Mnamkumbuka mzee Magambo?

Mnamkumbuka mzee Magambo?

No Escape

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2016
Posts
6,663
Reaction score
7,827
wahenga mliokaa maeneo ya Dsm hasa kinondoni,huyu mzee hamuwezi kumsaha.kipindi hicho mtoto km hataki kuoga au kula we mwambie mzee magambo yupo mlangoni utamkuta bafuni anakusubiri na mlango kaufunga Dah! raha sana
 
Nipo group flan huko Whassap kuna huyo Mzee Magambo anashusha material ya kilimo cha mazao na mbogamboga sasa sijui ndio yeye!!!
 
Mi mzee magambo nayemfaham alikuwa anatengeneza makochi
 
Nadhani mleta uzi ulitakiwa kuspecify kuwa huu uzi ni wa watu walioishi kinondoni enzi hizo unazosema, ingekuwa vizuri zaidi.....By the way ngoja wanaomjua mzee Magambo waje.
 
Alikuwa maarufu sana watoto wengi nikiwemo na Mimi tulikuwa tukimuogopa,alikuwa akiuza Karanga kwenye Kikapu sambamba na kuimba alikuwa akivalia kiasili,,,nimegundu humu jf wengi ni watoto ama ni mangosha yamekuja mjini wamekula idi mbili tatu afu wanasumbua
 
Yap tupo wa kinondonino toka enzi ya lang'ata,tazara na vijana kabla Biafra hawajaiharibu
 
Alikuwa maarufu sana watoto wengi nikiwemo na Mimi tulikuwa tukimuogopa,alikuwa akiuza Karanga kwenye Kikapu sambamba na kuimba alikuwa akivalia kiasili,,,nimegundu humu jf wengi ni watoto ama ni mangosha yamekuja mjini wamekula idi mbili tatu afu wanasumbua
Pumba. Vuuu unahisi kila mtu amekulia mtaani kwenu
 
Mzee magambo alikuwa anauza karanga na kutoa burudani fupi, kibwagizo chake anakutisha na sura yake na yale mavazi yake duu. Utoto balaa eti tulikuwa tunamuogopa. Enzi zetu Kariakoo ya zamani.
 
Alikuwa maarufu sana watoto wengi nikiwemo na Mimi tulikuwa tukimuogopa,alikuwa akiuza Karanga kwenye Kikapu sambamba na kuimba alikuwa akivalia kiasili,,,nimegundu humu jf wengi ni watoto ama ni mangosha yamekuja mjini wamekula idi mbili tatu afu wanasumbua
Afadhali bro. umeongea point,hakuna mtu wa Dsm asiyemjua magambo watu wanajifanya kujua halafu kumbe ni wakuja tupu.
 
Nadhani mleta uzi ulitakiwa kuspecify kuwa huu uzi ni wa watu walioishi kinondoni enzi hizo unazosema, ingekuwa vizuri zaidi.....By the way ngoja wanaomjua mzee Magambo waje.
we km mpaka leo hujajua kam kinondoni ndio Dsm sijui wa wapi? hivi jambo gani lifanyike kinondoni wana Dsm wasilijue.
 
Mzee magambo alikuwa anauza karanga na kutoa burudani fupi, kibwagizo chake anakutisha na sura yake na yale mavazi yake duu. Utoto balaa eti tulikuwa tunamuogopa. Enzi zetu Kariakoo ya zamani.
wengine walikuwa bado wananyonya halafu wanasingizia hbr za facebook.
 
Kamasikosei alikua akiitwa Majambo, kwahakika yule alikua ni kiboko ya watoto, maana kile kinyago changozi na yale meno sijui yalikuwa ya mnyama gani, kichwani anafunga manyoya ya ndege, sura ya kile kinyago ilitishasana watoto.
Na yule jamaa alikua anazunguka karibu DSM yote kwa nyakati tofauti. Ukiacha uuzaji wa karanga ilikua mteja unatoa fedha ili yeye aimbe na kucheza. Mkono mmoja ana manyanga mkono mwingine ameshika kapu la karanga, kifuani amevaa ngozi sijui ya mnyama gani, usoni amevaa kinyago cha ngozi chenye meno ya kutisha.

Ile ilikua miaka ya 80 ni kitambo kidogo. Enzi za mwanafunzi kulipa sent hamsini/thumni kwenye uda. Uwanja wa taifa kuna mlango wa kuingia watoto/wanafunzi kuangalia mpira kwa shilingi tano.

Dar ilikua haina foleni kama leo. Bustani za mnazi mmoja ilikua sehemu ya watu kupumzika, Kwenye uzio wa ikulu mnakwenda kuangalia ndege na wanyama. Dar ilikua haina Joto kama ilivyo sasa. Mleta mada umenikumbusha mbali.
 
Alikuwa maarufu sana watoto wengi nikiwemo na Mimi tulikuwa tukimuogopa,alikuwa akiuza Karanga kwenye Kikapu sambamba na kuimba alikuwa akivalia kiasili,,,nimegundu humu jf wengi ni watoto ama ni mangosha yamekuja mjini wamekula idi mbili tatu afu wanasumbua
Wewe ukadhani dsm wote tumekulia ushwazi..??? Kuna mtu hajawahi panda daladala hapa dsm..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom