Mnaoamini kuna uchawi mko nyuma sana

Mnaoamini kuna uchawi mko nyuma sana

Kama huamini uchawi..njoo mtaani kwetu..kuna bibi mmoja nitakuonyesha..mchukue mpige mtama..mpige vibao..halafu tuone kama utaamka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawaulize kwanza wazazi wako wamekuleaje hadi umefikia umri huo, inawezekana brother una chale hadi matakoni ambazo ulichanjwa ili usidhurike, ulifungwa hirizi shingoni na kiunoni, inawezekana pia kuna kamkoba ka uchawi kanakusubiri huko kwenu ila hujaambiwa.

Nakuombea Mungu pia wachawi wasone huu uzi wakujie usiku wakukabeee hadi unye.

Nahakika kukicha salama utakuja na uzi mbadala wa huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakunaga uchawi duniani tuache kudanganyana na kunyweshana chai kwa visa vya kutunga..Mimi nauhakika hakuna uchawi ndo maana mpaka Leo hii sijawahi kukutana na uchawi..watu wengi wanaoamini Kama Kuna uchawi point yao kubwa huwa wanasema eti kwenye bible imeandikwa kuna uchawi..au wengine wanadai eti karatasi moja iliponyoka kwenye kitabu Cha Mungu ndio inayotumika ulimwenguni kufanyia uchawi.zote hizi sio kweli hakuna uchawi jamani elimikeni acheni kuamini dhana na hadithi za kutunga.hakuna uchawi Mimi nauhakika hakuna mwanadamu ana maajabu ya kutisha kama ambayo tunasimuliwa kwenye visa vya kichawi..mwanadamu uwezo wake mkubwa Ni kuweza kukwepa majanga mfano maradhi na ajali huo ndio uwezo tulionao hakunaga uchawi acheni uwoga wa maisha ndugu zangu.

UCHAWI UPO NA UNATAJWA KATIKA BIBLIA: SOMA HAPACHINI.

»Shetani anawasaidizi wake watendao kazi pamoja naye. Wasaidizi hawa huitwa PEPO WABAYA au MAJINI au MASHETANI. Katika biblià majina haya yote yanazungumzia jambo moja (WAEFESO 6:11-12 ; MAMBO YA WALAWI 17:7; KUMBUKUMBU LA TORATI 32:17 ; ISAYA 13:21 ; 1 WAKORINTHO 10:20-21).

»UCHAWI ni kufanya tendo la kushirikiana na pepo au majini au mashetani hawa na kuwatumia ili kuwadhuru watu wengine.

»Kazi ya Shetani ni kuchinja, kuua , kuharibu na kuibiba chochote chema tulichonacho (YOHANA 10:10).

»Pepo hawa hawaonekani kwa macho ya kawaida na tena wanaweza kupenya na kufanya makao ndani ya kiungo cha mwanadamu hata kilicho kidogo sana kama mshipa na kukiharibu.

»USHIRIKINA ni ushirikiano na MASHETANI katika kukamilisha kazi zao mbaya.

»Mtu anaweza kufanya mambo ya kushangaza yasiyo ya kawaida au asili(SUPERNATURAL) kwa kutumia nguvu za giza za Shetani au uchawi kama Simoni mchawi (MATENDO YA MITUME 8:9-11).

»Kwa kutumia nguvu za kichawi mtu anaweza KUMLAANI mtu nakupatwa na madhara. Mfano, mtu anaweza kumlaani mtu aliyemwibia fedha zake na kupatwa na madhara mpaka wakati atakapokiri kuzichukua na kuzirudisha kama alivyotendewa MIKA (WAAMUZI 17:1-2). Laana inaweza kuathiri familia nzima, ukoo na hata kizazi hadi kizazi.

»
Wachawi walikuwepo tangu zamani. Kabla ya Yesu Kristo, tangu zamani za Farao wa Misri na nyakati zinazofuata wanatajwa wachawi wengi(KUTOKA 7:11; YOSHUA 13:22; 1 SAMWELI 28:9; 2 WAFALME 21:1-2,6; ISAYA 19:3; ISAYA 57:3; DANIELI 2:2; DANIELI 5:7).

»Hata baada ya Yesu Kristo, nyakati za kanisa la kwanza wachawi waliendelea kuwepo. Kulikuwepo mchawi aliyeitwa Simoni aliyekuwa akifanya uchawi katika taifa la Wasamaria(MATENDO 8:9-11). Mchawi mwingine anayetanjwa ni Bar-Yesu au Elima (MATENDO 13:6-8).

» Mungu aliweka sheria kwa lengo la kuwaondosha nyakati hizo (KUTOKA 22:18; MAMBO YA WALAWI 20:27) na akaeleza jinsi watu wake wasivyopaswa KULOGA au kufanya ushirikina na MASHETANI maana hayo ni MACHUKIZO KWA BWANA(MAMBO YA WALAWI 19:26; KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14).

»Watu wengi kwa kujifanya wako juu kiroho hukana kwamba hakuna uchawi kabisa na kufikiri kwamba kufanya hivyo ndiyo kuishikilia imani ya Ukristo.

»Kuwepo kwa uchawi ni jambo lisilopaswa kukanushwa na Mwanafunzi yeyote wa biblià.
Kwa sababu kuwepo kwa uchawi kunatajwa wazi sana katika biblià.

»Hivyo kulogwa ni jambo lililohalisi.

»Mtu aliyeokoka uchawi hauna nguvu kwake kwa sababu yeye ni Yakobo tena ni Israeli (HESABU 23:22-23) pia Mtu aliye OKOKA ana mamlaka ya kupambana na Wachawi na kuwashinda (LUKA 10:19).

JE, WACHAWI WANAKUSUMBUA?
Bila shaka bado hujaokoka, na hata kama umeokoka bado unasitasita lakini leo amua kuokoka kikwelikweli wala usiwe na michanganyo tena na mamlaka ya Ki-Mungu dhidi ya nguvu za shetani itakuwa juu yako.
JE, WEWE NI MCHAWI? Wachawi wote sehemu yao ni katika moto wa milele na milele alioandaliwa Shetani na hao wote wanaomsaidia kazi zake. Hebu achana na uchawi OKOKA sasa.
Fuatisha sala hii sasa iliupokee mamlaka ya Mungu na uwezo wa kuachana na dhambi ya uchawi. Sema " Bwana Yesu, ahsante kwa Neno lako, hakika mimi Sina uwezo wa kuzishinda nguvu za giza nahitaji uniwezeshe, Bwana Yesu futa Jina langu kwenye vitabu vya hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima, nipe uwezo dhidi ya nguvu za giza, niwezeshe kuushinda uchawi , siutaki uchawi kuanzia sasa. Ahsante Yesu kwa kunipa nguvu za kuushinda uchawi katika Jina la Yesu... Amen".

Tafuta kanisa linalohubiri kweli ya neno la Mungu ili uzidi kujifunza zaidi.
 
Hakunaga uchawi duniani tuache kudanganyana na kunyweshana chai kwa visa vya kutunga..Mimi nauhakika hakuna uchawi ndo maana mpaka Leo hii sijawahi kukutana na uchawi..watu wengi wanaoamini Kama Kuna uchawi point yao kubwa huwa wanasema eti kwenye bible imeandikwa kuna uchawi..au wengine wanadai eti karatasi moja iliponyoka kwenye kitabu Cha Mungu ndio inayotumika ulimwenguni kufanyia uchawi.zote hizi sio kweli hakuna uchawi jamani elimikeni acheni kuamini dhana na hadithi za kutunga.hakuna uchawi Mimi nauhakika hakuna mwanadamu ana maajabu ya kutisha kama ambayo tunasimuliwa kwenye visa vya kichawi..mwanadamu uwezo wake mkubwa Ni kuweza kukwepa majanga mfano maradhi na ajali huo ndio uwezo tulionao hakunaga uchawi acheni uwoga wa maisha ndugu zangu.
NDEGE JOHN, wewe unataka kupingana na vitabu vya mungu, uchawi upo ila nguvu ya mungu ni zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakunaga uchawi duniani tuache kudanganyana na kunyweshana chai kwa visa vya kutunga..Mimi nauhakika hakuna uchawi ndo maana mpaka Leo hii sijawahi kukutana na uchawi..watu wengi wanaoamini Kama Kuna uchawi point yao kubwa huwa wanasema eti kwenye bible imeandikwa kuna uchawi..au wengine wanadai eti karatasi moja iliponyoka kwenye kitabu Cha Mungu ndio inayotumika ulimwenguni kufanyia uchawi.zote hizi sio kweli hakuna uchawi jamani elimikeni acheni kuamini dhana na hadithi za kutunga.hakuna uchawi Mimi nauhakika hakuna mwanadamu ana maajabu ya kutisha kama ambayo tunasimuliwa kwenye visa vya kichawi..mwanadamu uwezo wake mkubwa Ni kuweza kukwepa majanga mfano maradhi na ajali huo ndio uwezo tulionao hakunaga uchawi acheni uwoga wa maisha ndugu zangu.
Kwanza ungeelezea huo uchawi nini, ndipo utuambie haupo Duniani.

Mimi naunga mkono hoja yako... siamini katika uchawi. Sema tu ni story za mtaani sometimes zinaogopesha, ndo maana nakua 50 50.. ila mpaka sasa kimoyomoyo bado siamini kama kuna uchawi. Unless unitokee live bila chenga siku moja. Na umri wangu huu wa karibu 40 years sijawahi kuexperience uchawi.. nimeona sanaa ma maigizo mengi lakini uchawi sijawahi. Hivyo kimoyomoyo siamini. Ila kwakua jamii inayonizunguka inaamini, nami mbele za macho yao najifanya naamini but deep inside naona uchawi ni usanii, na story za kutishana tu.
 
Niliamini hakuna uchawi kabla sijampokea Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wa maisha yangu. Nilipoamini(mwaka 2009) ndipo nikasoma habari za uchawi ndani ya biblia. Mwaka 2010, baada ya kuwa natangaza kuwa hakuna mchawi wa kuniweza(kisa nina Yesu), siku moja usiku wa saa nane, nikiwa nimelala, nikasituka baada ya kitu cha baridi kali Sana(sijawahi kugusa au kuguswa na kitu cha baridi kiasi kile kabla) kilipokatiza kwenye nyayo za miguu yote miwili.

Niliamuka baada ya hapo, sikuweza kutembea maana miguu yote ilikuwa imekufa ganzi, baada ya kuomba ndipo miguu angalau ikarejea hali ya kawaida.

Kuanzia hapo, imekuwa ni mchezo wa kuviziana tu. Ukizubaa unalizwa. Na ili wafanikishe kupambana kwao, ndipo wakanitumia bomu lao, ambalo mpaka sasa naishi nalo, ila kulipitisha hawakuja moja kwa moja kwangu, walizungukia kwa mzazi wangu. Hivyo endelea kuandika humu kuwa hakuna uchawi, ila usitangaze. Otherwise hata ukitangaza, kama hauna madhara katika ulimwengu wao, hakuna watakachokifanya kwako.
 
Hakunaga uchawi duniani tuache kudanganyana na kunyweshana chai kwa visa vya kutunga..Mimi nauhakika hakuna uchawi ndo maana mpaka Leo hii sijawahi kukutana na uchawi..watu wengi wanaoamini Kama Kuna uchawi point yao kubwa huwa wanasema eti kwenye bible imeandikwa kuna uchawi..au wengine wanadai eti karatasi moja iliponyoka kwenye kitabu Cha Mungu ndio inayotumika ulimwenguni kufanyia uchawi.zote hizi sio kweli hakuna uchawi jamani elimikeni acheni kuamini dhana na hadithi za kutunga.hakuna uchawi Mimi nauhakika hakuna mwanadamu ana maajabu ya kutisha kama ambayo tunasimuliwa kwenye visa vya kichawi..mwanadamu uwezo wake mkubwa Ni kuweza kukwepa majanga mfano maradhi na ajali huo ndio uwezo tulionao hakunaga uchawi acheni uwoga wa maisha ndugu zangu.
Kweli nakuunga mkono huwa nabishana sana na watu kuhusu hili. HAKUNA UCHAWI, uchawi ni mind yako hafifu. Yaani akili inaona maluwe luwe we unatuambia uchawi, kumbe afya ya akili ni mbaya na inakuathiri kwenye mambo mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi ni dhana ya kijinga na haupo. Hata Mungu hayupo..! Mfumo wa dini uliwekwa kuwatia uoga watu,kuepusha maafa km kuuana,kuibiana,uzinzi nk. Kwa kuwafanya watu wawe waoga kuyatenda hayo wakihofia kwenda motoni.

Uchawi ni ujinga na ndo maana unaaminiwa na wajinga. Ukiona mtu anaamini uchawi huyo automatically ni mjinga. Mungu mwenyewe pia hayupo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawazo
Uchawi ni dhana ya kijinga na haupo. Hata Mungu hayupo..! Mfumo wa dini uliwekwa kuwatia uoga watu,kuepusha maafa km kuuana,kuibiana,uzinzi nk. Kwa kuwafanya watu wawe waoga kuyatenda hayo wakihofia kwenda motoni.

Uchawi ni ujinga na ndo maana unaaminiwa na wajinga. Ukiona mtu anaamini uchawi huyo automatically ni mjinga. Mungu mwenyewe pia hayupo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakunaga uchawi duniani tuache kudanganyana na kunyweshana chai kwa visa vya kutunga..Mimi nauhakika hakuna uchawi ndo maana mpaka Leo hii sijawahi kukutana na uchawi..watu wengi wanaoamini Kama Kuna uchawi point yao kubwa huwa wanasema eti kwenye bible imeandikwa kuna uchawi..au wengine wanadai eti karatasi moja iliponyoka kwenye kitabu Cha Mungu ndio inayotumika ulimwenguni kufanyia uchawi.zote hizi sio kweli hakuna uchawi jamani elimikeni acheni kuamini dhana na hadithi za kutunga.hakuna uchawi Mimi nauhakika hakuna mwanadamu ana maajabu ya kutisha kama ambayo tunasimuliwa kwenye visa vya kichawi..mwanadamu uwezo wake mkubwa Ni kuweza kukwepa majanga mfano maradhi na ajali huo ndio uwezo tulionao hakunaga uchawi acheni uwoga wa maisha ndugu zangu.
Tawile[emoji1657]

wali nazi maharage nazi
 
Back
Top Bottom