Mmmh Mvuto Nao!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmmh Mvuto Nao!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Oct 18, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Bristol umebaina kwamba mwanaume au mwanamke akiutwika huwaona wengine wanavutia sana.
  Mwanaume huona wanawake wanavutia na ni warembo kwelikweli, na wanawake huona wanaume ni handsome wa nguvu.
  Pombe zikimtoka Guess what? ............................

  Tume ya uchaguzi hapa Canada mwaka 1974 iligundua kwamba wagombea uchuguzi wenye sura zinazovutia walipata kura mara mbili na nusu ya wale ambao sura zao zilikuwa za kutisha hasa pale wanapolingana uwezo.
  Hivi hii Tanzania haijawahi kutokea watu wakampigia kura mgombea kwa ushindi wa Tsunami? Maisha bora kwa kila mtanzania
  Sura inayovutia acha kabisa!

  Mwanamke anapotumia pills husababisha kupunguza uwezo wa kunusa, hii inatokana na utafiti uliofanywa a chuo kikuu cha Liverpool kwa wanawake kunusa (sniff) mashati 100 ya wanaume.
  Kawaida mwanamke huvutiwa na mwanaume tofauti na genetics zake (harufu tofauti).
  Hawa nao kazi kwelikweli, inamaana walikuwa wananusa vikwapa?????

  Tafiti za kisayansi zinasema si binadamu wote huvutiwa na binadamu wengine, inasemakana kuna binadamu ambao huvutiwa na vitu wala si wanyama bali vitu visivyo na uhai.
  Hawa watu huweza kusisimka, kupenda (fall in love) na pia huwa committed kuishi navyo au kuishi hapo vilipo.
  Eija-Riita Berliner-Mauer yeye ameolewa na ukuta wa Berlin tangu mwaka 1979.

  Duniani kuna vituko!

  Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Pennsylvania mwaka 1980 waligundua kwamba watuhumiwa waliokuwa wanavutia sura zao walipata adhabu laini zaidi ukilinganisha na watuhumiwa wenye sura zilizikuwa zinatisha.
  Yaani kwa sura nzuri wanakuhurumia?

  Wanawake wanapojipamba sana kwa vipodozi huweza kupunguza uwezo wa wanaume kuvutiwa nao hasa wakiwa wapo fertile.
  Wanawake huwa na aina ya harufu (scent) ambayo huvutia wanaume hasa mwanamke anapokuwa kwenye siku za ovulation.
  Kama hutaki kusumbuliwa na wanaume basi ukiwa fertile siliba vipodozi (makeup) vya nguvu finish!


  Unavyojionesha kwa mara ya kwanza ni muhimu sana (first impressions).
  Wengi huweza kutoa uamuzi wa mwenzake kuwa partner hasa kutokana na alivyojieleza dakika 4 za kwanza kuonana.
  Siyo kujieleza maneno tu bali ni vitendo vya mwili unapoongea, maneno unayoongea na sauti unayoongea.
  Maneno unayoongea kwa mara ya kwanza huvutia asilimia 7 tu, vitendo vya mwili unapoonga (body language) ni asilimia 55 na aina ya sauti na jinsi unavyoongea ni asilimia 38.

  Je, unadhani mpenzi wako alikuvutia kitu gani siku ya kwanza ulipokutana naye?

  Weekend Njema!
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  duh hii kali.....mie kusema kwelj chakwanza kjnivutia ni sura bwana na baada ya hapo ni matiti yake.
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  mh! siku ya kwanzaaaa.....nilichezea mitama na ngumi za kutosha baada ya kumkonyeza baada ya hapo nikazama kabsaaa baada ya kujua ni mjeshi.....she was special!!!!
   
 4. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tafiti zingine bwana!!!!!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  Haaaa siku ya kwanza sikumuongelesha kitu hadi akabebwa lakini skufa moyo
   
Loading...