Mmiliki wa FB ananufaikaje ?

Pishoni

Member
Jan 31, 2013
33
24
Habari! jamani naomba mnieleweshe kidogo au kwa mapana yake katika hili. Napenda kujua ni kwa namna gani Mmiliki wa facebook anavyonufaika? mfano kwa mimi mtumiaji wa kawaida mbaye huweka kifurushi changu cha MB 100 na kuanza kuperuzi fb,

yani huyo mmiliki ananufaikaje kwa mimi kufanya hivyo? . Kuna mtu aliniambia kuwa anapata faida kutokana na matangazo lakini nikajaribu kuwaza mbona mi nikiweka tangazo langu fb sidaiwi au ni kwa yale makampuni makubwa kama samsung,mitandao ya simu,etc. Naomba mnipe knowledge hapo jamani! Asante.
 
Matangazo ukitaka sasa kucustomize tangazo lako mfano lionekane kwa watanzania au watu wote walioko Dar unatengeneza ad unalilipia kwa credit card kwa hiyo watu wa dar wakifungua tu wanaliona.

Hayo matangazo unayoweka wanaona marafiki zako tu au watu wanakufollow hayo hulipii. Sasa mpango mwingine ni siku moja akiamua akishakuw na watumiaji wengi amue tu achanyi Tshs 1000 kwa mwaka mahela kibao.

Mimi nilijaribu kuweka moja la dolla 7 kwa wiki sikupata return ninayotaka ila kuanzia ya $ 50 kwa wiki inaonekana watu watakutambua na mengine yapo ya kila atakayeclick tanganzo unachajiwa sasa hili akijua mpinzani wako wa biashara anaweza kutuma watu waclick lakini hamna result hela inatoka kwako inaenda FB.

Hayo ni machache ninayojua Ahsante
 
Back
Top Bottom