka kama una pesa sana kasaidie hata wale watoto wanaoishi mazingira magum asee, mama simwambii mana najua mnaweza gombana bure
Wala sina pesa sana dada yangu kipenzi ila si unajua tena wanaume tukutanapo tunapeana maneno ya kujaribu mbinu mbalimbali za kujipanga kiume, ni kama nyie wanawake tu mkutanapo na story zenu za kusadikika

Ila nilichomuelewa rafiki yangu yule alisema wasaidie wapenzi wako kwa kujiangalia yeye na wingi wa alokua nao lakini mimi nina maanisha mpenzi, tena aweza kua mke, unajua kwa mazoea ya kiswahili mke tunamtoa kwenye kundi la mpenzi sijui kwanini dada!?
 
kwa hiyo na shemejio saa hizi anapewa mawazo kama haya eeeh??

Me nakuombea upate mwenza sahihi ambae baadae aje kua mkeo kaka, anatolewa sababu watu tunafikiri mpenzi ni hivi tu mnadate kuibana kila mtu kwa mwenzie hajulikani lakini mke ni official huyo watu wanafaham japo mke ni mpenzi vile vile sasa sjuu hua yawaje
 
kwa hiyo na shemejio saa hizi anapewa mawazo kama haya eeeh??
Naamini hata kama anapewa mawazo kama haya au mengine atachanganya na zake dada, nina imani atayachukua mawazo hayo akaja akayafanyia kazi kwako, atakua kapata mawazo mabaya kayapeleka pazuri, kuna shida hapo Madame...Ni kama nyie huko mnavyokutana na vishawishi vya kila aina kwani ni lazima kuvikubali, relax sis
 
Back
Top Bottom