Hii nimeitoa hukooooo.....Kuna mtu kapendekeza. Mimi pia imenivutia. Hebu sema lolote!!!
Imependekezwa kama ifuatavyo:
CHAMA CHENYEWE:
Mwenyekiti: Freeman Aikael Mbowe
Makamu Mwenyekiti Bara: Prof. Abdalah Safari
Makamu Mwenyekiti Zanzibar: Issa Issa Mohamed
Katibu Mkuu: Dr. Willbrod Peter Slaa
Naibu Katibu Mkuu Bara: Tundu Antiphas Lissu
Naibu Katibu Mkuu Zanzabar: Hamad Yusuph
Habari na Uenezi: John Mnyika
JUMUIYA ZA CHAMA:
BAWACHA:
Mwenyekiti: Halima Mdee
Makamu Mwenyekiti: Suzan Kiwanga/ Mhe. Maryam Msabaha/ Rose Mayemba
Katibu: Paulina Gekul/Naomi Kaihula
BAVICHA:
Mwenyekiti: Ben Saanane
Makamu Mwenyekiti: Atoke Zanzibar
Katibu: Mohamed Mtoi
BARAZA LA WAZEE:
Mwenyekiti: Mzee Sylivester Masinde
Makamu Mwenyekiti: Mzee Peter Mpema (Kata ya Somangira, Tawi la Kizani - Kigamboni)
Katibu: Prof. Mwesiga Baregu
NB: Nimelazimika kupendekeza Mhe. Tundu Lissu awe Naibu Katibu Mkuu wa Chama upande wa bara kwa sababu sioni tofauti iliyopo baina ya Mkurugenzi wa Sheria na Mwanasheria wa Chama. Akiwa kama Naibu Katibu Mkuu aweza pia kufanya kazi za kisheria zinazihusu chama kama wafanyavyo Mabere Marando na Prof. Abdalah Safari.
Aidha, safu yangu hii niliyopendekeza nimezingatia Changamoto ambazo CHADEMA imekuwa ikipitia na pengine itaendelea kupitia hasa masuala ya Propaganda za Ukanda na Udini.
Zaidi mapendekezo yangu yamejikita katika watu wenye nguvu na ushawishi kwa Umma wa Watanzania. Mapendekezo yangu yamelenga sana kwamba hii Safu mpya ya Uongozi kila mtu awe na uwezo wa kupanda jukwaani na kutema cheche. Tunakubalina kimsingi kuwa watu tuna vipaji tofauti. Wakati wengine wana kipaji cha kaundika na kusoma maandishi, wengine wana vipaji vya kuyaongea hayo maandishi na kuyanakshi vizuri na yakaeleweka miongoni mwa wasikilizaji. Hao wote niliowapendekeza bila shaka mtakubaliana nami kuwa ni waongeaji wazuri katika majukwaa.
Tunataka BAWACHA yanye Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na Katibu machachari kwelikweli. BAWACHA itakayotembea nchi nzima kuwaamsha akina mama ndani ya miezi tisa hadi kumi baada ya uchaguzi na kuzindua Vuguvugu mbalimbali kama ambavyo Conchester Rwamlaza anafanya kule Mkoani Kagera au kule Mkoani Geita kwa Kamanda Husna Amri. Tunataka wanawake waamke kwa vyovyote vile.
Tunataka BAVICHA itakayouwaunganisha vijana. BAVICHA itakayoendelea kuvutia wasomi zaidi. BAVICHA itakayowashawishi, wasomi wetu baada ya kumaliza vyuo vikuu wale wenye interest na siasa wakagombee kwenye maeneo yao kuanzia Udiwani. BAVICHA itakayokwenda kupata vijana kuanzia Shule za Msingi, Sekondari ya Kati na juu hadi vyuo vya Ufundi....Hapa ndio maana BEN SAANANE anatakiwa kuongoza jahazi hili
Tunataka BARAZA LA WAZEE wenye hekima na msimamo. Wazee walio tayari kukifia Chama. Hapa Mzee Sylivester Masinde na Katibu akiwa Prof Baregu nina hakika CHADEMA 2015 Ikulu itakuwa nyeupe kupitia washirika wetu wa CUF, NCCR, DP na NLD
Aluta Continua