Uchaguzi 2020 Mnaojiandaa kukatwa kesho someni hapa ili mjiandae kisaikolojia

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,749
21,202
Kamati kuu ya CCM inayoendelea na vikao vya kuchakata majina ya wagombea nafasi ya Ubunge jijini Dodoma inaendelea na kazi moja kubwa na yenye machungu kwa safari ya ahadi.

Kitu kimoja ambacho wale walio ndani ya tatu bora wanapaswa kuichukua hasa wale wanaojipanga endapo watakatwa wasepe/waondoke na kijiji nafasi hiyo uenda, nasema uenda isiwepo na watabaki kuunga juhudi kwa lazima ndani ya chama.

Ikumbukwe vikao hivi vimechelewa kuanza kutokana na inteljinsia ya CCM kung'amua mpango unaosubiliwa na wao au vyama vya upinzani kwa garasa ambazo zitaachwa ili wakose pa kwenda.

SOMA...

Mpango mahususi ni huu hapa, msema chochote wa CCM Humphrey Polepole alitoa taarifa kwa wagombea wote wawepo kwenye vituo vyao vya kuchukulia fomu, kwa wajuzi wa mambo hii imekaa kimachale sana.

Papo kwa hapo majina ya wagombea yatasomwa siku ya mwisho kabisa kabla ya kurudisha fomu ili pale mgombea anapotangazwa (akiwa tayari na taarifa) anaenda kuchukua fomu (faster) kujaza na kurudisha kwa haraka sana.

Na ndipo wale watakaoisoma namba watashindwa ku_jump upande wa pili na kurudi nyumbani na kilio kikuu na kusaga meno, ambapo masaa machache dirisha la usajili linafungwa rasmi.

Hapo ndipo unaweza kuona chama janja kikongwe wameweza kucheza mchezo wa kupaki basi kwenye final ili kuwapatia hukumu wale wanaosubili makombo au wenye mlengo wa kutaka kukidhoofisha chama kiaina.

Kwenu ACT, CDM nk kwenye majimbo ambayo hamjasimamisha wagombea fanyeni hima mkasimamishe watu, vinginevyo itakula kwenu.

👋 Alamsiki.
 
Eti chama janja....kwani mliona wangechukuliwa na upinzani ndio ccm wangeumia zaidi? Hamna akili kabisa. Sasa hivi mnapelekeshwa na upinzani kwasababu ya kuwabana miaka 5 leo mnarudia ujinga uleule? Akikatwa ina maana na ushawishi wake mnauzuia. Mnaogopa hasira ya mtu mmoja kuliko ya wafuasi wake? Subirini muone.
 
Kuna watu wanakatwa vibaya sana!
FB_IMG_1597846617926.jpeg
 
Back
Top Bottom