Hii nimeitoa
hukooooo.....Kuna mtu kapendekeza. Mimi pia imenivutia. Hebu sema
lolote!!!
Imependekezwa kama ifuatavyo:
CHAMA CHENYEWE:
Mwenyekiti: Freeman Aikael Mbowe
Makamu Mwenyekiti Bara: Prof. Abdalah Safari
Makamu Mwenyekiti Zanzibar: Issa Issa Mohamed
Katibu Mkuu: Dr. Willbrod Peter Slaa
Naibu Katibu Mkuu Bara: Tundu Antiphas Lissu
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar: Hamad Yusuph
Habari na Uenezi: John Mnyika
JUMUIYA ZA CHAMA:
BAWACHA:
Mwenyekiti: Halima Mdee
Makamu Mwenyekiti: Suzan Kiwanga/ Mhe. Maryam Msabaha/ Rose Mayemba
Katibu: Paulina Gekul/Naomi Kaihula
BAVICHA:
Mwenyekiti: Ben Saanane
Makamu Mwenyekiti: Atoke Zanzibar
Katibu: Mohamed Mtoi
BARAZA LA WAZEE:
Mwenyekiti: Mzee Sylivester Masinde
Makamu Mwenyekiti: Mzee Peter Mpema (Kata ya Somangira, Tawi la Kizani -
Kigamboni)
Katibu: Prof. Mwesiga Baregu
NB: Nimelazimika kupendekeza Mhe. Tundu Lissu awe Naibu Katibu
Mkuu wa Chama upande wa bara kwa sababu sioni tofauti iliyopo baina ya
Mkurugenzi wa Sheria na Mwanasheria wa Chama. Akiwa kama Naibu Katibu
Mkuu aweza pia kufanya kazi za kisheria zinazihusu chama kama wafanyavyo
Mabere Marando na Prof. Abdalah Safari.
Aidha, safu yangu hii niliyopendekeza nimezingatia Changamoto ambazo
CHADEMA imekuwa ikipitia na pengine itaendelea kupitia hasa masuala ya
Propaganda za Ukanda na Udini.
Zaidi mapendekezo yangu yamejikita katika watu wenye nguvu na ushawishi
kwa Umma wa Watanzania. Mapendekezo yangu yamelenga sana kwamba hii
Safu mpya ya Uongozi kila mtu awe na uwezo wa kupanda jukwaani na
kutema cheche. Tunakubalina kimsingi kuwa watu tuna vipaji tofauti.
Wakati wengine wana kipaji cha kaundika na kusoma maandishi, wengine
wana vipaji vya kuyaongea hayo maandishi na kuyanakshi vizuri na
yakaeleweka miongoni mwa wasikilizaji. Hao wote niliowapendekeza bila
shaka mtakubaliana nami kuwa ni waongeaji wazuri katika majukwaa.
Tunataka BAWACHA yanye Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na Katibu
machachari kwelikweli. BAWACHA itakayotembea nchi nzima kuwaamsha akina
mama ndani ya miezi tisa hadi kumi baada ya uchaguzi na kuzindua
Vuguvugu mbalimbali kama ambavyo Conchester Rwamlaza anafanya kule
Mkoani Kagera au kule Mkoani Geita kwa Kamanda Husna Amri. Tunataka
wanawake waamke kwa vyovyote vile.
Tunataka BAVICHA itakayouwaunganisha vijana. BAVICHA itakayoendelea
kuvutia wasomi zaidi. BAVICHA itakayowashawishi, wasomi wetu baada ya
kumaliza vyuo vikuu wale wenye interest na siasa wakagombee kwenye
maeneo yao kuanzia Udiwani. BAVICHA itakayokwenda kupata vijana kuanzia
Shule za Msingi, Sekondari ya Kati na juu hadi vyuo vya Ufundi....Hapa
ndio maana BEN SAANANE anatakiwa kuongoza jahazi hili
Tunataka BARAZA LA WAZEE wenye hekima na msimamo. Wazee walio tayari
kukifia Chama. Hapa Mzee Sylivester Masinde na Katibu akiwa Prof Baregu
nina hakika CHADEMA 2015 Ikulu itakuwa nyeupe kupitia washirika wetu wa
CUF, NCCR, DP na NLD
Aluta Continua