Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,635
- 6,535
Nilikaa mbali na mijadala ya kisiasa kwa muda ila nimelazimika kulisema hili. Huu uzi nilikusudia kuuleta kitambo sana ila nikawa napotezea au kuahirisha kuuleta.
Kuna watu kutokana na sababu wanazojua wao wamekuwa wanatoa kauli za kutaka JWTZ lichukue uongozi wa nchi. Kuna wakati hadi nahisi kuna wanaharakati ambao ni mapandikizi waliowekwa ili kuwalinda CCM na viongozi wake pale hali itakapokuwa ngumu sana kwao.
Nasema hili la jeshi linaweza kuwa pona ya CCM. Kama mnataka mrudi nyuma hatua 50 kwenye demokrasia basi mkubaliane na hilo.
Sehemu kama Sudan, harakati za demokrasia zilizikwa rasmi baada ya jeshi kuingilia kati. Misri ni hivyo hivyo. Maeneo mengi tu demokrasia ilirudi nyuma sana baada ya mapinduzi ya kijeshi.
Mnapopambana kupata uchaguzi huru na wa haki, msitamani kamwe njia za mkato kama hizo za kutaka jeshi lichukue nchi.