Kamasikosei alikua akiitwa Majambo, kwahakika yule alikua ni kiboko ya watoto, maana kile kinyago changozi na yale meno sijui yalikuwa ya mnyama gani, kichwani anafunga manyoya ya ndege, sura ya kile kinyago ilitishasana watoto.
Na yule jamaa alikua anazunguka karibu DSM yote kwa nyakati tofauti. Ukiacha uuzaji wa karanga ilikua mteja unatoa fedha ili yeye aimbe na kucheza. Mkono mmoja ana manyanga mkono mwingine ameshika kapu la karanga, kifuani amevaa ngozi sijui ya mnyama gani, usoni amevaa kinyago cha ngozi chenye meno ya kutisha.
Ile ilikua miaka ya 80 ni kitambo kidogo. Enzi za mwanafunzi kulipa sent hamsini/thumni kwenye uda. Uwanja wa taifa kuna mlango wa kuingia watoto/wanafunzi kuangalia mpira kwa shilingi tano.
Dar ilikua haina foleni kama leo. Bustani za mnazi mmoja ilikua sehemu ya watu kupumzika, Kwenye uzio wa ikulu mnakwenda kuangalia ndege na wanyama. Dar ilikua haina Joto kama ilivyo sasa. Mleta mada umenikumbusha mbali.