Mnada mnada mnada

Mnada mnada mnada

Duu alikuwa mtemi kiasi hicho? Alikuwa na mume kweli???

Kwa kweli sifahamu ila si unajua tena rafiki utemi nje akiwa ndani anabaki kuwa mama na heshima inachukua nafasi yake kwa mzee
 
Usiogope, kuna magari mengi tu huko barabarani unapishana nayo hayana power sterling ila yanaendeshwa kinamna unaweza ukafikiri malaini

Mkuu hii ngoma babu alikuwa nayo inaenda bush kubeba mpunga ikirudi babu mpaka kavua shati
 
Mkuu usimshushe hadhi yule alikuwa Mmama na bisu (kisu) lake kachomeka kwenye kitenge, halafu hataki mtu aning'inie akisema Mara ya kwanza ya pili anasimamisha gari anateremka anakufuata, sasa hivi atakuwa mtu mzima sana

Mkuu inawezekana ulikuwa unasoma mbagala kizuiani au mbagala rangi tatu ya enzi hizo....
 
Limefanana na mbunge mmoja alikuwa anasinzia sana bungeni
 
Mkuu mshana jr upo deep kwenye issue za Magari kuliko kule kwingine ambako huishia kugombana tu watu.

Eti rangi "mkono mmoja"

Hahaha ndio wanavyodanganyana gereji za vichochoroni, binafsi sijawahi kuona rangi mkono mmoja kwakuwa kuna primer/undercoat, primary coat, over coat au clear coat
 
Last edited by a moderator:
Mkuu inawezekana ulikuwa unasoma mbagala kizuiani au mbagala rangi tatu ya enzi hizo....

Hapana Mkuu, Mama siku moja moja alikuwa anapiga Mwenge Kariakoo, nilimshuhudia siku moja Morocco abiria alikuwa mdogo kama sisimizi kisa kirefu tuishie hapo
 
Hii ngoma ya bb cha ng'ombe enzi ya80's.Waliopo kampuni dada Kassam transport wanamind mzuka.

kassam transport!! ha ha ha ole wako ubadili njia! enzi hizo kalikuwepo ka bibi ndo kasimamizi ka kila kitu! Leyland fomoko!!!
 
Alikuwa mama wa Kinyakyusa, alianza kwanza na Mbaura za Zambia kabla yankuja kwenye UDA

ahaaa....mkuu uko vizuri....mama likuwa akikaa kwenye kiti chake anaenea vilivyo......

Zamani hizo kaka, kilikuwa ni kipande cha mama

Ahahahahaaa jamani mmenikumbusha mbali kama namuona vile, mtu hata alewe namna gani akipanda gari ya Mama pombe inaisha hadi ateremke ndio inarudi.
 
Back
Top Bottom