Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,709
Hii ni kwa wote tunaotumia hili jukwaa!Hivi kwa mfano akatokea mtu mmoja kule Chile anajua kiswahili vizuri,akafungua JF na kuja hapa kwenye jukwaa hili,hizi mada zote zilizoko humu zinaendana na jukwaa?Pili michango tunayotoa iko ndani ya mada?Hiyo michango itamfanya ajue uwezo wetu wa kufikiri,atagundua nini?Yaani michango yetu imawakilisha watu walio karne 21?Atatutazamaje na ataionaje Tanzania katika suala zima la kutatua na kupambana na changamoto za kijamii?Maana sisi tulioko humu tunaiwakilisha nchi,namna tunavyotoa mada na kuchangia ndo tunajieleza namna tunavyofikiri na kuyaona mambo!TUJIULIZE!