Mnakumbuka Enzi hizo?????

Hapo sasa kwenye kutafuta kipenyo...............kichwa kilkuwa kinauma............lakini siku hizi hata ukiniamsha usiku wa manane nakokotoa kipenyo mpaka unashangaa.

BTW Nimekumbuka wimbo;

Mabata madogomadogo yanaogelea yanaogelea katika shamba zuri la bustani
Yanapenda kutembea bila viatu....bilaaa ..bila viatu katika shamba zuri la bustaniii
 
Enzi hizo wanafunzi mnagaiwa kila kitu shuleni..
kuanzia madaftari ya masomo yote,hadi penseli na peni.

Wapi hizi huduma siku hizi???

Labda hizi shule za academia, kule ununio na mavurunza primary hakunaga hii tena.

 

DA like this blue
 
Safi. Nlidhani ungesema tookn't she?? Manake kulikuwa na balaa darasani kwetu, acha tu.


Ha ha ha ha nakumbuka tukiwa darasa la tatu ndo tunaanza kusoma kiingishi mambo ya kusebu mpaka 10, 20, 30 mpaka mia kwa kiingilishi kuna msichana alikuwa anahesabu 1-20, kufika eleven ilikuwa mbinde si akahesabu vizuri kufika 11 akasema ten one, ten two na kuendelea sitasahau mpaka leo
 


Hahahahahah huyo alikuwa kiboko lol......ten one.....daaah! Waalimu wana kazi sana!
 

Sasa sisi kuna huyo mwalimu wetu mmoja alituuliza tunda la kokomanga linaitwaje kwa kiinglish, mpk tunamaliza shule hamna aliyemjibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…