Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
844
Mambo vipi wanajamii.

Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.

Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.

Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.
 
Mimi sikwepo enzi zenu ila ntaweka niliyowahi yasikia

Continental ..the quality to talk about.
Startimes...ulimwengu wa digitaliiiii
Vodacom...kazi ni kwako..power to you.

Fountain view academy ni kisima cha mafanikio..hili nalipenda hadi kesho.
Je unamaumivu flue..je unamaumivu ya kichwa..Tumia dawa tatu. Mimi natumia dawa tatu wewe je?

Attentiiiiion!!!nimelazimika kutangaza vita dhidi ya wadudu wote warukao na watambaaaooo. Tangazo la Rungu

Airtel..babalao
Tigo...express your self
Buzz...buzz ni bomba
Cloud's fm tunakufungulia dunia.
Tembomaster card. ATM crdb
Wakwe: kijana unakazi?
Kijana: kazi ninayo mzee
Wakwe: je unanyumba?
Kijana: nyumba ninayo mzee
Mkwe: una gari?
Kijana: gari ninalo gx 100
Mkwe: je unayo Tembomaster card?
Kijana : mmmh eeeh aaa hiyo mzee eeeh
Mkwe : kijana katika ulimwengu huuu huna Tembomaster card unataka kumchukua binti yetu aaa aaaa
 
Gazeti Alasiri...kila siku Alasiri...kwa bei nafuu...Shilingi Mia Moja tuu...Kwa habari motomoto, za Kimataifa, Biashara na Michezo...Usilikose gazeti Alasiri.
Kulikuwa na alasiri na kama sikosei na lile la dar Leo vile vile kuna moja lile lilikuwa katuni mwanzo mwisho watawala wakalifungia hata sababu Hamna lilikuwa linaitwa Sanifu
 
Back
Top Bottom