Mapendekezo yako si mabaya kwani huo ni mtazamo wa mtu, na hii inaonyesha jinsi CHADEMA ilivyo na rasilimali watu wa kutosha ndani ya chama, na hii inaonyesha ni jinsi gani Mbowe na Dr Slaa uongozi wao ulivyo thabiti na mafanikio makubwa katika kuliongoza jahazi, kwa mtazamo wangu, nafasi ya naibu katibu mkuu na makamu mwenyekiti, zinahitaji watu wafia chama watakaoongeza nguvu wakishirikiana na Mbowe na Dr Slaa tofauti na ilivyo sasa, hapa nafikili kwa nafasi ya naibu katibu mkuu watu kama kamanda Lema, kamanda Mnyika, kamanda Msigwa wanafaa kabisa, kwa Tundulisu nafikili uanasheria mkuu ni mahali pake, hakuna haja ya kumuongezea majukumu mengine, na ili tufike salama, Mbowe na Dr Slaa waendelee na nyadhifa zao, tusikubali kupangiwa uongozi na maccm wakishirikiana na msajili wa vyama, wao wanajua wanatuposha, kumbe wanazidi kutufumbua macho na kuuona uimara wa uongozi wao, kiongozi mzuri ni lazima achukiwe na maccm, kwa sababu wanashindwa kuwarubuni.